settings icon
share icon
Swali

Je! Kutakuwa na dhabihu ya mnyama wakati wa ufalme wa milenia?

Jibu


Kuna vifungu kadhaa katika Agano la Kale ambavyo vinaonyesha wazi dhabihu ya wanyama itaanzishwa tena wakati wa ufalme wa milenia. Vifungu vingine vinaitaja kuwa ya kupita wakati maudhui ya ufalme wa milenia inajadiliwa, ni vifungu kama vile Isaya 56: 6-8; Zakaria 14:16; na Yeremia 33: 15-18.

Kifungu ambacho kina maelezo zaidi na ni pana ni Ezekieli 43:18-46:24. Lazima ikumbukwe kwamba hii ni sehemu ya vifungu vingi vinavyoshughulikia ufalme wa milenia, kifungu kinachoanza na Ezekieli 40. Katika Ezekieli 40, Bwana anaanza kutoa maelezo pana ya hekalu litakalo kuwepo wakati wa kipindi cha ufalme wa milenia, hekalu ambalo litadumaza hekalu zingine zimewai jengwa, hata lile la Herode ambalo lilikuwa kubwa sana, na lilikuwai kuwapo mwanzoni mwa huduma ya Kristo duniani.

Baada ya kupeana maelezo maalum ya upana na vile hekalu na madhabahu itaaonekana, Bwana anaanza kupeana maagizo zaidi ya mnyama ambaye atatolewa kama dhabihu (Ezekieli 43:18-27). Katika sura ya 44, Bwana anatoa maagizo ya ni nani anafaa kutoa dhabihu kwa Bwana. Bwana anakauli kuwa sio wote wa nyumba ya Lawi watatoa dhibihu ya damu na mafuta kwa Bwana kwa sababu ya dhambi waliyokwisha itenda hapo awali; itakuwa ni wale ni wale wanatoka katika uzao wa Zadoki (aya ya 15). Sura za 45 na 46 zinaendelea kutaja kuwa dhabihu za wanyama zitaendelea kutolewa.

Pingamizi la msingi lililotolewa kwa wazo la dhabihu za wanyama kurudiwa wakati wa ufalme wa milenia ni kwamba Kristo amekuja na kutoa dhabihu kamili kwa ajili ya dhambi, na kwa hivyo hakuna haja ya kutoa dhabihu ya wanyama kwa ajili ya dhambi. Walakini, ni lazima ikumbukwe kwamba dhabihu ya mnyama haikuondoa kamwe dhambi iliyotenganisha mtu kiroho na Bwana.

Waebrania 10:1-4, "Sheria ni kivuli tu cha mambo mema yajayo, wala si uhalisi wa mambo yenyewe. Kwa sababu hii, haiwezekani kamwe kwa njia ya dhabihu zitolewazo mwaka hadi mwaka kuwakamilisha wale wanaokaribia ili kuabudu. Kama dhabihu hizo zingeweza kuwakamilisha, hazingeendelea kutolewa tena. Kwa kuwa hao waabuduo wangekuwa wametakaswa mara moja tu, wala wasingejiona tena kuwa na dhambi. Lakini zile dhabihu zilikuwa ukumbusho wa dhambi kila mwaka, kwa sababu haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi."

Si sahihi kufikiria kuwa dhabihu ya wanyama iliondoa dhambi katika Agano la Kale, na vile vile sio sahihi kufikiria kuwa zitaondoa dhambi wakati wa ufalme wa milenia. Dhabihu za wanyama zilitumika kama somo kwa mwenye dhambi kwamba dhambi ilikuwa kitu mbaya zaidi dhidi ya Mungu, na kuwa matokeo ya dhambi ni kifo. Warumi 3:20 yasema, "Kwa hiyo hakuna binadamu hata mmoja atakayehesabiwa haki mbele za Mungu kwa matendo ya sheria, kwa maana sheria hutufanya tuitambue dhambi"

Wachanganuzi wengi wa kipindi kabla ya milenia hukubaliana kuwa kusudi la dhabihu ya mnyama wakati wa kipindi cha ufalme wa milenia ni ukumbusho katika hali. Jinsi vile Meza ya Bwana ni ukumbusho wa kifo cha Kristo kwa kanisa hii leo, dhabihu ya wanyama itakuwa ukumbusho wakati wa ufalme wa milenia. Kwa wale watakao zaliwa wakati wa kipindi cha ufalme wa milenia dhabihu ya wanyama bado itakuwa kitengo cha ukumbusho. Wakati wa kipindi hicho cha baadaye, haki na uadilifu zitanawili, bali wale walio na miili ya dunia bado watakuwa na hali ya dhambi, na kutakuwa na haja ya kufundisha juu jinsi dhambi ilivyo uasi kwa Mungu mtakatifu na mwenye haki. Dhabihu za wanyama zitatumika kwa kusudi hilo, "Lakini zile dhabihu zilikuwa ukumbusho wa dhambi kila mwaka" (Waebrania 10:3).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Kutakuwa na dhabihu ya mnyama wakati wa ufalme wa milenia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries