settings icon
share icon
Swali

Dini ya kweli ni gani?

Jibu


Dini yaweza elezewa kuwa “imani katika Mungu au miungu ya kuabudiwa, ambayo yadhihirishwa katika matendo au matambiko” au “mfumo maalumu wa imani, ibada, na kadhalika, ambao kila mara wahuzisha mfumo wa maadili.” Zaidi ya 90% ya idadi ya watu duniani wanafuata dini fulani. Shida ni kwamba, kunayo dini nyingi sana tofauti. Ni dini gani iliyo kweli? Dini ya kweli ni gani?

Mambo mawili makuu katika dini ni sheria na kanuni. Dini zingine si dini ila ni taratibu za sheria za kufanya na za kutofanya, ambazo mtu lazima azitunze ili ahesabiwe kuwa muumini mwaminifu wa dini, na papo hapo hana ubaya na Mungu wa huyo dini. Mifano miwili ya dini mbili ambazo ni za sheria ni Islamu na Kiyahudi. Islamu iko na nguzo zake tano ambazo ni lazima zitunzwe. Kiyahudi iko na mamia ya amri na tamaduni ambazo zinatunzwa. Dini hizi zote, katika kiwango fulani zasema kuwa kwa kuzitii sheria za dini mtu atachukuliwa kuwa wa Mungu.

Dini zingine zaangazia sana katika kuzitimiza kanuni. Kwa kutoa kafara hizi, kutenda jukumu hili, kushiriki katika ibada, kula chakula hiki na mengine, mtu amefanyika kuwa vizuri na Mungu. Mfano mkuu wa dini ambayo ni ya kanuni ni kanisa la Kikatholiki. Kanisa la Kikatholiki laamini kuwa kwa kubatizwa kwa maji ukiwa mtoto, kwa kushiriki katika misa, kwa kukiri dhambi zako kwa kuani, kwa kuomba kwa watakatifu mbinguni, kwa kupakwa mafuta na kuani kabla ya kifo na mengine, Mungu atakubalia mtu kama huyo kuingia mbinguni baada ya kifo. Ubudha na Uhindu pia ni dini za kanuni, lakini kwa kiwango kidogo zinaweza kuchukuliwa kuwa za sharia.

Dini yakweli sio ile ya kuangazia sheria bali ya kanuni. Dini ya kweli ni uhusiano na Mungu. Mambo mawili ambayo dini zote zashikilia ni kwamba mwanadamu kwa njia moja au nyingine ametengwa kutoka kwa Mungu na anahitaji kupatanishwa Naye. Dini za uongo zatafuta kuzuluhisha shida hii kwa kutunza sheria au kanuni. Dini ya kweli yazuluhisha tatizo kwa kutambua kwamba ni Mungu pekee anaweza kurekebisha utengano, na amekwisha fanya. Dini ya kweli yatambua yafuatayo:

• Wote tumetenda dhambi na kwa hivyo tumetenganishwa na Mungu (Warumi 3:23).

• Kama hautarekebishwa, adhabu ya haki ya dhambi ni mauti na utengano na Mungu wa milele baada ya kufa (Warumi 6:23).

• Mungu alikuja kwetu kupitia Kristo Yesu na akafa kwa ajili yetu, akachukua adhabu ambayo tulistahili, na akafufuka kutoka kwa wafu ili adhihirishe kuwa kifo chake kulikuwa dhabihu iliyotosha (Warumi 5:8; 1Wakorintho 15:3-4; 2Wakorintho 5:21)

• Kama tutampokea Yesu kama mwokozi wetu, kuamini kifo chake kama fidia kamili ya dhambi zetu, tumesamehewa, tumeokolewa, kombolewa, patanishwa na kufanywa wenye haki na Mungu (Yohana 3:16; Warumi 10:9-10; Waefeso 2:8-9).

Dini ya kweli haina sheria wala kanuni, lakini kuna utafauti mkubwa. Katika dini ya kweli, sheria na tamaduni zafuatwa kwa sababu ya ile furaha ya wokovu Mungu amepeana- SIO juhudi za kupata wokovu. Dini ya kweli, ambayo ni Ukristo wa Biblia, iko na sheria za kutii (usiue, usifanye uzinzi, usinene uongo na mengine) na kanuni za kutimiza (ubatizo wa maji mengi kwa kuzikwa na kushiriki mesa ya Bwana/Mwili wa Yesu). Kwa kuzitunza hizi sheria na tamaduni sio eti ndio vitu vinavyo mfanya mtu awe mkamilifu kwa Mungu. Bali sheria na kanuni hizi ni matokeo ya uhusiano na Mungu, kwa neema kupitia kwa imani katika Yesu Kristo pekee kama mwokozi. Dini ya uongo ni kufanya mambo kama (sheria na kanuni) ili ujaribu kupata kibali cha Mungu. Dini ya kweli ni kumpokea Yesu Kristo kama mwokozi na kuwa na uhusiano mwema na Mungu- na basi kufanya mambo kama (sheria na kanuni) kwa kumpenda Mungu and kutamani kukua karibu na Yeye.

Je, umefanya uamuzi kwa Kristo kwa kile ulicho soma hapa? kama ndiyo, tafadhali bonyeza kwa “Nime mkubali Kristo hivi leo” hapo chini.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Dini ya kweli ni gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries