Swali
Kuna elezo gani la dhehebu?
Jibu
Wakati tunasikia neno “dhehebu,” kila mara twafikiria kikundi ambacho chamwabudu Shetani, chatoa dhabihu ya wanyama, au kushiriki katika maovu, vioja, na tamaduni za kidunia. Hata hivyo kwa kweli, madhehebu mengi yanaonekana kuwa hawana habari yo yote. Elezo kamili la Kikristo la madhehebu ni “kikundi cha dini ambacho chakana moja au zaidi ya misingi halisi ya ukweli wa Bibilia.” Kwa njia rahisi, dhehebu ni kikundi ambacho chafunza kitu Fulani ambacho kitamfanya mtu abaki awe hajaokoka ikiwa atakiamini. Kama alama kuu ya kitambulisho kutoka kwa dini, dhehebu ni kikundi ambacho chadai kuwa sehemu ya dini, huku kikikana misingi halisi ya ukweli wa dini hiyo. Dhehebu la kikristo ni kikundi ambacho kinakana mojawapo au zaidi ya misingi halisi ya ukweli wa kikristo, huku kikidai kuwa Wakristo.
Mafunzo mawili makuu ya madhehebu ni kuwa Yesu hakuwa Mungu na kuwa wokovu sio kwa imani peke. Kataa la uungu wa Kristo ilipelekea kuwa kifo cha Yesu hakitoshi kulipia dhambi zetu. Kataa kuwa wokovu hauji kwa imani peke yaleta dhana kuwa tutapata wokovu kwa matendo yetu, kitu ambacho bibilia inakataa. Mifano miwili ambayo inajulikana sana ya madhehebu ni Mashahidi wa Yehova na Wamomoni. Vikundi hivi vyote viwili vinadai kuwa Wakristo, huku wote wakikana uungu wa Kristo na wokovu kwa imani. Mashahidi wa Yehova na Wamomoni wanaamini mambo mengi ambayo yanakubaliana au yamefanana na yale ambayo Bibilia yafunza. Ingawa dhana kwamba wanakana uungu wa Kristo na kuhubiri wokovu kwa matendo yawafanya kuhitimu kuwa dhehebu. Wengi wa Washahidi wa Yehova, Wamomoni na washirika wa madhehebu mengine ni “watu wazuri” ambao kwa kweli wanaamini kuwa wanashikilia imani ya kweli. Sisi kama Wakristo, tumaini letu na maombi yetu lazima yawe kwamba watu wengi ambao wamejihuzisha na madhehebu watauona uongo na wavutwe karibu na ukweli wa wokovu kupitia kwa imani iliyo katika Kristo peke.
English
Kuna elezo gani la dhehebu?