settings icon
share icon
Swali

Hali ya kati ni nini?

Jibu


"Hali ya kati" ni dhana ya kitheolojia inayoelezea kuhusu aina gani ya mwili, ikiwa ipo, waumini mbinguni wanapokuwa nayo wakati wanasubiri miili yao kufufuliwa. Biblia inaonyesha kuwa waumini wafu wamekuwa na Bwana (2 Wakorintho 5: 6-8; Wafilipi 1:23). Biblia pia inaonyesha wazi kwamba ufufuo wa waumini haujafanyika bado, maana yake ni kwamba miili ya waumini waliokufa bado imo kaburini (1 Wakorintho 15: 50-54; 1 Wathesalonike 4: 13-17). Kwa hiyo, swali la hali ya kati ni kama waumini mbinguni hupewa miili ya muda mfupi hadi watakapofufuliwa, au kama waumini mbinguni wako katika fomu ya kiroho / isiyo ya mwili mpaka watakapofufuliwa.

Biblia haitoi maelezo mengi kuhusu hali ya kati. Andiko pekee ambalo hasa, lakini sio kwa moja kwa moja, linazungumzia suala hili ni Ufunuo 6: 9, "... Niliona chini ya madhabahu nafsi za wale waliouawa kwa sababu ya neno la Mungu na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao." Katika huu mstari Yohana amepewa maono ya wale watakaouawa kwa sababu ya imani yao wakati wa mwisho. Katika maono haya waumini waliokuwa wameuawa wamo chini ya madhabahu ya Mungu mbinguni na wanaelezewa kama "roho." Kwa hiyo, kutokana na aya hii moja, ikiwa kuna jibu la kibiblia ya hali ya kati, inaonekana kwamba waumini mbinguni wako katika fomu ya kiroho / isiyo ya mwili hadi ufufuo.

Mbingu ambayo hatimaye inasubiri waumini ni Mbingu mpya na Dunia Mpya (Ufunuo 21-22). Mbingu itakuwa kweli mahali pa kijiografia. Miili yetu itafufuliwa na kutukuzwa, iliyofanyika kamilifu kwa milele katika Dunia Mpya. Kwa sasa, mbingu ni eneo la kiroho. Inaonekana, basi, kwamba hakutakuwa na haja ya miili ya muda mfupi ikiwa waumini wako katika mbingu ya kiroho. Hali ya kati inawezakuwa chochote kile,lakini tunaweza kuhakikisha kuwa waumini mbinguni wameridhika, na kufurahia utukufu wa mbingu na kuabudu utukufu wa Bwana.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Hali ya kati ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries