settings icon
share icon
Swali

Gogu na Magogu ni nani?

Jibu


Kihistoria, Magogu alikuwa mjukuu wa Nuhu (Mwanzo 10: 2). Wazao wa Magogu walikaa kaskazini mwa Israeli, labda huko Ulaya na kaskazini mwa Asia (Ezekieli 38:15). Hatimaye Magogu akawa jina la nchi ambapo wazao wa Magogu walikaa. Watu wa Magogu wanaelezewa kuwa wapiganaji wenye ujuzi (Ezekieli 38:15; 39: 3¬-9). Gogu ni jina la kiongozi wa baadaye katika Magogu ambaye ataongoza jeshi kushambulia Israeli. Bwana anatabiri adhabu ya Gogu: "Mwanadamu, kaza uso wako, umwelekee Gogu, wa nchi ya Magogu… ukatabiri juu yake" (Ezekieli 38: 2).

Gogu na Magogu wanatajwa katika Ezekieli 38-39 na katika Ufunuo 20: 7-8. Ingawa vifungu hivi viwili vinataja majina sawa, kujifunza kwa karibu kwa Maandiko huonyesha kwamba hazirejelei watu sawia na matukio. Katika unabii wa Ezekieli, Gogu atakuwa kiongozi wa jeshi kubwa ambalo linashambulia nchi ya Israeli. Gogu anaelezwa kuwa "wa nchi ya Magogu, mkuu wa Mesheki na Tubali" (Ezekieli 38: 2). Vita vya Ezekieli ya Gogu na Magogu hutokea katika kipindi cha dhiki, labda katika miaka mitatu na nusu ya kwanza. Uthibitisho mkubwa zaidi wa maoni haya ni kwamba mashambulizi yatakuja wakati Israeli ipo na amani (Ezekieli 38: 8, 11) — taifa limeweka ulinzi wake. Israeli dhahiri haina amani sasa, na haiwezekani kwamba taifa litaweka ulinzi wake ili kujikinga na matukio kubwa. Wakati agano la Israeli na Mpinga Kristo linatumika mwanzoni mwa wiki ya 70 ya Danieli (dhiki ya miaka saba-Danieli 9: 27a), Israeli watakuwa na amani. Labda vita vitafanyika tu kabla ya kipindi cha miaka saba. Kulingana na Ezekieli, Mungu Mwenyewe atamshinda Gogu juu ya milima ya Israeli. Kuchinjwa kutakuwa kubwa sana itachukua miezi saba kuzika wafu wote (Ezekieli 39: 11-12).

Gogu na Magogu wanatajwa tena katika Ufunuo 20: 7¬-8. Hii ni vita tofauti, lakini kurudia kwa majina Gogu na Magogu huonyesha kwamba historia itajirudia yenyewe. Uasi huo dhidi ya Mungu unaonekana katika Ezekieli 38-39 utaonekana tena.

Kitabu cha Ufunuo kinazia unabii wa Ezekieli wa Magogu kuwa unaelezea mwisho wa nyakati za kushambulia taifa la Israeli (Ufunuo 20: 8-9). Matokeo ya vita hii ni kwamba maadui wote wa Mungu wameharibiwa, na Shetani atapata nafasi yake ya mwisho katika ziwa la moto (Ufunuo 20:10).

Hapa chini ni baadhi ya sababu zilizo wazi zaidi za ni kwa nini Ezekieli 38-39 na Ufunuo 20: 7-8 hutaja watu tofauti na vita tofauti:

1. Katika vita vya Ezekieli 38-39, majeshi huja kutoka kaskazini na kuhusisha mataifa machache tu duniani (Ezekieli 38: 6, 15; 39: 2). Vita katika Ufunuo 20: 7-9 vitahusisha mataifa yote, kwa hiyo majeshi yatakuja kutoka pande zote, si tu kutoka kaskazini.

2. Hakuna kutajwa kwa Shetani katika muktadha wa Ezekieli 38-39. Katika Ufunuo 20: 7 muktadha unaonyesha wazi vita mwishoni mwa milenia na Shetani kama mshambuliaji wa msingi.

Ezekieli 39: 11-12 inasema kwamba wafu watazikwa kwa miezi saba. Hakutakuwa na haja ya kuzika wafu ikiwa vita katika Ezekieli 38-39 ni sawa na ilivyoelezwa katika Ufunuo 20: 8-9, kwa mara baada ya Ufunuo 20: 8-9 ni hukumu kubwa ya kiti cha enzi cheupe (20: 11- 15), na kisha mbinguni na mbingu ya sasa na dunia zinaharibiwa na kubadilishwa na mbingu mpya na dunia mpya (Ufunuo 21: 1). Kwa dhahiri kutakuwa na haja ya kuzika wafu ikiwa vita hufanyika katika sehemu ya kwanza ya dhiki, kwa kuwa nchi ya Israeli itachukua muda wa miaka 1,000, urefu wa ufalme wa milenia (Ufunuo 20: 4-6).

4. Vita katika Ezekieli 38-39 hutumiwa na Mungu kumleta Israeli kwake (Ezekieli 39: 21-29). Katika Ufunuo 20, Israeli imekuwa mwaminifu kwa Mungu kwa miaka 1,000 (ufalme wa milenia). Waasi katika Ufunuo 20: 7-10 wameharibiwa bila nafasi yoyote ya kutubu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Gogu na Magogu ni nani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries