settings icon
share icon
Swali

Je, dini huru itafutayo ukweli na maana ni nini?

Jibu


Dini huru itafutayo ukweli na maana ni kikundi kidogo, lakini kilio na ushawishi mkubwa cha kidini. Upatanisho, uvumilivu, na maisha mbadala ni maneno ya ambayo yaliyotumiwa na hii dini.

Jina la hii dini linatokana na kukataa mafundisho ya Utatu na imani yao kwamba wanadamu wote hupata wokovu. Kwa mujibu wa Wafuasi wa hii dini, wazo kuwa mtu anaweza kwenda kuzimu haliambatani na tabia ya Mungu mwenye upendo. Mizizi yake inarudi hadi karne ya kumi na sita wakati imani ya wafuasi wa dini hii ilikuwa maarufu wakati wa urejesho. Mawazo yao yaliunganishwa pamoja wakati wa karne ya kumi na nane katika Amerika wakati wa kisasi hicho. Wasomi tajika wa wakati huo walikataa kuamini katika mafundisho hayo ya kibiblia kama uharibifu wa jumla na hukumu ya milele, lakini badala yake kukubali wazo la Mungu mwenye upendo ambaye hawezi kumfanya mtu ateseka.

Wafuasi wa dini hii hueka msingi wa imani yao hasa juu ya uzoefu wao wenyewe na hawajajitolea kwa mfumo wowote wa kidini. Wanaamini kwamba watu wana haki ya kuamua wenyewe nini cha kuamini na kwamba wengine hawapaswi kukiuka haki hii. Kwa hivyo, mwamini mmoja kama huyo anaweza kutegemea Ukristo huru, wakati mwingine anaweza kuegemea msingi wa kiroho wa kisasi kipya. Hakuna fundisho la kweli zaidi ya kuvumilia-kwa kila kitu isipokuwa Ukristo wa kibiblia. Wafuazi wa dini hii wanaona Biblia kama kitabu cha mashairi, hadithi, na mafundisho ya maadili, kitabu cha binadamu kabisa na si Neno la Mungu la kweli. Wanakataa maonyesho ya Biblia ya Mungu wa utatu, wakiacha wazo la Mungu hadi mawazo na uamuzi wa kila mtu.

Kwa wafuasi hawa, Yesu alikuwa mwalimu mzuri wa maadili, lakini hakuna zaidi. Yeye hakuchukuliwa kuwa Mungu mkuu, na kila muujiza unaohusishwa na Yeye unakataliwa kama kuwa nje ya sababu ya kibinadamu. Maneno mengi ya Yesu yaliyoandikwa katika Biblia yanaonekana kama maandishi juu ya sehemu ya waandishi. Miongoni mwa imani zao: Yesu hakukufa ili kuwaokoa wanadamu kutoka kwa dhambi, kwa kuwa mtu si mwenye dhambi aliyeanguka; msisitizo huwekwa juu ya uwezo wa wanadamu wa wema; dhambi imehusishwa tu, na neno lenyewe halitumiwi mara kwa mara; mtu anajiokoa kwa njia ya kujiboresha binafsi, wokovu ukiwa ni uzoefu wa kidunia tu, "mwanzo mpya" kwa ulimwengu unaozunguka. Hii ni muhimu sana, kwa kuwa kifo ni cha mwisho. Wafuasi wa dini hii wengi wanakataa kuwepo kwa maisha baada ya kifo, kwa hivyo yote tuliyo nayo duniani ni yote tutaweza kupata.

Biblia, kwa upande mwingine, inakataa uongo huu. Yesu anaokoa wanadamu, ambao ulikuwa katika hali ya kuanguka tangu bustani ya Edeni na kujitenga na Mungu kwa dhambi (Yohana 10:15, Waroma 3: 24-25, 5: 8, 1 Petro 2:24). Mtu si mzuri, lakini ni mwenye dhambi na aliyepoteza. Ni kwa njia ya neema ya Mungu na imani katika damu iliyomwagika ya Kristo msalabani kwamba wanadamu wanaweza kuunganishwa na Mungu Mtakatifu, Mungu mkuu wa vyote (Mwanzo 2: 16-17; 3: 1-19; Yohana 3:36; 3:23, 1 Wakorintho 2:14, Waefeso 2: 1-10, 1 Timotheo 2: 13-14, 1 Yohana 1: 8).

Dini huru itafutayo ukweli na maana haina kitu chochote sawa na Ukristo wa kibiblia. Ni injili ya uongo, mafundisho yake ni kinyume na Biblia, na wanachama wake wanapinga sana imani za jadi, za kibiblia za Kikristo (huku wakidai kuwa huru na hawana ubaguzi au nia mbaya ya aina yoyote). Bibilia inakataa waziwazi dini hii katika hoja zake zote kuu za mafundisho yake.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, dini huru itafutayo ukweli na maana ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries