settings icon
share icon
Swali

Je! Ni kwa nini haki ya Kristo inafaa kuingizwa ndani yetu?

Jibu


Katika Mahubiri yake Mlimani, Yesu alitamka maneno haya: "Kwa hiyo kuweni wakamilifu kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu" (Mathayo 5:48). Hii inakuja mwishoni mwa sehemu ya mahuribi ambapo Yesu anawarekebisha wasikilizaji kwa kuielewa vibaya Sheria. Katika Mathayo 5:20, Yesu anasema kwamba, ikiwa wasikilizaji wake wanataka kuingia ufalme wa mbinguni, haki yao lazima izidi ile ya Mafarisayo, ambao walikuwa wataalam wa Sheria.

Tena, katika Mathayo 5:21-48, anaendelea kwa kuifafanua sheria kinaga naga kutoka katika kuifuata tu kwa nje, ambayo ilitambua "haki" ya Mafarisayo, hadi kuitii nje na ndani. Anasema, "Mmesikia kwamba ilinenwa, lakini mimi nawaambia kwamba" kutofautisha kati ya namna ambayo watu waliisikia sheria ikifunzwa na vile Yesu aliifafanua. Kuitii sheria ni zaidi ya kujuzuia kutoka kuua, kufanya usinzi, na kuvunja nadhiri. Pia sio kuhisi hamaki na ndugu yako, si kuwa na tamaa ndani ya moyo wako, na sio kuweka nadhiri isiyo ya kweli. Mwisho wa haya yote, tunajifunza kwamba lazima tupite haki ya Mafarisayo, na hiyo hutokana na kuwa wakamilifu.

Katika hatua hii itikio la kiasili ni "Lakini siwezi kuwa mkamilifu," ambayo ni kweli kabisa. Mahali kwingine katika Injili ya Mathoyo, Yesu anafupisha Sheria ya Mungu kwa amri mbili: Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote na kwa akili zako zote na mpende jirani yako kama nafsi yako (Mathayo 22:37-40). Kwa hakiki hili lengo la kupendeza, lakini je! kunaye mtu ambaye amewahi mpenda Bwana kwa moyo wake wote, roho yake yote, na akili yake yote, na nguvu zake zote na jirani yake kama anavyoipenda nafsi yake? Kila kitu tunachofanya, kusema, na kuwaza lazima vifanywe, visemwe, na kufundishwa kutoka kwa upendo wetu kwa Mung una kwa majirani zetu. Ikiwa sisi ni waaminifu kwa nafsi zetu, lazima tukubali kuwa hatujawai fikia kiwango hiki kiroho.

Ukweli wa mambo ni kuwa, peke yetu na kwa juhudi zetu wenyewe, hatuwezi kuwa wakamilifu kama Baba yetu wa mbinguni alivyo mkamilifu. Hatumpendi Mungu kwa moyo wetu wote, roho, akili na nguvu zetu zote. Hatuwapendi majirani zetu jinzi tunavyojipenda. Tuko na shida nayo shida hiyo ni dhambi. Tunazaliwa nayo, na hatuwezi kushinda madhara yake sisi wenyewe. Dhambi hutuadhiri sana hadi kwa msingi. Dhambi huadhiri kile tunafanya, kusema na kufikiria. Kwa maneno mengine, kinatia doa kila kitu kinachotuhusu. Kwa hivyo, haijalishi ni namna gani tunajaribu kuwa, hatutawai fikia kiwango cha Mungu cha ukamilifu. Biblia inasema kwamba maentendo yetu yote mema ya haki ni kama "vazi lililochafuliwa" (Isaya 64:6). Haki yetu wenyewe sio njema ya kutosha na kamwe haitakuwa, haijalishi jinsi tutakavyo tia bidi.

Hiyo ndiyo sababu Yesu aliishi maisha makamilifu katika utiifu kamili wa sheria ya Mungu katika mawzo, maneno na matendo. Ujumbe wa Yesu haukuwa wa kukufa msalabani tu kwa ajili ya dhambi zetu bali sisi tuishi maisha ya haki kamili. Wanatheolojia hurejelea hili kama "utiivu wa Kristo wa vitendo na usio wa vitendo." Utiivu wa vitendo hurejelea maisha ya Kristo yasiyo ya dhambi. Kila alifanya kilikuwa kikamilifu. Utiivu usioonekana ni ule wa Kristo kunyenykea hadi kufa msalabani. Alienda kwa hiari msalabani na akakubali kusulubiwa bila pingamizi (Isaya 53:7). Utiivu wake usioonekana ulilipa dani yetu ya dhambi mbele za Mungu, lakini ni utiivu unaonekana ambao unatupa ukamilifu ule Mungu anahitaji.

Mtume Paulo anaandika, "Lakini sasa, haki itokayo kwa Mungu imedhihirishwa pasipo sheria, ambayo Sheria na Manabii wanaishuhudia. 22Haki hii itokayo kwa Mungu hupatikana kwa Yesu Kristo kwa wote wamwaminio" (Warumi 3:21-22). Kupitia Imani yetu katika Kristo, tumepewa haki ya Mungu. Hii ndio inaitwa haki ya "kupwe." Kuingiz kitu ni kuhuzisha au kufikiria kitu kwa mtu. Wakati tunaiweka imani yetu kwa Kristo, Mungu hupachika haki kamilifu ya Kristo kwetu ili sisi tuweze kuwa wakamilifu mbele Zake. "Kwa maana Mungu alimfanya yeye asiyekuwa na dhambi kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kufanywa haki ya Mungu kwake yeye" (2 Wakorintho 5:21).

Sio haki ya Kristo hupachikwa kwetu tu kwa imani, bali dhambi zetu hupachikwa kwa Kristo. Hivyo ndivyo Kristo alilipa deni ya dhambi zetu kwa Mungu. Hakuwa na dhambi ndani Yake, lakini dhambi yetu ilipachikwa kwake, ili alipoteseka msalabani, aliteseka hukumu ya haki ambayo dhambi zetu zilistahili. Hiyo ndiyo sababu Paulo anasema, "Nimesulubiwa pamoja na Kristo, wala si mimi tena ninayeishi, bali Kristo ndiye aishiye ndani yangu. Uhai nilio nao sasa katika mwili, ninaishi kwa imani ya Mwana wa Mungu, aliyenipenda na kujitoa kwa ajili yangu" (Wagalatia 2:20).

Kupata haki ya Kristo kupachikwa kwetu au kuhesabiwa, tuanweza kuonekana bila dhambi vile Yesu alivyo. Sisi peke yetu si wenye haki; badala yake, tunamiliki haki ya Kristo kuhesabiwa kwa niapa yetu. Sio ukimilifu wetu, bali ule wa Kristo ambao Mungu anauona wakati anatuleta katika ushirika Naye. Kimatendo sisi bado ni wenye dhambi, lakini neema ya Mungu imetutangaza kuwa na haki mbele ya sheria.

Katika mfano wa Yesu wa karamu ya harusi, wageni wemealikwa kwa karamu kutoka kwa kila pempe ya kinjia, na wameletwa ndani, "wabaya vile vile na wema" (Mathayo 22:10). Wageni wote wana kitu kimoja sawia: wote wemepewa vazi la harusi. Hawastahili kuvaa mafazi yao tambara kwenye chumba cha karamu bali wanafaa kuvaa mavazi ambayo mfalme alipeana. Hii ni taswira nzuri sana ya upachikaji. Kama wageni katika nyumba ya bwana, tumepewa vazi jeupe nzuri sana la haki ya Kristo. Tunapokea zawadi hii neema ya Mungu kwa imani.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Ni kwa nini haki ya Kristo inafaa kuingizwa ndani yetu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries