settings icon
share icon
Swali

Dhambi mbaya zaidi ni ipi?

Jibu


Kwa kadri ikilinganishwa na utakatifu wa Mungu, dhambi zote ni sawa. Kila dhambi, kuanzia hamaki, hadi mauaji, uongo wa wazi hadi uzinzi, zote zitaongoza katika hukumu ya milele (Yakobo 4:17; Warumi 6:23). Dhambi zote, haijalishi ni “ndogo kiasi gani,” huwa kinyume na asili na mapenzi ya Mungu aisye na mwisho na wa milele na kwa hiyo inastahili adhabu isiyo na kikomo na ya milele (Isaya 13:11). Kwa sababu hii, hakuna dhambi “mbaya” zaidi kuliko zingine.

Kwa hivyo hakuna dhambi “mbaya” kwamba dhambi zote ni mbaya, kwa asili dhambi zote ni ovu. Wenye dhambi wote wanapungukiwa na utukufu wa Mungu (Warumi 3:23). Lakini tafakati njia nyingine, dhambi zote ni sawa angalau kwa sababu mbili:

Kwanza, dhambi zote sio sawa katika matokeo yao ya kidunia. Ingawa tamaa na uzinzi ni dhambi, uzinzi wa mara moja utakuwa na madhara mabaya zaidi kuliko dhambi zingine. Matokeo ya kuwa na tamaa ndani ya moyo wa mtu hayatakuwa makubwa kama kufanya tendo la kimwili la uzinzi. Ndivyo ilivyo katika kuburudisha mawazo ya tamaa dhidi ya wizi. Dhambi zote ni mbaya, lakini si dhambi zote zina adhabu sawia katika ulimwengu huu. Kwa maana hiyo, dhambi zingine ni mbaya zaidi kuliko zingine.

Maandiko yanabainisha dhambi ya zinaa kuwe yenye athari ya kipekee kwa mwenye anaifanya: “Ikimbieni zinaa. Dhambi zingine zote atendazo mtu ziko nje ya mwili wake, lakini yeye aziniye hutenda dhambi ndani ya mwili wake mwenyewe” (1 Wakorintho 6:18). Katika kifungu hiki, usherati umewekwa katika kitengo tofauti na dhambi zingine kwa kuwa na athari ya moja kwa moja kwenye mwili wa mtu. Je, hii inamaanisha kuwa dhambi ya zinaa labda ni dhambi “mbaya” zaidi? Kwa hakika inamaanisha kwamba dhambi zinazohusisha usherati zina matokeo mabaya zaidi katika ulimwengu huu.

Pili, sio dhambi zote ziko sawa katika kiwango cha adhabu ya milele. Akitoa maelezo kuhusu hitaji la kuwa tayari kwa ujio wake, Yesu alizungumza kuhusu viwango tofauti vya adhabu: “Yule mtumishi anayefahamu vyema mapenzi ya bwana wake na asijiandae wala kufanya kama apendavyo bwana wake, atapigwa kwa mapigo mengi. Lakini yeyote ambaye hakujua naye akafanya yale yastahiliyo kupigwa, atapigwa kidogo. Yeyote aliyepewa vitu vingi, atadaiwa vingi; na yeyote aliyekabidhiwa vingi, kwake vitatakiwa vingi” (Luka 12:47-48). Kwa hivyo dhambi za ufidhuli na uzembe zinahitaji adhabu kubwa katika hukumu ya mwisho kuliko dhambi zilizofanywa kwa kutojua. Kuzimu kuna joto, lakini kunaweza kuwa moto ziadi kwa wengine. Kwa hali hiyo, dhambi zingine ni mbaya zaidi kuliko zingine.

Lazima tujilinde dhidi ya dhana tatu kuhusu dhambi “mbaya” zaidi:

Kwanza, iwapo kuna dhambi “mbaya” zaidi, hiyo haimaanishi kwamba dhambi zingine si mbaya na zimeruhusiwa. Dhambi ni dhambi, na zote si haki.

Pili, tusianguke katika mtego wa kulinganisha dhambi zetu na za wengine. Tunapojilinganisha, kila wakati tutahitimisha kwamba watu wengine wanafanya dhambi “mbaya zaidi” kutuliko sisi; dhambi zetu kwa namna fulani ni “bora.” Jambo letu la kwanza linapaswa kuwa kuhusu dhambi zetu wenyewe, kama ni mbaya, na si dhambi za wale wanaotuzunguka (Mathayo 7:4-5). Kiwango cha Mungu sio jinsi tunavyopima watu wengine bali ni jinsi tunavyojipima na Kristo.

Tatu, hata kama kuna dhambi “mbaya zaidi,” Mungu bado anaweza kuisamehe. Kama vile ilivyo kuwa hakuna dhambi ndogo sana ambay haistahili adhabu, hakuna dhambi kubwa sana ambayo Mungu hawezi kuisamehe. Wakati kahaba aliyetubu alipomjia Yesu, alipata neema; kisha Yesu akawaambia watazamaji, “Kwa hiyo, nakuambia, dhambi zake zilizokuwa nyingi zimesamehewa” Luka 7:47). Na Mungu amekwisha msamehe mtu yule tayari anajiona kuwa “mwovu kuliko wengine wote” (1 Timotheo 1:15). Yesu alikufa ili kulipa adhabu ya dhambi zote (Yohana 3:16; 1 Yohana 2:2). “Kwa maana Mungu alimfanya yeye asiyekuwa na dhambi kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kufanywa haki ya Mungu kwake yeye” (2 Wakorintho 5:21). Kwa muumini, hakuna dhambi dhabihu ya Yesu haiwezi kufunika (ona Warumi 8:1).

Mungu anachukia dhambi. Kwa bahati, Ametoa njia ya “kututakasa na uovu” (1 Yohana 1:8-10) kupitia kwa Mwanawe, Yesu Kristo (Yohana 3:17). Baba yetu wa Mbinguni “anayetaka watu wote waokolewe na wafikie kuijua kweli” (1 Timotheo 2:4).

Katika hitimizo la mwisho, tunaweza, tunaweza kusema kwamba dhambi “mbaya” zaidi ni kutoamini. Imani katika Kristo ni jinsi watu wanavyoitikia kwa usahihi toelo la Mungu la wokovu. “je, sisi tutapaje kupona kama tusipojali wokovu mkuu namna hii? (Waebrania 2:3). Kumkataa Mwokozi ni kukubali adhabu ya dhambi ya mtu mwenyewe.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Dhambi mbaya zaidi ni ipi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries