settings icon
share icon
Swali

Je! Dhambi yangu binafsi, ya fargha inaathiri wengine aje?

Jibu


Ikiwa uliishi pekee kwenye kisiwa katikati ya bahari, labda dhambi yako ya faragha haitaathiri mtu yeyote bali wewe mwenyewe. Hata hivyo, tangu hekima ni "hakuna mtu ni kisiwa," kuna fursa nzuri ya kuwa una familia au angalau marafiki na jamaa unaowasiliana nao mara kwa mara. Wote wataathirika kwa njia fulani na dhambi kwa sababu dhambi ina matokeo (Warumi 6:23). Hiyo ni kanuni inayofuata mfano uliowekwa wakati wa uumbaji. Kila kitu kilichoumbwa kina mbegu ambayo hueneza yenyewe baada ya "aina" yake (Mwanzo 1:11, 21, 25). Kwa maneno mengine, huwezi panda nafaka na kutarajia kiazisukari wakati wa mavuno. Huwezi "kupanda" dhambi-hata kwa faragha-na husitarajie kuvuna matokeo ya mavuno. Na madhara yana njia ya kumwaga kwa kila mtu na mtu yeyote anayewasiliana nasi kwa sababu ya kanuni nyingine inayoitwa "ushirikiano." Hii ina maana kwamba wale walio karibu nawe wanaweza kubarikiwa au kuadhirika kwa kushirikiana na wewe na uchaguzi na matendo unayofanya, kwa faragha na hadharani.

Mtu anahitaji tu kutazama kashfa za hivi karibuni zinazojumuisha viongozi maarufu wa kiinjili kuona madhara ya dhambi za wengine za "faragha". Mara baada ya kugunduliwa-na Biblia inatuambia kuwa "nanyi jueni ya kwamba hiyo dhambi yenu itawapata hapana budi" (Hesabu 32:23) -familia, marafiki, makanisa, na jumuia ya Kikristo kwa ujumla itakuwa na madhara. Mbaya bado, sababu ya Kristo itaharibiwa kama wasioamini wanadhihaki na kukenua kwetu na kukashifu jina lake. Inaweza kuonekana kuwa watu hufanya dhambi bila matokeo yanayoonekana, lakini kilicho siri kitakuwa wazi siku moja . "Kwa maana hakuna neno lililositirika ambalo halitafunuliwa; wala lililofichwa ambalo halitajulikana na kutokea wazi" (Luka 8:17). Je, unasema kwa uaminifu kwamba hakuna mtu ambaye atakuwa ameathiriwa na dhambi zako za siri ikiwa zinapaswa kujulikana?

Dhambi iliyohifadhiwa kwa siri hutoa hatia, na hatia ina njia ya kutubadilisha. Wengine wanaona mabadiliko hayo na wanaathiriwa nayo. Labda mke, kwa mfano, hajui juu ya mazoea ya mumewe kwa picha za ngono, lakini mazoea yake uongoza kwa hatia ya usiri na mabadiliko katika hisia kuenda kwake kama mpenzi wake wa ngono. Anaona mabadiliko hayo na kutafakari juu ya sababu inayoweza kusababisha-hugundua kuwa hafutii, hampendi tena, au ana uhusiano.Wakati hakuna mambo haya yote ni ya kweli, matokeo ya dhambi yake ya "faragha" yanaweza kumdhuru, ndoa yao, na familia zao, hata kama siri yake haijulikani kamwe.

Hapa kuna kanuni nyingine ya kuzingatia. "Lakini unapoomba, ingia kwenye chumba chako, funga mlango na kumwomba Baba yako, asiyeonekana.Kisha Baba yako, ambaye anaona yanayofanyika kwa siri, atakupa zawadi ... ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi "(Mathayo 6: 6, 18). Tunapotafakari kutoka kwa Maandiko, tunaweza kuona kanuni hapa ambayo inaweza kutumika kwa njia nzuri na mbaya. Tunachofanya kwa siri, Mungu atatoa jazi waziwazi. Ikiwa tunaomba na kufunga kama BWANA, atatupa jazi. Hivyo, kusimamo kutafakari kwamba ikiwa tutafanya dhambi kwa siri, tutaweza pia "kulipwa" kwa wazi kwa hatua hiyo. Katika hali yoyote, Mungu anaona na anajua kuhusu dhambi, iwe faragha au ya umma, na haachilii dhambi iende bila kuadhibiwa.

Matokeo makubwa zaidi ya dhambi ya faragha, binafsi ni nafsi yetu ya kufa. Ezekieli 18: 4 inasema kwamba nafsi ambayo hufanya dhambi itakufa, na Warumi 6:23 inatuambia kwamba mshahara wa dhambi ni mauti. Hii inazungumzia mtu ambaye kwa asili, desturi ni mwenye dhambi bila faida ya upya wa uzima. Kwa mtoto aliyezaliwa tena wa Mungu-ambaye amemkubali Bwana Yesu Kristo kama mwokozi wake-kuna kiwango cha mwenendo, yote kwa faragha na kwa umma: "Kwa hivyo iwe unakula au kunywa au chochote unachofanya, fanya yote kwa utukufu wa Mungu "(1 Wakorintho 10:31). Mtoto wa Mungu aliyezaliwa tena ana hamu ya kuishi kumtukuza Mungu, na ingawa kuna nyakati ambapo tunaweza na kufanya kushindwa, Mungu ametupatia fursa ya kuwa katika ushirika na Yeye. Ameahidi kwamba, "ikiwa tutatubu dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na mwenye haki na atatusamehe dhambi zetu na kututakasa kutoka kwa udhalimu wote" (1 Yohana 1: 9).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Dhambi yangu binafsi, ya fargha inaathiri wengine aje?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries