settings icon
share icon
Swali

Fedha za kanisa zinafaa kuwa na uwazi gani?

Jibu


Wakati wowote fedha zinazungumziwa huwa ni suala la kugusa sana, hii pia ni kweli kwa fedha za kanisa,na mengi hueleweka. Ikiwa mtu amejitolea kuchangia kanisa ni vizuri kwa mtu kama uyo kujua jinsi fedha izo zinatumika. Katika kanisa zingine karibu kila maamuzi ya kifedha huamuliwa na umati kupitia maoni yao na kwenye kanisa zingine ni mhubiri tu ama viongozi wachache hujua jinsi fedha za kanisa hutumika. Ukweli wa Biblia unaelea apo katikati.

Biblia haijarekodi matumizi au vikao vyovyote vya kifedha za kanisa ya kale . Mtindo unaonekana kuwa, kanisa iliamini kiongozi ama viongozi na fedha zake na viongozi hao walisimamia matumizi ya fedha izo. Warumi 15:25-28 na 1Wakoritho 16:1-4 inaelezea jinsi kanisa ilikusanya fedha na kuzipea Paulo na makundi ya wengine ambao waligawa fedha izo. Je, kanisa ya kisasa inafaa kufuata huu mtindo aje? Kwa sababu hakuna maagizo ya kibiblia inaonekana Mungu anataka uhuru fulani kuhusu suala hili. Je, kanisa linaweza kuwa na baraza,liwe la wazee ,mashemasi ama waumini ambao wanaangazia maamuzi ya kifedha? Ndio. Je, umati wa kanisa unaeza toa maoni na kuhusishwa katika shughuli za kifedha? Ndio.Je, kanisa linaweza kumchagua mtu mmoja kama mweka hazina ama mhubiri mkuu awe akisimamia fedha zote? Ingawa mtindo huu unakosa uwajibikaji,Biblia haijakataa na kwa hivyo jibu ni ndio.

Kitu ya muhimu ni jinsi fedha zinatumika si mwenye anaamua matumizi yake. Fedha za kanisa hutumika kwa njia gani? Fedha za kanisa zikitumika kwa njia ya uaminifu,uadilifu,uwakili mzuri na kwa uwazi haina haja ya kujua mwenye anazieka. Kamati inaeza tumia fedha vibaya kama vile tu mtu binafsi anaeza tumia vibaya. Kanisa linafaa kuwa makini kwa kumchagua mtu am watu watakao linda fedha zake. Kitu muhimu kwa mtu atakaye chunga fedha za kanisa asiwe anapenda pesa na awe anashughulikia majukumu yake ya nyumbani vizuri( 1Timotheo 3:3-5)

Hata kama ni nani ama akina nani uwajibikaji ni muhimu sana. Jinsi kanisa linatumika fedha zake inafaa kuwa ya uwazi. Kanisa inafaa ikue tayari kuelezea jinsi fedha ambazo Mungu amepeana zimetumika kwa ubora. Kashfa za kifedha zimeharibu na kuangusha kanisa mingi na ni kwa sababu ya ukosaji wa uwajibikaji na uwazi.Kuweka risiti za kila mradi inaeza kua kazi ngumu lakini kanisa inafaa kulinda rekodi hizi vile fedha zinatumika kwa malipo, faida, ununuzi na kwa urekebishaji n.k. Umati unafaa kuwa na uaminifu kwa uwezo wa viongozi wao katika utumizi wa fedha za kanisa. Bwana wake akamwambia, "Vema mtumishi mwema na mwaminifu. Umekuwa mwaminifu katika mambo madogo, nitakukabidhi makubwa. Njoo ufurahi pamoja na bwana wako."(Mathayo 25:21)

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Fedha za kanisa zinafaa kuwa na uwazi gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries