settings icon
share icon
Swali

Je! Dhambi ilitoka wapi?

Jibu


Mungu hakuumba dhambi, lakini aliwaumba viumbe wenye hiari huru ambao wana uwezo wa kutenda dhambi. Hii ni pamoja na Shetani, malaika walioanguka (mapepo), na wanadamu. Tukiifafanua wazi, dhambi ni kupungukiwa na viwango vya Mungu. Dhambi si kitu chenyewe hasa au kitu “kilichopo”; haina kiumbe huru. Badala yake, dhambi ni ukosefu wa kitu, kushindwa kutii kikamilifu amri za Mungu na kuishi kwa ajili ya utukufu Wake (Warumi 3:23).

Wakati aliumba anga na ulimwengu tuliomo, “Mungu akaona vyote alivyoumba, na tazama, ilikuwa vizuri sana” (Mwanzo 1:31; linganisha na 1 Timotheo 4:4). Uumbaji huo “mzuri sana” ulikuwa ni pamoja na wanadamu na malaika ambaoye baadaye alijulikana kama Shetani. Kufikia wakati huu, hakuna mwanadamu au malaika alikuwa ametenda dhambi, lakini walikuwa na uwezo wa kufanya hivyo. Mungu hakuumba kiumbe chochote chenye dhambi, lakini kundi la malaika lilimwasi Mungu mbinguni na kuwa wenye dhambi.

Kuanguka kwa Shetani kutoka mbinguni kumeelezewa kiishara katika Isaya 14:12-14 na Ezekieli 28:12-19. Malaika aitwaye Lusifa alitaka “kupaa mbinguni” na kuwa “juu ya nyota za Mungu” (Isaya 14:13). Mstari wa 14 unaongeza kwamba alitamani kujifanya “kama Yeye Aliye Juu Sana.” Mungu alimhukumu Lusifa kwa kumuondoa katika uwepo wa Wake unaoendelea (Isaya 14:15). Malaika huyo aliyeanguka sasa anajulikana kama Shetani (“adui”) au ibilisi (“mchochezi”).

Katika Ezekieli tunapata kwamba Shetani aliumbwa malaika mkamilifu, mwenye hekima na mzuri (Ezekieli 28:14). Lakini Shetani aliasi: “Ulikuwa mnyofu katika njia zako tangu siku ile ya kuumbwa kwako, hadi uovu ulipoonekana ndani yako” (aya ya 15). Hapo ndipo hali ilibadilika. Maandiko yanadokeza ni kwa nini Shetani alichagua kutenda dhambi: “Moyo wako ukawa na kiburi kwa ajili ya uzuri wako, nawe ukaiharibu hekima yako kwa sababu ya fahari yako.” (aya ya 17; pia soma 1 Timotheo 3:6). Anguko la Shetani lilitokea wakati fulani kabla ya kuwa joka na kumjaribu Hawa katika bustani ya Edeni katika Mwanzo 3. Baada ya kutupwa duniani (Ezekieli 28:17) Shetani aliwajaribu wanadamu kufanya dhambi, na ameendelea na mazoea hayo tangu wakati huo (ona Mathayo 4:1-11).

Tangu dhambi ya Adamu, wanadamu wemerithi uharibifu wa kiroho wa Adamu na wamezaliwa wakiwa na asili ya dhambi. Kwa kawaida tuna mazoea ya kutaka kutenda dhambi (Warumi 6-7; Yakobo 1:13-15). Lakini katika Kristo Yesu tunaweza kusamehewa dhambi zetu. “Kwa maana Mungu alimfanya yeye asiyekuwa na dhambi kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kufanywa haki ya Mungu kwake yeye” (2 Wakorintho 5:21). Tunapokea msamaha kutoka kwa adhabu ya milele ya dhambi tunapoweka imani yetu kwa Yesu. Pia tunapokea uhuru kutoka kwa utumwa wa dhambi na tanaweza kujifunza, kwa kujitoa kwa Roho Mtakatifu, kuishi kwa haki. Utaratibu huu wa kutenda kiasi kama Adamu na zaidi kama Kristo unaitwa utakaso.

Wengine wameshangaa ni kwa nini Mungu aliumba viumbe vinavyoweza kufanya dhambi. Mbona hangeweza kuumba malaika na wanadamu ambao hawana uwezo wa kutenda dhambi? Njia mbadala ingekuwa kuumba viumbe visivyoweza kuchagua mema na mabaya. Lakini katika hali hiyo, malaika na wanadamu wangekuwa kama roboti , ambao hawana uwezo wa kuonyesha upendo na shauku ya kweli kwa Bwana. Mungu angeweza kufanya dhambi isiwezekane, au Angeweza kufanya viumbe kuwa huru kuchagua, lakini hangeweza kufanya yote mawili kimantiki. Bila uwezo wa kuchagua, hakuna kiumbe anayeweza kuwa na uhusiano wa maana naye Mungu. Hakungekuwa na uzoefu wa maana wa rehema na upendo Wake, haki yake na uadilifu. Ukamilifu wa asili na utukufu wa Mungu haungeonyeshwa.

Kuwepo kwa dhambi sio jambo nzuri (Warumi 6:23), lakini sio mwisho wa hadithi. Shetani hatimaye atashindwa. Mwisho wake umetangazwa, na uovu wake hautaendelea milele (Ufunuo 20:7-10). Kupitia imani katika Yesu Kristo, tunaweza kupokea msamaha wa dhambi na ushirika uliorejeshwa na Mungu (Yohana 3:16; Waefeso 2:8-9). Uhusiano huu hutoa uzima wa milele pamoja na uzima tele kupitia uhusiano wetu na Bwana (Yohana 10:10). Yesu anashinda dhambi na kifo na kutuleta kwenye utimilifu wa uhusiano na Mungu wa ajabu(1 Wakorintho 15:50-58; Ufunuo 21-22).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Dhambi ilitoka wapi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries