settings icon
share icon
Swali

Je, Hare Krishnas ni akina nani na wanaamini nini?

Jibu


Mwanzo wa Hare Krishna, pia inayoitwa Gaudiya Vaishnavism au Chaitanya Vaishnavism, inakuzwa kupitia Shirika la Kimataifa kwa Utambuzi wa Krishna (au ISKCON). Hare Krishna ni madhehebu ya siri ya Uhindu. Kwa kawaida huainishwa kama aina ya kuabudu Mungu mmoja ya Uhindu, kwa kuwa Hare Krishnas anaamini kwamba miungu yote ni tu maonyesho mbalimbali ya mungu mmoja, Vishnu au Krishna. "Imani ya kuwa kuna Mungu mmoja" ya Hare Krishna inatatanisha kidogo, hata hivyo, kama Sri Krishna ana "mume wa milele" aitwaye Srimati Radharani; pamoja, Krishna na Radharani hujumuisha "Wanandoa wa Mungu."

Harakati ya Hare Krishna ilianza karne ya kumi na tano (1486), wakati mwanzilishi wake, Chaitanya Mahaprabhu, alianza kufundisha kwamba Krishna alikuwa Bwana mkuu juu ya kila mungu mwingine. Mahaprabhu alitetea njia ya ibada ya imani ambayo wafuasi wa Gaudiya Vaishnavism waliingia katika uhusiano na Krishna na walionyesha kuabudu kwao kwa Krishna kwa kucheza na kuimba. Maonyesho ya umma ya Mahaprabhu ya kuabudu yalipata ufuasi mkubwa, kwa sehemu fulani, kwa sababu ya tofauti zao kali na maneno yasiopendelea na ya kujinyima raha na anasa kawaida ya Uhindu. Madhehebu haya ya Kihindu, hata hivyo inaitofautisha katika uaminifu wake kwa Krishna, bado ni Kihindu kabisa, kwani hata Krishna ni lakini udhihirisho (au "Avatar") wa Vishnu-moja ya miungu ya kale ya Uhindu. Aidha, Hare Krishnas anahifadhi Bhagavad Gita, Maandiko ya Kihindu, pamoja na mafundisho ya roho kuzaliwa upya katika mwili wa mtu mwingine na karma.

Lengo kuu kwa Hare Krishnas ni njozi, uhusiano wa upendo na Bwana Krishna. Hare inamaanisha "furaha yenye nguvu ya Krishna." Kutokana na ibada yao ya siri inayoonyeshwa katika kuimba na kucheza, Hare Krishnas inaweza kulinganishwa na Waislamu wa Sufi ("Harakati la Darweshi") na baadhi ya maneno ya Kikristo ya fumbo ambayo yanasisitiza uzoefu wa furaha/huzuni na miujiza ya siri .

Hare Krishna inahitaji sana wafuasi wake. Kuwa mwanachama kunahusisha kuchagua guru na kuwa mwanafunzi wake. Guru huyu ni muhimu kwa kupata kuelimika; inasemekana kwamba bila guru ni vigumu kuendeleza ufahamu wa Krishna. Wafuasi wanajiwasilisha kwa guru wao kama mwalimu wa kiroho na hata kuwaabudu kama miungu. Na maisha yote ya mtu inapaswa kuzingirwa na mazoea ya msingi wa Kishna na moyo wa ibada. ISKCON huwavuta wanachama wake katika mipangilio ya jumuia ambako kila kitu kinazingatia kwa makusudi Krishna. Mengi ya utamaduni wa Hindi/Kihindu huingizwa katika jumuia hizi. Ni lazima ieleweke kwamba jumuia hizi zimeshutumiwa vikali na wanachama wa zamani, na ISKCON imepata mashtaka ya jinai yanashutumiwa na mazoea haramu na ya uasherati, ikiwa ni pamoja na unyanyasaji ulioenea wa watoto, unaofanyika ndani ya harakati.

Imani ya Hare Krishnas ni Kihindu hasa na haipatani na Ukristo wa kibiblia. Kwanza, mtazamo wa Mungu kimsingi ni kuabudu miungu, kumaanisha kwamba wanaamini Mungu ni wote na katika wote. Kwa Hare Krishnas, Mungu ni kila kitu na kila kitu ni Mungu. Kwa Mkristo, Mungu ni wa miujiza — Yeye ni juu ya vyote alivyoumba. Moja ya mafundisho ya ISKCON mawazo ni kwamba sisi hakika tunafikia umoja wa uhusiano na Mungu wenyewe. Lengo la Hare Krishna ni kufikia "utambuzi wa Krishna," aina ya kuelimisha. Hii ni kitambulisho cha kina zaidi na Krishna. Kwa kiasi kwamba vile ISKCON ni Hindu kweli, inaweza kudhani kwa mtazamo wa Mungu wa kuabudu miungu na kwa hivyo kufundisha kwamba mtu hatimaye ni sawa na Mungu. Huu ni uongo wa zamani ulioanza Bustani ya Edeni: "Utakuwa kama Mungu" (Mwanzo 3:5).

Kama dini zote za uongo, Hare Krishna inahitaji mfululizo wa kazi kwa wokovu. Ndiyo, ibada na uhusiano zimejaa katika mfumo wao wa imani, lakini hizi zimejengwa kutoka kwa kazi, kutoka kwa bhakti-yoga hadi tafakuri mbele ya madhabahu kwa kuomba fedha. Kuimba ni sehemu kuu ya Hare Krishna. Sri Chaitanya alipendekeza kwamba wafuasi wake wanaimba majina takatifu 100,000 kila siku. Kuimba kunawezeshwa na matumizi ya mala, tasbihi ya shanga 108. Kula nyama haikubaliki, kama ni kula katika mikahawa, kwa sababu ya imani kwamba chakula kinaweka ufahamu wa mpishi -- kumeza chakula kilichoandaliwa na mpishi mwenye hasira kitamfanya mwenye kula awe na hasira. Katika Hare Krishna, daima kuna kushinikiza kuimba zaidi, kucheza zaidi, na kufanya kazi kwa bidii ili baadhi ya sehemu ya madeni ya karmic huhifadhiwa na kusababisha mtu kushindwa kuingia ufahamu Krishna.

Kujikana na dhabihu pia ni muhimu kwa ajili ya wokovu katika Hare Krishna. Wokovu, kulingana na ISKCON, imesokotwa kabisa na dhana ya Hindu ya karma, au haki ya kuadhibu. Mafundisho haya yanahitaji imani katika kuzaliwa kiroho upya katika mwili wa mtu mwingine na/au uhamiaji wa nafsi. Kazi ya mtu, nzuri na mbaya, hupimwa na kuhukumiwa baada ya kifo. Ikiwa matendo ya mtu ni mema, anaendelea kuzaliwa upya kiroho katika fomu za maisha ya juu; ikiwa matendo yake ni mabaya, atakuwa fomu ya maisha ya chini. Ni tu wakati matendo mema ya mtu yameshinda mabaya kwamba anaweza kuacha mzunguko wa kuzaliwa upya na kutambua umoja wake na Krishna.

Ni jinsi gani Krishna ni tofauti kutoka kwa Mungu wa Biblia mwenye rehema na mwenye huruma ambaye "aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele" (Yohana 3:16). Biblia ni wazi kwamba wokovu ni kwa neema kupitia imani katika damu iliyomwagika ya Yesu Kristo (Waefeso 2:8-9). "Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye" (2 Wakorintho 5:21). Hakuna kiasi cha matendo mema yanaweza kufikia wokovu kwa mtu yeyote. Hare Krishnas, kama ubinadamu wote, wana tumaini moja tu kwa uzima wa milele: Yesu Kristo, alisulubiwa, alifufuliwa, na ameinuliwa milele. Njia zingine zote huongoza kwa uharibifu. Yesu mwenyewe alisema, "Mimi ndimi Njia, na Kweli, na Uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi "(Yohana 14:6). "Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo" (Matendo 4:12).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, Hare Krishnas ni akina nani na wanaamini nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries