settings icon
share icon
Swali

Je! Mkristo anapaswa kwenda kwenye sinema/kanda? Je! Kutizama filamu ni dhambi?

Jibu


Kwa Mkristo sana sana swali sio “Je! Kutazama sinema hii ni dhambi?” bali ni “hili ni jambo ambalo Yesu angelinitaka nifanye?” Biblia inatuambia kwamba vitu vingi ni halali, lakini sio vitu vyote ni vya manufaa au vinavyojenga (1 Wakorintho 10:23). Pia inasama kwamba chochote tunachosema au kufanya (au kutazama) kinapaswa kufanywa kwa utukufu wa Mungu (1 Wakorintho 10:31). Tunapaswa kutafakari kuhusu mambo ya heshima na safi (Wafilipi 4:8). Na ikiwa tunaweza kutazama filamu au kipindi katika runinga ambacho kina maudhui ya kutiliwa shaka na BADO tukubaliane na amri hizi kutoka kwa Biblia, basi ni vigumu kuona kosa katika hili.

Hatari iko katika (1) jinsi mambo tunayotazama yanavyoathiri moyo wetu na (2) jinsi yanavyoathiri wengine. Kwetu sisi wenyewe, ikiwa tukio tunaloona linaleta hisia ya tamaa, hasira, au chuki, basi tumefanya dhambi (Mathayo 5:22, 28), na ni lazima tufanye lolote tuwezalo ili kuepuka hilo kutokea tena. Mara nyingi hiyo inamaanisha kutotazama aina hiyo ya filamu/onyesho tena. Pia, inaweza kuwa kikwazo kwa mtu ambaye anapambana na tabia fulani au tabia ambayo inakua kikwazo kati yake na Mungu (1 Wakorintho 10:25-33; Warumi 14:13). Kama viungo vya mwili wa Kristo, tunapaswa kuwa nuru kwa ulimwengu (Mathayo 5:14) na mfano mtakatifu wa kile ambacho Mungu amefanya katika maisha yetu (1 Petro 2:11-12). Iwapo tutaonekana na wengine tukiingia katika kwenye filamu iliyokadiriwa “R”, inaweza kutuma ujembe usio sahihi kwao-kwamba tunafurahia na/au kuunga mkono ngono haramu na vurugu. Hilo halifai kuwa nuru katika ulimwengu wa giza.

Kwa hivyo, tunajuaje kwa uhakika ikiwa tunachotazama kina manafuaa? Tunapofanyika wafuasi wa Kristo, tunapewa Roho wake Mtakatifu kuishi ndani yetu (Matendo 2:28; 2 Timotheo 1:14). Yesu anatuambia kwamba Roho huyu atatuongoza katika kweli yote (Yohana 16:13). Njia moja ambayo Roho wa Mungu hutuongoza ni kwa dhamiri zetu (Warumi 1:12; 9:1). Ikiwa dhamiri yako inakuambia kwamba kile unachotazama si sahihi, huenda hivyo ndivyo ilivyo.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Mkristo anapaswa kwenda kwenye sinema/kanda? Je! Kutizama filamu ni dhambi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries