settings icon
share icon
Swali

Je! kuna mbinu gani mbaya/njema ya kushiriki injili? Je! Ni sehemu gani injili inakua habari mbaya?

Jibu


Mambo mengi katika Maisha yana habari njema na habari mbaya kuhusishwa nayo. Ukweli wote hasa unapatikana katika muunganiko wa mambo yote mawili. Kusisitiza upande mmoja na kutenga mwingine sio ukweli wote. Hivyo ilivyo kwa injili ya Yesu Kristo.

Tukiongea kiroho, habari mbaya ni, sisi wote ni wenye dhambi na tunastahili jahannamu kwa sababu ya dhambi zetu dhidi ya Mungu mtakatifu (Warumi 3:23; 6:23). Dhambi zetu zimetutenga na uwepo wake na uzima wa milele (Yohana 3:15-20). Hakuna anayeweza kupata njia inayoenda mbele za Mungu kwa sababu hakuna aliye "mwenye haki" (Warumi 3:10). Juhudi zetu bora za kumpendeza Mungu ni kama "matambaa machafu" (Isaya 64:6). Baadhi ya wainjilisti na wahubiri wa vinjia wanaangazia san asana sehemu hii ya ukweli wa Mungu, ambayo inaweza kuchukuliwa kuwa "mtindo wa habari mbaya."

Habari njema ni kuwa Mungu anatupenda (Yohana 3:15-18). Anataka uhusiano na wanadamu aliowaumba na amezungumza nazi kwa njia mbali mbali kama vile masingira (Warumi 1:20), Biblia (2 Timotheo 3:16), na Yesu kuja katika umbo la mwanadamu na kuishi pamoja nasi (Yohana 1:14). Mungu anatupenda. Mungu anataka kutubariki. Anataka uhusiano nasi na anatamani kutufunza njia zake ili tuwe kile alituumbia tuwe (Warumi 8:29). Walimu ambao wanaoangazia habari njema pekee wanaacha nje sehemu muhimu sana ya mpango wa wokovu wa Mungu, ambao unahusisha toba (Mathayo 3:2; Marko 6:12) na kuchukua msalaba wetu na kumfuata Yesu (Luka 9:23).

Hadi tujue habari mbaya, hatuwezi kuthamini habari njema. Huwezi kuthamini mgeni anayeingia nyumbani kwako na kukuvuta nje, isipokuwa una ufahamu kuwa nyumba yako inachomeka. Hadi tufahamu kuwa tunaelekea kuzimuni kwa sababu ya dhambi zetu, hatuwezi kuthamini yale yote ambayo Yesu alitufanyia msalabani (2 Wakorintho 5:21). Ikiwa hatuwezi kugundua jinsi hatuna tumaini, hatuwezi kutambua tumaini kuu ambalo Yesu anatoa (Waebrania 6:19). Isipokuwa tutambue kuwa sisi ni wenye dhambi, hatuwezi kumthamini Mwokozi.

Njia bora ni kuwakilisha kile mtume Paulo alikiita "mapenzi yote ya Mungu" (Matendo 20:27). Mapenzi yote ya Mungu hujumuisha habari mbaya na habari njema kuhusu mpango wa Mungu wa kutukomboa. Yesu hakuoondoa lolote kati ya hili wakati Alileta "iwe amani kwa watu aliowaridhia" (Luka 2:14). Amani yake inapatika kwa kila mtu ambaye ameletwa katika toba na "habari mbaya" na kwa furaha kukubali "habari njema" ya kwamba Yeye ni Bwana wa wote (Warumi 10:8-9).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! kuna mbinu gani mbaya/njema ya kushiriki injili? Je! Ni sehemu gani injili inakua habari mbaya?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries