settings icon
share icon
Swali

Je! Haki ni nini?

Jibu


Kamusi inafafanua haki kama "mwenendo ambao hasa unaweza thibitishwa au uko adilifu." Tabia kama hiyo hutambulika kwa vile viwango vimekubalika vya maadili, haki, wema, na heshima. Kiwango cha Biblia cha haki ya mwanadamu ni ukamilifu wa Mungu pekee katika kila uadilifu, kila nia, kila tabia na kila neno. Hivyo, sheria ya Mungu, vile imepeanwa katika Biblia, zote zinaelezea tabia yake na kuunda kiwima ambacho kwacho Anakadria haki ya mwanadamu.

Neno la Kigiriki la Agano Jipya kwa "haki" kimsingi linaelezea mwenendo kuhusiana na maneno mengine, hasa kuhusiana na haki za wengine katika biashara, katika maswala ya kisheria, na kuanza na uhusiano na mungu. Linatofautishwa na uovu, mwenendo wa mmoja ambaye kwa ajili ya ubinafsi mwingi, hamheshimu Mungu wala mwanadamu. Biblia inaelezea mtu mwadilifu kama yule aliye wa haki, au mnyoofu, anayemshikilia Mung una kumtumainia Yeye (Zaburi 33:18-22).

Habari mbaya ni kuwa haki ya kweli na kamilifu ni vigumu kwa mwanadamu kuifikia kwa juhudi zake mwenyewe; kiwango huwa cha juu sana. Habari njema ni kwamba kuna uwezekano mwanadamu kuwa na haki ya kweli, lakini kwa kupitia utakazo wa dhambi unaofanywa na Yesu Kristo na ujazo wa Roho Mtakatifu. Hatuna uwezo wa kufikia haki sisi wenyewe. Lakini Wakristo wanamiliki haki ya Kristo, kwa sababu "Mungu alimfanya ahusike na dhambi kwa ajili yetu, ili sisi kwa kuungana naye, tupate kuushiriki uadilifu wake Mungu" (2 Wakorintho 5:21). Huu ni ukweli wa ajabu. Msalabani, Yesu alibadilishana na dhambi na haki Yake kamilifu ili siku moja tuweze kusimama mbele za Mungu na asione dhambi zetu, lakini haki takatifu ya Bwana Yesu.

Hii inamaanisha kwamba tumefanywa watakatifu mbele za Mungu; hiyo ni kusema kwamba, tumekubalika kuwa wenye haki na kuhesabiwa wenye haki na Mungu juu ya kile Bwana Yesu amefanya. Alifanywa kuwa na dhambi; sisi tukafanywa wenye haki. Msalabani, Yesu alichukuliwa kana kwamba alikuwa mwenye dhambi, ingawa alikuwa mtakatifu kikamilifu na mwadilifu, na sisi tumechukuliwa kuwa wenye haki, ingiwa tumeharibiwa na kupotoshwa. Kwa sababu ya kile ambacho Bwana Yesu alivumilia kwa niapa yetu, tumechukuliwa kana kwamba tuliitimiza Sheria yote ya Mungu na hatujawai karibia hukumu yake. Tumepokea karama hii maalum ya haki kutoka kwa Mungu mwenye huruma yote na neema. Utukufu kwake.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Haki ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries