settings icon
share icon
Swali

Je, divai au maji ya zabibu inapaswa kutumika kwa ushirika?

Jibu


Ikiwa inakubalika kugawa (na / au kupokea) divai wakati wa ushirika ni mjadala sahihi kati ya Wakristo. Tunapochunguza mada hii, tusipoteze maana kwa suala kubwa, na hicho ndicho kile kinywaji katika kikombe kinawakilisha — damu iliyomwagwa ya Bwana na Mwokozi wetu kuanzisha Agano Jipya.

Kwanza, maelezo ya juu ya suala la divai katika Maandiko. Utumiaji wa divai katika nyakati za Agano la Kale ni wazi sana. Tunaona matumizi yake kwanza (au matumizi mabaya) wakati Nuhu alipolewa na akalala uchi katika hema yake (Mwanzo 9:21). Baadaye, tunaona Mfalme Melkizedeki kumhudumia Abramu divai (Mwanzo 14: 17-18). Katika Kutoka 29:40 Mungu anaamuru matumizi ya divai kama sehemu ya mfumo wa dhabihu. Wakati Daudi alipofanywa mfalme, watu wake walisherekea siku tatu kwa chakula na divai (1 Mambo ya Nyakati 38-40). Kwa kweli, Zaburi 104: 15 inatuambia kwamba Mungu alifanya divai ambayo "hufurahisha mioyo ya wanadamu." Sisi pia tuna ahadi ya kwamba Bwana atawaandalia watu wake sikukuu ya vyakula vinono ambavyo vitajumuisha "karamu ya divai mzee" (Isaya 25: 6).

Katika Agano Jipya, muujiza wa kwanza wa Yesu ulikuwa kubadilisha maji kuwa divai katika harusi ya Kana (Yohana 2: 1-11). Na Bwana wetu hakunywa tu divai mwenyewe (Luka 7:34) lakini alisema angekunywa mbinguni pamoja nasi (Mathayo 26:29). Zaidi ya hayo, mtume Paulo alimwambia Timotheo kutumia divai badala ya "maji tu" ili afanye tumbo lake vyema (1 Timotheo 5:23).

(Licha ya marejeo ya mara kwa mara ya divai katika Biblia, ni dhahiri kuwa ulevi haukubaliki kabisa.Waefeso 5:18 inasema hivi kwa hakika: "Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho.")

Kwa hiyo, wasaidizi wa kunywa divai katika ushirika wana Maandiko ya kutosha kusaidia msimamo wao, na mifano hapo juu (isipokuwa Nuhu) huonyesha jinsi divai, wakati inatumiwa vizuri na kwa kiasi, inaweza kuwa jambo jema.

Wale ambao wanahisi mvinyo haupaswi kutumiwa pia wanafanya hoja zito, na wao, pia, wana marejeo ya maandiko ya kutaja. Ona, kwa mfano, onyo dhidi ya divai katika Mithali 4:17; 20: 1 na 23: 29-32. Na katika Mambo ya Walawi 10: 9 Bwana anamwambia Haruni kwamba yeye na wanawe hawakupaswa kunywa divai wakati waliingia katika hema ya kukutania, chini ya adhabu ya kifo.

Divai au maji ya zabibu katika Meza ya Bwana? Hakuna kanuni ngumu na ya haraka ya kibiblia ambayo inasema ni moja gani ya kupendekelewa au kukubalika zaidi. Kwa kweli, vifungu vinavyohusika na Meza ya Mwisho kamwe huitaji hata "divai" au "maji ya zabibu"; wao tu hutaja "kikombe." Hata hivyo, kuna baadhi ya mambo muhimu ya kuzingatia. Ikiwa uwepo wa pombe utakuwa shida kwa njia yoyote, basi hiyo ni wasiwasi halali. Kwa hakika, hakuna kanisa linataka kuona mtu aondoke kwa ushirika kwa sababu ana imani juu ya matumizi ya pombe. Mafundisho ya Kristo ilikuwa kwamba kanisa "fanyeni hivi, kila mnywapo, kwa kukumbusho wangu" (1 Wakorintho 11:25). Ingekuwa huruma kwa uwepo wa divai ili kusababisha mtu kupoteza mwelekeo na hivyo kupuuza amri ya Kristo.

Hakuna popote katika Neno la Mungu tunaloona sharti lililohusiana na kiwango cha uchochefu wa yaliyomo kwa kikombe. Hata hivyo, kama mtu ana maoni yenye nguvu ama njia kuhusu kile kinachoheshimu Mwokozi, ni vyema kushikilia imani hiyo. Lakini tunapaswa kuwa makini tusisahau kile kikombe kinawakilisha na tusihukumu ndugu au dada katika Kristo katika masuala ya maoni ya kibinafsi.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, divai au maji ya zabibu inapaswa kutumika kwa ushirika?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries