settings icon
share icon
Swali

Je! Harakati ya Neno la Imani ni la Kibiblia?

Jibu


Mafundisho ya Neno la Imani bila shaka sio ya kibiblia. Sio dhehebu na haina shirika au uongozi rasmi. Badala yake, ni harakati ambayo imeshawishiwa sana na wachungaji na wallimu wengi wenye hadhi ya juu kama vile Kenneth Hagin, Benny Hinn, Kenneth Copeland, Paul na Jan Crouch, na Fred Price.

Harakati ya Neno la Imani ilikua kutoka kwa harakati ya Pentekoste mwishoni mwa karne ya 20. Mwanzilishi wake alikuwa E. W. Kenyon, ambaye alisoma udhanifu wa Mawazo Mapya ya Phineas Quimby. Sayansi ya akili (ambapo ilitokea kwa "iitaje na kuidai") iliunganishwa na Upentekoste, na kusababisha mchanganyiko wa kipekee wa Imani ya Kikristo na mafundisho ya kumfikia Mungu kwa tafkira. Kenneth Hagin, kwa upande wake, alisoma chini ya E. W. Kenyon na kufanya harakati ya Neno la Imani ilivyo leo. Ijapokuwa mafundisho ya kibinafsi yanayotofautiana kutoka uasi kabisa hadi kudharauliwa kabisa, kile kinachofuata ni teolojia ya msingi walimu wengi wa Neno la Imani wanafungamana wenyewe nalo.

Katika moyo wa harakati ya Neno la Imani ni imani katika "nguvu ya imani." Inaaminika maneno yanaweza kutumiwa kuendesha nguvu ya imani, na hivyo kwa kweli kuunda kile msemaji anaamini Maandiko yanaahidi (afya na utajiri). Sheria za kudhaniwa kutawala nguvu ya imani zinasemekana kufanya kazi kwa kujitegemea mapenzi huru ya Mungu na kwamba Mungu Mwenyewe anatii sheria hizi. Hii sio kitu ila aina ya ibada ya sanamu, kugeuza imani yetu-na kwa kujieneza wenyewe-kwa mungu.

Kutoka hapa, teolojia yake inapotea zaidi na zaidi kutoka kwa Maandiko: inadai kuwa Mungu aliumba wanadamu katika picha yake halisi, ya kimwili kama miungu wadogo. Kabla ya kuanguka, wanadamu walikuwa na uwezo kuita vitu kuwepo kwa kutumia nguvu ya imani. Baada ya kuanguka, wanadamu walichukua asili ya Shetani na kupoteza uwezo wa kuwaita vitu kuwepo. Ili kurekebisha hali hii, Yesu Kristo alitoa uungu Wake na akawa mwanadamu, akafa kiroho, akachukua asili ya Shetani juu Yake, akaenda kuzimu, alizaliwa tena, na kufufuka kutoka kwa wafu kwa asili ya Mungu. Baada ya haya, Yesu alimtuma Roho Mtakatifu badala ya mwili katika Waumini ili waweze kuwa miungu wadogo kama vile Mungu alitarajia awali.

Kufuatia maendeleo ya asili ya mafundisho haya, kama miungu midogo sisi tena tuna uwezo wa kuendesha nguvu ya imani na tuwe na usitawi katika maeneo yote ya maisha. Ugonjwa, dhambi, na kushindwa ni matokeo ya ukosefu wa imani, na hutibiwa kwa kuungama — kudai ahadi za Mungu kwa mtu binafsi kuwepo. Weka tu, harakati ya Neno la Imani inamtukuza mtu kwa hali ya mungu na kupunguza Mungu kwa hali ya mwanadamu. Ni wazi kwamba, hii ni uwakilishi wa uwongo wa Ukristo ni kuhusu nini. Kwa kawaida, mafundisho ya Neno la Imani haizingatii kile kinachopatikana katika Maandiko. Ufunuo wa kibinafsi, sio Maandiko, unategemea sana ili kuja na imani hizo za kipumbavu, ambazo ni ushahidi mmoja tu wa asili yake ya uasi.

Kupinga mafundisho ya Neno la Imani ni jambo rahisi la kusoma Biblia. Mungu peke yake ndiye Muumba Mwenye Enzi Kuu wa Ulimwengu (Mwanzo 1:3, 1 Timotheo 6:15) na hahitaji imani — Yeye ni chombo cha imani (Marko 11:22; Waebrania 11:3). Mungu ni roho na hana mwili wa kimwili (Yohana 4:24). Mwanadamu aliumbwa katika mfano wa Mungu (Mwanzo 1:26, 27; 9:6), lakini hii haimfanyi mungu mdogo au Mungu. Mungu peke yake ana asili ya kimungu (Wagalatia 4:8; Isaya 1:6-11, 43:10, 44:6; Ezekieli 28:2; Zaburi 8:6-8). Kristo ni wa Milele, Mwana wa Pekee aliyezaliwa, na mwili tu wa Mungu (Yohana 1:1, 2, 14, 15, 18; 3:16; 1 Yohana 4:1). Ndani yake unaishi ukamilifu wa Uungu wa mwili (Wakolosai 2:9). Kwa kuwa mwanadamu, Yesu alitoa utukufu wa mbinguni lakini sio Uungu Wake (Wafilipi 2:6-7), ingawa aliamua kuficha nguvu zake wakati alitembea duniani kama mtu.

Harakati ya Neno la Imani ni kuwadanganya watu wasiohesabika, na kuwasababisha kuelewa baada ya njia ya maisha na imani ambayo sio ya kibiblia. Katika kiini chake ni uongo sawa Shetani amekuwa akisema kutoka bustani: "Utakuwa kama Mungu" (Mwanzo 3:5). Kwa kusikitisha, wale wanaokubali mafundisho ya Neno la Imani bado wanamsikiliza Shetani. Matumaini yetu ni kwa Bwana, si kwa maneno yetu wenyewe, sio hata kwa imani yetu wenyewe (Zaburi 33:20-22). Imani yetu inatoka kwa Mungu kwanza (Waefeso 2:8; Waebrania 12:2) na sio kitu tunachojenga kwa sisi wenyewe. Hivyo, jihadharini na harakati ya Neno la Imani na kanisa lolote linalojiweka na mafundisho ya Neno la Imani.

English


Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Harakati ya Neno la Imani ni la Kibiblia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries