settings icon
share icon
Swali

Dhambi saba mbaya sana ni zipi?

Jibu


Dhambi saba mbaya sana ni orodha hasa iliyotumika katika mafundisho ya Wakristo wa kwanza kuelimisha na kuonya wafuasi kuhusu mwanadamu aliyeanguka na kuendelea kutenda dhambi. Eleo mbaya juu ya dhambi saba “mbaya sana” ni kwamba ni zile dhambo ambazo Mungu hawezi kuzisamehe. Bibilia ii wazi kwamba dhambi pekee ambayo Mungu hataisamehe ni ile ya kuendelea kutokuwa na imani, kwa sababu inakataa njia pekee ya kupokea msamaha-wa Yesu Kristo na kifo chake mbadala msalabani.

Je! Hoja ya dhambi saba mbaya sana ni ya kibibilia? Naam na La. Methali 6:16-19 yasema, “ Kuna vitu sita anavyovichukia BWANA, naam, viko saba vilivyo chukizo kwake: 1) Macho ya kiburi, 2) Ulimi wa uongo, 3) Mikono imwagayo damu isiyo na hatia, 4) Moyo uwazao mawazo mabaya, 5) Miguu iliyo myepesi kukimbilia maovu, 6) Shahidi wa uongo asemaye uongo, 7) Naye apandaye mbegu za fitina kati ya ndugu.” Ingawa orodha hii sio ile ambayo watu wengi waielewa kama dhambi saba chukizo kwa Mungu.

Kulingana na Papa Gregory mkuu katika karne ya 6, dhambi saba chukizo kwa Mungu ni hizi zifuatazo: kiburi, husuda, ulafi, tamaa, hasira, uroho, na uzembe. Ingawa hizi ni dhambi sizizo weza katawaliwa, hazijawai patiwa elezo la “dhambi saba mbaya sana” katika Bibilia. Orodha ya kale ya dhambi saba mbaya sana inaweza fanya kazi kama njia nzuri ya kuratibisha aina mbali mbali ya dhambi ambazo ziko. Takribani kila aina ya dhambi itaorodheshwa jini ya hii orodha saba ya dhambi mbaya sana. Cha muimu sana ni, lazima tugundue kwamba hizi dhambi saba si chukizo tena kuliko dhambi zingine. Dhambi zote zinaleta kifo (Warumi 6:23). Sifa na kwa Mungu kwamba kupitia Kristo Yesu, dhambi zetu zote, pamoja na hizi “dhambi saba mbaya sana” zinaweza samehewa (Mathayo 26:28; Matendo Ya Mitume 10:43; Waefeso 1:7).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Dhambi saba mbaya sana ni zipi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries