settings icon
share icon
Swali

Ni dhambi gani ya uasi?

Jibu


Yakobo 4:17 inasema, " Basi yeye ajuaye kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi." Dhambi ya uasi ni dhambi ambayo hutokea tunapokosa kufanya yale neno la Mungu linafundisha kwamba tunapaswa kufanya. Kwa ujumla hutumiwa kinyume na maneno yanayoafikiana "dhambi ya kusudia," au dhambi ambazo mtu hufanya kikamilifu. Paulo anafafanua dhana mbili katika Warumi 7: 14-20. Anatia hatia tabia yake kwa aina zote mbili za dhambi. Anatenda lile ambalo hataki kutenda na anajua si sahihi-dhambi ya kusudia-na hatendi lile analojua anapaswa kutenda na kwa kweli anataka kutenda-dhambi ya uasi. Hii inaonyesha picha ya asili mpya katika mgogoro na mwili inayokaa ndani yake.

Katika Agano Jipya, mfano mzuri uliotolewa na Yesu ni hadithi ya Msamaria Mzuri. Baada ya mtu kupigwa na kuachwa bila msaada, wanaume wawili wa kwanza kupita-kuhani na Mlawi, wote wawili walijua la kufanya, ila hawakufanya lolote. Mtu wa tatu, Msamaria, alisimama kuonyesha huruma kwa mtu aliyehitaji msaada (Luka 10: 30-37). Yesu alitumia mfano huu kufundisha kwamba sisi pia tunapaswa kusaidia wale walio na mahitaji. Kwa kufanya hivyo, alieleza kwa wazi kwamba ni dhambi kuepuka kufanya mema, kama vile ni dhambi kutenda mabaya.

Yesu anaeleza tena dhambi za kuasi katika Mathayo 25: 31-46. Mbuzi, wale ambao walifukuzwa na Kristo, ni wale ambao waliona wengine wana njaa na kiu, lakini hawakutoa chakula na maji. Wao ndio waliona wengine wanaohitaji mavazi, ambao walikuwa wagonjwa au katika jela lakini hawakuwa na kitu cha kuvaa au kuwafariji. Hii ni mifano ya dhambi za uasi. Hakukuwa na dhambi iliyofanyika dhidi ya watu hawa masikini-hawakuwa na njaa ya kimakusudi au kunyimwa nguo zao. Lakini dhambi ya uasi ilifanyika wakati wale ambao wangeweza kuwapa walichagua kutowapa.

Hatimaye, mtume Paulo anatoa muhtasari wa taarifa inayoelezea kwa nini tunapaswa kufanya yaliyo sahihi na kujiepusha na dhambi za uasi: "Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho."(Wagalatia 6: 9). Tunapofanya mapenzi ya Baba yetu wa mbinguni (Mathayo 12:50), tunaepuka dhambi za uasi na kuishi maisha mazuri, maisha yenye matunda yanayompendeza Mungu (Warumi 12: 1-2; Yohana 15: 1-11).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni dhambi gani ya uasi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries