settings icon
share icon
Swali

Je, uraibu wa buni ni dhambi?

Jibu


Wakorintho wa Kwanza 6:12 inasema, "Vitu vyote ni halali kwangu, lakini si vyote vifaavyo; vitu vyote ni halali kwangu, lakini mimi sitatiwa chini ya uwezo wa kitu cho chote." Hakuna mahali popote Biblia inataja ubuni, hivyo suala la kulewa kwa ajili ya buni halijatajwa moja kwa moja katika Biblia. Zote ambazo zinaweza kufanywa ni kuchukua kanuni za kibiblia ambazo zinatumika kwa kuwa mraibu kwa chochote, na kisha kutumia kweli hizo kwa kulewa kwa buni. Wakorintho wa Kwanza 6:12 inaweza kutumiwa katika kuhusisha maandiko. Wakati mazingira yanapohusiana na uasherati wa kijinsia, maneno ya Paulo yanapita wazi zaidi uasherati wa kijinsia wakati anasema, "Mimi sitatiwa chini ya uwezo wa kitu cho chote."

Sawa na ulavi, uraibu wa kahawa ni kitu ambacho Wakristo mara nyingi huwa wanafiki. Wakristo kwa haraka uhukumu uraibu wa pombe na tumbaku, lakini hupuuza zile ambazo "zimekubalika kijamii" uraibu kama vile kula zaidi na buni. Pombe kwa wazi inaweza kuwa na madhara zaidi juu ya tabia na inaweza kuwa na madhara kwa afya wakati unatumiwa vibaya. Tumbaku ni hatari kwa afya hata kama ni kwa kiasi kidogo. Kwa kulinganisha, kahawa inaweza kuwa si mbaya sana, lakini "si mbaya kama ..." sio kitu ambacho Wakristo wanapaswa kuishi kwayo. Badala yake, Wakristo wanapaswa kuishi kwa "Je, ni bora? Je, inamheshimu Mungu? "

Buni, kwa kiasi cha kutosha, sio hatari zaidi kwa afya au uraibu. buni, kwa kiasi kikubwa, ni madhara kwa afya na raibu. Je, ni makosa kuwa na kikombe cha kahawa asubuhi ili kujiamsha? Hapana, bila shaka sio. Je, ni makosa kutegemea kahawa sana kwamba huwezi kufanya kazi asubuhi mpaka utakapokuwa na kikombe chako cha kahawa? Kulingana na 1 Wakorintho 6:12, jibu linapaswa kuwa ndiyo. Hatupaswi kuwa waraibu kwa chochote. Hatupaswi kujiruhusu kuwa chini / kudhibitiwa / kuwa mtumwa wa chochote. Hakika hii inajumuisha buni. Wakati mtu anatumia kahawa kwa kiasi, kahawa sio dhambi. Wakati mtu anakuwa mraibu na kutegemeana kahawa, hapo ndipo inakuwa suala la kiroho, na dhambi ambayo inahitaji kushindwa.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, uraibu wa buni ni dhambi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries