Dhambi zote ni sawa?


Swali: "Dhambi zote ni sawa?"

Jibu:
Katika Mathayo 5:21-28 Yesu anasawazisha kutenda uzinzi na kuwa na tamaa katika moyo wako, kuua na kuwa na chuki kwa moyo wako. Ingawa, hii haimanishi kuwa dhambi zote ni sawa. Chenye Yesu alijaribu kuleta karibu na Mafarisayo ni kwamba dhambi bado ni dhambi hata kama ulinuia kufanya tendo bila, hata bila kulitenda. Viongozi wa dini wa wakati wa Yesu walifunza kuwa ilikuwa sawa kufikiria juu ya kitu cho chote ulitaka, bora tu usifanye tendo juu ya hizo thamanio. Yesu anawalazimisha kugundua kwamba Mungu anahukumu mawazo ya mtu vilevile na matendo. Yesu alitangaza kuwa matendo yetu ni matokeo ya yale yaliyo katika mioyo yetu (Mathayo 12:34).

Kwa hivyo ingawa Yesu alisema kwamba tamaa na uzinzi zote ni dhambi, hiyo haimanishi kuwa ziko sawa. Itakuwa mbaya sana ukiua mtu kuliko kuchukia mtu, hata kama zote ni dhambi mbele za Mungu. Kuna viwango vya kusini. Dhambi zingine ni mbaya zaidi ya zingine. Kwa wakati huo huo kuambatana na madhara yote ya milele na wokovu, dhambi zote ni sawa. Kila dhambi itaelekeza kwenye hukumu ya milele (Warumi 6:23). Dhambi zote, haijalishi jinsi ilivyo “ndogo” ni kinyume na Mungu asiye na mwisho na wa milele na kwa hivyo anastahili hukumu isiyo na mwisho na ya milele. Zaidi, hakuna dhambi “kubwa” sana ambayo Mungu hawezi samehe. Yesu alikufa ili alipe hukumu ya dhambi (1 Yohana 2:2). Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zetu zote (2 Wakorintho 5:21). Je! Dhambi zote ni sawa? Naam na La. Kwa ukali? La. Kwa adhabu? Naam. Kwa msamaha? Naam.

English
Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Dhambi zote ni sawa?

Jua jinsi ya ...

kutumia milele na MunguPata msamaha kutoka kwa Mungu