settings icon
share icon
Swali

Ninawezaje kujifunza kutofautisha kati ya haki na mbaya?

Jibu


Kila mwanadamu ameumbwa kwa mfano wa Mungu (Mwanzo 1:27; Yakobo 3: 9). Maana ya kuumbwa wa mfano wa Mungu ni kwamba tuna dhamiri ambayo inatambua mema na mabaya na inatofautisha mema na mabaya. Kila utamaduni wenye ustaarabu duniani umekubali viwango sawa kwa watu wake kulingana na ufahamu huu wa asili wa mema na mabaya. Kuua, wizi, na udanganyifu yote haya yaeleweka kuwa ni mabaya. Wakati mwingine uharibifu huwa zaidi ya hekima hio, na kundi la watu huchagua kufuata uovu badala ya kuasi, kama ilivyo katika kesi ya mauaji ya watoto yaliyofanywa na mataifa ya jirani ya Israeli (Mambo ya Walawi 18:21; 2 Wafalme 23:10).

Kutokana na asili yetu ya dhambi, tunaruhuru uovu ndani yetu (Warumi 5:12; Yeremia 2:35). Tunapoendelea kuruhusu uovu basi tunasababisha ugumu wa dhamiri. Warumi 1:28 huwapa majibu ya Mungu kwa wale wanaoendelea katika uovu: " Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa." Kuna jambo ambalo Mungu anaruhusu kufanyika. Wale ambao wanasisitiza kuzingatia dhambi zao sasa wanaweza kutenda kwa ujasiri na hawatapata dhiki ya dhamiri. Wao wanaamini kuwa wameisinda dhamiri na kuwa ni werevu kuliko Mungu. Lakini hukumu yao itakuja wakati watakaposimama mbele ya Kristo (Waebrania 9:27; Malaki 3: 5

Kama giza inavyoelezewa kama ukosefu wa mwanga, dhambi inaelezewa kama ukosefu wa wema (Yakobo 4:17). Kwa kuwa Mungu ni mfano mzuri wa wema (Zaburi 86: 5, 119: 68), kitu chochote kinyume na asili yake ni mabaya (Warumi 3:23). Tunajifunza kutofautisha mema na maovu kwa kumjua Mungu. Neno lake ni msingi wa kumwelewa Yeye (Zaburi 1: 1-2, 119: 160; Yohana 17:17). Tunakaribia utakatifu wa Mungu, dhambi huonekana mbaya zaidi(Isaya 6: 1, 5). Shati inaweza kuonekana nyeupe dhidi ya ukuta mweusi. Lakini unapoweka shati juu ya theluji iliyoanguka, inaonekana inafaa sana kushinda shati. Vivyo hivyo, majaribio yetu ya wema yanaonekana yanayojitokeza sana wakati wa kuwekwa karibu na utakatifu wa Mungu. Tunapoenda mbele ya uwepo wake, tunaanza kutambua jinsi tunavyijishughulisha na mawazo na matendo yetu binafsi. Tunaona tamaa zetu wenyewe, tamaa ya vitu za wenyewe na udanganyifu kuwa ni maovu kabisa. Ni katika mwanga wa Mungu tu kwamba tunaanza kujiona wenyewe vizuri.

Pia tunajifunza kutofautisha kati ya mema na maovu kwa kujua Neno. Ni Biblia ambayo inafafanua kile ambacho ni dhambi na sio dhambi. Mwandishi wa Waebrania anaelezea juu ya wale ambao ni wachanga katika imani yao, ambao wanaweza tu kusyaga "maziwa" ya kiroho — kanuni la msingi ya Neno la Mungu (Waebrania 5:13). Tofauti na "watoto wachanga" ndani ya Kristo kuna wale waliokomaa wa kiroho, "... ambao kwa matumizi ya mara kwa mara wamejifunza kutofautisha mema na mabaya" (Waebrania 5:14). Kumbuka kwamba akili za kiroho za Kikristo zinaimarishwa kupitia "matumizi ya mara kwa mara" ya Neno. Uwezo wa kuelezea haki na uovu, kutofautisha kati ya mafundisho ya Kristo na ya mwanadamu, huja kwa kujifunza na kutumia Neno la Mungu.

Neno la Mungu limejaa mifano ya wale ambao walifanya haki na wale waliofanya makosa. Mifano hiyo iko ili tuweze kujifunza jinsi Mungu alivyo na kile anachotaka kutoka kwetu (1 Wakorintho 10:11). Mika 6: 8 inatoa muhtasari mfupi wa kile Mungu anatamani kutoka kwa kila mtu: " Ee mwanadamu, yeye amekuonyesha yaliyo mema; na Bwana anataka nini kwako, ila kutenda haki, na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako!

"Malaki 3:18 inaweka wazi zaidi. Mungu anasema, " Ndipo mtakaporudi, nanyi mtapambanua kati ya wenye haki na waovu, na kati ya yeye amtumikiaye Mungu na yeye asiyemtumikia.

Katika kufungu hiki, mema hufafanuliwa kama kumtumikia Mungu hivyo basi uovu ni kukataa Mungu na kukataa kumtumikia. Haijalishi jinsi mtu anavyoonekana kuwa wa msaada kwa wengine, kazi yake nzuri huwa kidogo ikiwa anaifanya kwa sababu za ubinafsi. Ikiwa tunaifanya kuwa lengo letu kumtafuta Mungu na kumheshimu katika kila kitu tunachofanya (1 Wakorintho 10:31), tutaelewa haki na mbaya na kujua kwamba chaguo letu maishani linampendeza (Yeremia 29:13, 1 Petro 3: 12; Zaburi 106: 3).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ninawezaje kujifunza kutofautisha kati ya haki na mbaya?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries