settings icon
share icon
Swali

Je! Ni kwa nini mfumo wa dhabihu ulihitaji kafara ya damu?

Jibu


Katika Agano la Kale lote, kila kitabu kinalenga katika Dhabihu Kuu, ambayo ilikuwa inakuja-ile ya Yesu kujitolea kwa kuyatoa maisha yake kwa ajili yetu. Mambo ya Walawi 17:11 ni kiungo muhimu cha Agano la Kale cha kauli kuhusu umuhimu wa damu katika mfumo wa dhabihu. Mungu akizungumza na Musa anasema: "Kwa kuwa uhai wa kiumbe uko ndani ya damu, nami nimewapa hiyo damu ili mfanyie upatanisho kwa ajili yenu wenyewe juu ya madhabahu; damu ndiyo ifanyayo upatanisho kwa ajili ya maisha ya mtu."

"Dhabihu" hufafanuliwa kama sadaka ya kitu cha thamani kwa ajili ya kusudi au sababu. Kufanya upatanisho ni kumridhisha mtu au kitu kwa kosa alilifanya. Aya ya Mambo ya Walawi inaweza kusomwa vyema sasa: Mungu alisema, "Nami nimewapa (uhai wa kiumbe, ambao uko ndani ya damu) ili ujifanyie upatanisho (ufunike makosa ambayo umefanya dhidi yangu)." Kwa maneno mengine, wale ambao wamefunikwa na damu ya dhabihu wamewekwa huru kutoka kwa madhara ya dhambi.

Ijapokuwa Waisraeli hawakumjua Yesum au jinsi angekufa kwa niaba yao na kisha kufufuka tena, lakini waliamini kuwa Mungu atawatumi Mwokozi. Kati ya dhabihu zote nyingi za damu zinazoonekana katika Agano la Kale zilikuwa mfano wa dhabihu ya kweli, moja lakini ya nyakati zote itakayokuja ili Waisraeli wasiweze kusahu hili, bila damu, hamna msamaha. Umwagikaji huu wa damu ni tendo la mbadala. Kwa hivyo, maneno ya mwisho ya Mambo ya Walawi 17:11 yanaweza kusomwa "damu 'inafanya upatanisho' kwa gharama ya maisha" (kwa mfano maisha ya mnyama) au "kufanya upatanisho kwa niaba ya uhai" (mfano, maisha ya mwenye dhambi, Yesu Kristo akiwa ni Yeye mmoja ambaye anatoa uzima kupitia damu Yake iliyomwagika).

Waebrania 9:11-18 inathibitisha uashiriaji wa damu kama uhai na inatumika katika Mambo ya Walawi 17:11 kuashiria dhabihu ya Bwana Yesu Kristo. Aya ya 12 inasema wazi kuwa dhabihu ya damu ya katika Agano la Kale, zilikuwa za muda na za kusamehe dhambi kwa sehemu na kwa muda mfupi, na hivyo kuwa na haja kurudia dhabihu kila mwaka. Lakini wakati Kristo aliingia Mhali Patakatifu pa Patakatifu, alifanya hivyo kutoa damu Yake mara moja kwa nyakati zote, na kufanya dhabihu ya baadaye kutohitajika. Hili ndilo Yesu alimaanisha kwa maneno yake ya kufa msalabani: "Yote yameisha" (Yohana 19:30). Kamwe tena damu ya ng'ombe na mbuzi haitasafisha mwanadu toka kwa dhambi yake. Ni kwa kukubali damu ya Yesu, iliyomwagika msalabani kwa ondoleo la dhambi, tunaweza kusimama mbele za Mungu tukiwa tumefunikwa na haki ya Kristo (2 Wakorintho 5:21).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Ni kwa nini mfumo wa dhabihu ulihitaji kafara ya damu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries