settings icon
share icon
Swali

Nini kinafaa kufanywa ikiwa mume na mke hawakubaliani juu ya kutoa fungu la kumi / kiasi gani wanafaa kutoa?

Jibu


Wakati mume na mke hawakubaliani juu ya "kutoa zaka" au kwa kiasi gani cha kutoa kwa kanisa la mahali na huduma zingine, ugomvi unaweza kujibuka. Kwanza, ni muhimu kuelewa kwamba Wakristo chini ya Agano Jipya hawana wajibu wa kutoa sehemu 10 ya mapato yao. Mungu alianzisha zaka kwa Israeli katika uchumi wa Agano la Kale. Toleo la fungu la kumi lilikuwa hata kabla ya sheria kutolewa (Mwanzo 14:20), na Mambo ya Walawi 27:30 inasema kwamba watu walipaswa kutoa zaka ya ardhi, mbegu au matunda ya miti kwa kuwa yote ni ya Bwana. Katika Kumbukumbu la Torati 14:22, Musa anawaambia watu kwamba Mungu anasema, "Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka." Watu wa Israeli walipaswa kuleta sehemu ya kumi ya ongezeko lao wote na kumrudishia Bwana. Zaka ziliunga zilizaidia kazi katika hema ya Bwana na baadaye hekalu pamoja na ukuhani.

Leo, zaka zetu na sadaka ni sadaka za upendo tunayompa Mungu kwa shukrani kwa baraka ambazo tunapokea kama watoto Wake. Hatuko chini ya sheria ya uchumi wa Agano la Kale lakini katika wakati wa neema. Zaka zetu na sadaka ni njia ya kuunga mkono kazi ya Mungu katika makanisa yetu ya ndani pamoja na juhudi za kimisionari.

Tunapomtolea Bwana, tunapaswa kutoa kwa moyo wenye furaha. "Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu. Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu" (2) Wakorintho 9: 6-7). Kutoa kwa kulazimishwa au kutoa ili kuunda kitu ambacho kimekosekana hakutatusaidia kiroho, wala hakutaleta baraka kwa familia.

Kwa amri ya Mungu, mume na mke ni mwili mmoja (Marko 10: 8). Kwa kweli, mume na mke wanapaswa kuzungumza utoaji wao na kuafikia makubaliano ya pande zote juu ya kiwango cha kutosha na maeneo sahihi ya kutoa kulingana na kanuni za kibiblia. Ikiwa kuna kutofautiana juu ya kutoa, mke hastahili kupuuza mamlaka ya mumewe na kutoa kwa niapa yake au kujaribu kumzuia kutoa. Katika kufanya hivyo, mke huchukua mamlaka ya uongozi (Waefeso 5: 22-33) juu yake mwenyewe, na hiyo ni nje ya amri ya Mungu. Vivyo hivyo wanawake wanapaswa kutembea kwa kutii amri ya Mungu na kujiwasilisha Kwake (Waefeso 5:22). Vivyo hivyo, waume wanapaswa kujiwasilisha kwa Mungu na kuwapenda wake zao bila kujitegemea (Waefeso 5: 22-33). Mume anapaswa kuzingatia mchango wa mke wake na mwisho kufuata uongozi wa Bwana. Ikiwa mume au mke si muumini, kanuni hizo zinatumika. Mume, kama kichwa cha familia, huwa na jukumu la mwisho kwa maamuzi kuhusu kutoa.

Kunyenykea kwa amri ya Mungu kuleta baraka na neema ya kusimama katika imani. Mungu ana njia ya kupata mambo kufanyika, na tunaweza kusimama kwa uaminifu na kuangalia bila kujishughulisha wenyewe na kile tunachoona kama kibaya. Katika Samweli 1 tunaona kanuni hii ya milele: "Naye Samweli akasema, je! Bwana huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya Bwana? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu"(1 Samweli 15:22).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Nini kinafaa kufanywa ikiwa mume na mke hawakubaliani juu ya kutoa fungu la kumi / kiasi gani wanafaa kutoa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries