settings icon
share icon
Swali

Harusi ya Kikristo inapaswa kuwa tofauti na harusi isiyo ya Kikristo ki vipi?

Jibu


Tofauti ya msingi kati ya harusi ya Kikristo na harusi isiyo ya Kikristo ni Kristo. Wakristo ambao wanaolewa wanajitolea kwa Kristo,na vile vile kwa kila mmoja, na ahadi hiyo inapaswa kuwa dhahiri kwa kila mtu anayehudhuria harusi hiyo. Katika harusi isiyo ya Kikristo, wanandoa-hasa bibi harusi-huwa ni sehemu ya msingi. Katika harusi ya Kikristo, Kristo ndiye kipaumbele.

Wanandoa Wakristo ambao wanataka kumtukuza Kristo kwa njia ya harusi yao wanaweza kuanza na maandalizi mapema, na kuanza kwa ushauri wa Kibiblia wa kabla ya ndoa na mchungaji wao. Ushauri wa kabla ya ndoa kulingana na kanuni za kibiblia zinaelezea majukumu ya mume na mke kama wanavyohusiana na watoto wao wanaotazamiwa (Waefeso 5: 22-6: 4; Wakolosai 3: 18-21). Harusi inathibitisha mbele ya Mungu na marafiki na familia kwamba hamu ya wanandoa ni kuishi kulingana na mpango wa Mungu kwa familia.

Sherehe ya harusi inapaswa pia kuwa mfano wa kujitolea kwa wanandoa kwa utukufu wa Yesu Kristo. Kila sehemu ya huduma, kutoka kwa muziki hadi maadili kwa ujumbe uliotolewa na msimamizi, inapaswa kutafakari ahadi hiyo. Muziki unapaswa kuwa wa heshima na Kristo-kuheshimu, sio wa kidunia. Ahadi au zile vidokezo vinapaswa kuchukuliwa na kuelewaka kamili kwa wanandoa kwamba maneno wanayoyazungumza yanajumuisha ahadi ya maisha na kwa ujuzi kwamba wanaoahidiana, wanaahidi pia Mungu. Ujumbe uliotolewa na mchungaji unapaswa kuonyesha ukweli huu na kujitolea.

Wanandoa Wakristo wanapaswa kuchagua wahudumu wao kwa makini na wakitilia maananani kujitolea kwao kwa Kristo. Wafanyakazi wa kike na wavulana hawahudhurii tu kwa ajili ya mavazi ya sherehe. Uwepo wao unathibitisha makubaliano yao na ahadi yao ya kuunga mkono, ahadi ya wanandoa kumheshimu Kristo katika ndoa yao. Pamoja na hayo, nguo ya bi harusi na mavazi ya wanawake ambao wanasimamia haursi yanapaswa kuwa sahihi kwa kusimama mbele ya Mungu. Hakuna nafasi ya mavazi, yasiyo na heshima katika sherehe inayoheshimu Kristo.

Ikiwa kuna mapokezi au sherehe ya baada ya harusi, inapaswa kuwa inaheshimu Kristo. Ingawa jamaa wasio Wakristo mara nyingi uhudhuria ndoa za Kikristo na sherehe baadaye, kuandaa pombe kwenye sherehe ya Kikristo huwapa wasioamini ujumbe usio sahihi, ujumbe unaosema kuna tofauti finyu sana kati ya wale wanaomcha Mungu na wale amabao hawamchi Mungu .Hata kama waumini ambao hupanga harusi hawaoni chochote kibaya na kunywa pombe , na wa hunywa pombe kwa dhamiri safi, Wakristo wengine wanaweza kusumbuliwa na kuwepo kwa pombe, na hatupaswi kutumia uhuru wa kufanya jambo na kusababisha mtu yeyote kuanguka.

Wanandoa ambao wanafanya harusi ya kuheshimu Kristo watakumbuka uzuri na umakini wa harusi hio kwa maisha yote na watapata njia nzuri ya kuanza maisha yao pamoja.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Harusi ya Kikristo inapaswa kuwa tofauti na harusi isiyo ya Kikristo ki vipi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries