settings icon
share icon
Swali

Ni dhabihu gani mbalimbali zilikuwa katika Agano la Kale?

Jibu


Kuna aina tano kuu za dhabihu, au sadaka, katika Agano la Kale. Sadaka ya kuteketezwa (Mambo ya Walawi 1; 6:8-13; 8:18-21; 16:24), sadaka ya nafaka (Mambo ya Walawi 2; 6:14-23), sadaka ya amani (Mambo ya Walawi 3; 7:11-34) ), sadaka ya dhambi (Mambo ya Walawi 4; 5:1-13; 6:24-30; 8:14-17; 16:3-22), na sadaka ya hatia (Mambo ya Walawi 5:14-19; 6:1- 7; 7:1-6). Kila moja ya dhabihu hizi ilihusisha mambo fulani, labda mnyama au tunda la shamba, na ilikuwa na madhumuni maalum. Wengi waligawanywa katika sehemu mbili au tatu-sehemu ya Mungu, sehemu ya Walawi au makuhani, na, ikiwa kuna sehemu ya tatu, sehemu iliyowekwa na mtu anayetoa dhabihu. Sadaka zinaweza kugawanywa kwa upana kama dhabihu ya hiari au ya lazima.

Dhabihu za Hiari
Kulikuwa na sadaka za hiari tatu. Ya kwanza ilikuwa sadaka ya kuteketezwa, tendo la hiari la ibada ya kuonyesha moyo wa ibada au kujitolea kwa Mungu. Pia ilitumiwa kama upatanisho kwa ajili ya dhambi isiyo ya kimakusudi. Mambo ya sadaka ya kuteketezwa yalikuwa fahali, ndege, au kondoo dume bila dosari. Nyama na mifupa na viungo vya mnyama vilikuwa vichomeke kabisa, na hii ilikuwa sehemu ya Mungu. Ngozi ya mnyama ilitolewa kwa Walawi, ambao baadaye wangeiuza ili kupata pesa kwa ajili yao wenyewe.

Sadaka ya pili ya hiari ilikuwa sadaka ya nafaka, ambayo matunda ya shamba yalitolewa kwa namna ya keki au mikate iliyooka iliyotengenezwa kwa nafaka, unga mwembamba, na mafuta na chumvi. Sadaka ya nafaka ilikuwa moja ya dhabihu iliyofuatana na sadaka ya kinywaji cha robo ya hini (karibu kwati) ya divai, ambayo ilimwagwa kwa moto kwenye madhabahu (Hesabu 15:4-5). Kusudi la sadaka ya nafaka lilikuwa kuonyesha shukrani katika kutambua utoaji wa Mungu na sifa njema kwa mtu anayefanya dhabihu. Wakuhani walipewa sehemu ya sadaka hii, lakini ilikuwa ikuliwe ndani ya ua wa hema.

Sadaka ya tatu ya hiari ilikuwa sadaka ya amani, ambayo ilijumuhisha mnyama yeyote asiye na dosari kutoka kwa kundi la wanyama la mwabudu, na/au nafaka mbalimbali au mikate. Hii ilikuwa dhabihu ya shukrani na ushirika ulifuatiwa na chakula cha pamoja. Kuhani Mkuu alipewa kidari cha mnyama; kuhani aliyeongoza alipewa mguu wa mbele wa kulia. Hivi vipande vya sadaka viliitwa "sadaka ya kupeperusha" na "sadaka ya kuinuliwa" kwa sababu vilipeperushwa au kuinuliwa juu ya madhabahu wakati wa sherehe. Mafuta, figo, na ndewe ya ini zilipewa kwa Mungu (kuteketezwa), na mabakio mengine ya mnyama yalikuwa ya washiriki kula, yakiashiria utoaji wa Mungu. Sadaka ya kiapo, sadaka ya shukrani, na sadaka ya hiari zilizotajwa katika Agano la Kale zote zilikuwa sadaka za amani.

Dhabihu za Lazima
Kulikuwa na dhabihu mbili za lazima katika Sheria za Agano la Kale. Ya kwanza ilikuwa sadaka ya dhambi. Madhumuni ya dhabihu ya dhambi ilikuwa kupatanishwa kwa dhambi na kusafisha kutokana na unajisi. Kulikuwa na vipengele vitano vya dhabihu ya dhambi-fahali mchanga, beberu, mbuzi wa kike, njiwa/njiwa, au 1/10 efa ya unga mwembamba. Aina ya mnyama alitegemea utambulisho na hali ya kifedha ya mtoaji. Mbuzi wa kike alikuwa sadaka ya dhambi kwa mtu wa kawaida, unga mwembamba ilikuwa dhabihu ya masikini sana, fahali mchanga alitolewa kwa ajili ya kuhani mkuu na kutaniko kwa ujumla, na kadhalika. Dhabihu hizi kila moja ilikuwa na maagizo maalum kuhusu kile cha kufanya na damu ya mnyama wakati wa sherehe. Sehemu za mafuta na ndewe la ini na figo zilipewa Mungu (kuteketezwa); mnyama aliyesalia angekuwa labda kuteketezwa kabisa juu ya madhabahu na majivu kutupwa nje ya kambi (katika kupatanisha kuhani mkuu na kutaniko), au kuliwa ndani ya ua ya hema.

Sadaka nyingine ya lazima ilikuwa sadaka ya hatia, na dhabihu hii ilikuwa mwana-kondoo pekee. Sadaka ya hatia ilitolewa kama upatanisho kwa dhambi zisizo za makusudi ambazo zilihitaji malipo kwa chama kilichokoshewa, na pia kama kusafishwa kutoka dhambi za kunajisi au magonjwa ya kimwili. Tena, sehemu za mafuta, figo, na ini zilitolewa kwa Mungu, na mwana-kondoo aliyebaki lazima angeliwa ndani ya ua ya hema.

Dhabihu katika Agano la Kale zilielezea dhabihu kamili na ya mwisho ya Kristo. Kama ilivyo kwa Sheria yote, dhabihu zilikuwa ni "kivuli cha mambo yajayo; ukweli, hata hivyo, hupatikana katika Kristo"(Wakolosai 2:17). Wakristo leo wanatambua kifo cha Kristo cha kupatanisha msalabani kama sadaka pekee ya dhambi inayohitajika, iliyotolewa mara moja na ya mwisho (Waebrania 10:1-18). Kifo Chake kilifungulia "mahali patakatifu" kwetu (Waebrania 10:19-22) ili tuweze kuingia kwa Mungu kwa uhuru na kutoa "sadaka yetu ya sifa" (Waebrania 13:15, tazama 9:11-28; 4:14; 5:10).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni dhabihu gani mbalimbali zilikuwa katika Agano la Kale?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries