settings icon
share icon
Swali

Ina maana gani kwamba chuma hunoa chuma?

Jibu


Maneno "chuma hunoaa chuma" hupatikana katika Mithali 27:17: "Chuma hunoa chuma; Ndivyo mtu aunoavyo uso wa rafiki yake." Kuna faida ya pande zote katika kusagwa kwa vyombo viwili vya chuma pamoja; pande zote huwa kali, na kufanya visu vizuri zaidi katika kazi zao za kukata vipande vipande. Vivyo hivyo, Neno la Mungu ni 'upanga wa pande mbili' (Waebrania 4:12), na kwa hili tunapaswa kuimarishana-wakati wa mikutano, ushirika, au ushirikiano wowote.

Methali pia inaonyesha haja ya ushirika na mtu mwingine. Mwanadamu hakuumbwa awe peke yake, kwa maana Bwana Mungu hakusema hivi, hata kabla ya Kuanguka (Mwanzo 2:18)? Basi, itakuaje zaidi baada ya Kuanguka kwa Mwanadamu, tunahitaji kuja pamoja na ndugu na dada zetu katika Kristo kwa msimu wa ushirika na sala. Kwa wazi, hii ilikuwa kitambulisho kwa watakatifu wa kanisa la kwanza (Matendo 2: 42-47) ambao "walijitolea wenyewe" kwa mafundisho, jumuia, ushirika, na maombi-shughuli zote za ushirika ambazo ziliipa fursa za kuimarishana. Matokeo yake ni kwamba "walijazwa na hofu" na walipokutana pamoja; walimsifu Mungu kwa neema waliyopata kwa kila mmoja.

Kuna pointi mbili za kusema juu ya mithali ilyo hapo juu. Kwanza, mkutano wa wawili pamoja kwa jina la Bwana daima umehakikishiwa baraka. Ni njia ya neema ambayo Bwana Mwenyewe aliaahidi-ambapo wawili au zaidi wamekusanyika kwa jina Lake, huko Yeye yupo miongoni mwao (Mathayo 18:20). Pia, tunaona maana sawa katika Malaki kwa wale waliomcha Bwana walineneana wao kwa wao, na Bwana akawasikiliza na kuwasikia (Malaki 3:16). Tunapokutana katika ushirika wa Kikristo, Bwana husikilia kutoka mbinguni na anafurahi. Hakuna neno hata moja linalomletea utukufu litapita.

Manukato ya umoja wa Uungu ni bora zaidi katika uhusiano wa Daudi na Yonathani, mwana wa Sauli. Daudi alipokuwa akifuatwa na Sauli, Yonathani akamtafuta Daudi "kumsaidia kupata nguvu katika Mungu" (1 Samweli 23:16), ambayo inatuongoza kwenye hatua yetu ya pili. Chuma kunoa chuma kingine ni fursa ya kutimiza Sheria ya Kristo. Mtume Paulo anasema kwamba tunapaswa kubebeana na kushiriki mizigo tunayopata kila siku, kuomboleza juu ya dhambi ya kibinafsi, kushauriana jinsi gani ya kutubu, na kufurahi juu ya ushindi huo. Hii ni sawia na "sheria ya kifalme" iliyotajwa katika Yakobo 2: 8, ambapo tunashauriwa kupendana.

Kurudi kwa mlinganisho, kama kisu sio kikali, bado kitaendelea kuwa kisu, ingawa hakiwezekani, haitoshi. Kwa hiyo, hebu tuhimizwe kutumia muda mwingi pamoja, kujengana, kuhimiza, kuomba, kuonyana, kushiriki Neno la Mungu, kuomba juu ya Neno la Mungu na mahitaji ya kanisa letu, ili tuwe na nguvu zaidi katika huduma ambayo Bwana amempa kila mmoja wetu. Mara nyingi, kile kinachoonekana kama ushirika katika kanisa la leo msingi uko katika chakula na furaha, si kwa kuimarishana kwa Neno la Mungu.

Hatimaye, kisu ambacho kimenolewa pia kitaangazia zaidi kwa sababu ubutu wote umekwisha kuharibiwa. Vivyo hivyo, tutaangaza vizuri zaidi kwa Bwana wetu ikiwa tunafanya mambo yaliyotajwa hapo juu, yote ambayo yatatuunganisha kwa umoja. "Tazama, jinsi ilivyo vema, na kupendeza, Ndugu wakae pamoja, kwa umoja" (Zaburi 133: 1). Kwa hiyo, kama mwandishi kwa Waebrania anasema, "Tukaangaliane sisi kwa sisi na kuhimizana katika upendo na kazi nzuri; wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia "(Waebrania 10: 24-25).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ina maana gani kwamba chuma hunoa chuma?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries