settings icon
share icon
Swali

Kuhesabiwa haki ni nini?

Jibu


Kuiweka rahisi, kuhalalisha ni kutangaza uadilifu, na hivyo kumfanya mtu haki na Mungu. Haki ni Mungu hutangaza wale ambao wamempokea Kristo kuwa waadilifu , kwa kuzingatia haki ya Kristo kuwa tafsiriwa kwenye akaunti ya wale ambao humpokea Kristo (2 Wakorintho 5:21). Ingawa haki kama kanuni hupatikana katika maandiko, kifungu kuu kinachoelezea haki kwa mahusiano na waumini ni Warumi 3:21-26 : "Lakini sasa, haki ya Mungu imedhihirika pasipo sheria; inashuhudiwa na torati na manabii, na haki ya Mungu iliyo kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote waaminio. Maana hakuna tofauti, kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu, wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu; ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa njia ya haki yake, kwa sababu ya kuziachilia katika ustahimili wa Mungu dhambi zote zilizotangulia kufanywa; apate kuonyesha haki yake wakati huu, ili awe mwenye haki na mwenye kumhesabu haki yeye amwaminiye Yesu."

Sisi tumefanywa waadilifu, na kutangazwa waadilifu, wakati wa wokovu wetu. Haki haitufanyi sisi kuwa wenye haki, lakini badala yake hutangaza sisi kuwa wenye haki. Haki yetu inatokana na kuweka imani yetu katika kazi ya Yesu Kristo. Sadaka yake inafunika dhambi zetu, kumruhusu Mungu kutuona sisi kama watu kamili na wwasio na kasoro. Kwa sababu kama waumini tuko ndani ya Kristo, Mungu anaona haki ya Kristo pekee wakati yeye anatuangalia. Hii hutimiza mahitaji ya Mungu kwa ukamilifu, hivyo, anatutangaza kuwa wenye haki -Yeye anatufanya kuwa haki.

Warumi 5:18-19 yatoa mhutasari vizuri: "Basi tena, kwam kwa kosa moja watu wote walihukumiwa adhabu, kadhalika kwa tendo moja la haki watu wote walihesabiwa hakie yenye uzima. Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya weney dhambi, kadhalika kwa kutii kwake mmoja watu wengi wameingizwa katika hali ya wenye haki." Ni kwa sababu ya haki kwamba amani ya Mungu inaweza kutawala katika maisha yetu. Ni kwa sababu ya haki kwamba waumini wanaweza kuwa na uhakika wa wokovu. Ni ukweli wa haki ambao unamwezesha Mungu kwa kuanza mchakato wa utakaso - utaratibu ambao Mungu hutufanya sisi katika hali halisi ambayo tumekwisha hesabika kwayo. "Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo" (Warumi 5:1).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kuhesabiwa haki ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries