settings icon
share icon
Swali

Mafundisho ya Calvin na mafunzo ya Arminian- ni mtazamo upi uko sawa?

Jibu


Mafundisho ya Calvin na mafunzo ya Arminian ni mifumo miwili ya teolojia ambayo inajaribu kuelezea uhusiano kati ya uweza wa Mungu na jukumu la mwanadamu katika mada ya wokovu. Mafundisho ya Calvin yapewa jina la John Calvin (Yohana Calvin) mwanateolojia wa Kifaranza aliyeishi kati ya miaka ya 1509-1564. Na mafunzo ya Arminian yamepewa jina la Jacobus Arminius, mwanateolojia wa Uholanzi aliyeishi kati ya miaka ya 1560-1609.

Mifumo yote inaweza fupishwa kwa alama tano. Mafundisho ya Calvin yanashikilia upotovu wa mwanadamu ile hali mafunzo ya Arminian yanashikilia kuwa wanadamu hawana uwezo wa kuja kwa Mungu kwa uwezo wao wenyewe. Upotovu kiasi wasema kwamba kila sehemu ya mwanadamu imearibiwa na dhambi, lakini si kwa kiwango kuwa hawana uwezo wa kuweka imani kwa Mungu kwa majalio yao

Mafundisho ya Calvin yajumlisha imani kuwa unyakuzi usio na masharti, ile hali mafunzo ya Arminian yaamini kuwa unyakuzi ni wa masharti. Unyakuzi usio na masharti ni mtazamo kuwa Mungu uwachagua watu binafsi kwa wokovu kwa misingi ya mapenzi yake mwenyewe, si kwa misingi ya kitu chochote ndani ya mtu. Unyakuzi wa masharti wasema kwamba Mungu anawachagua watu kwa wokovu kwa misingi ya hekima ya asili ya kuwa ni nani ataamini Kristo kwa wokovu, kwa masharti ikiwa mtu angemchagua Mungu.

Mafunzo ya Calvin yanaona upatanisho wa Mungu na mwanadamu kuwa kikomo, ile hali mafunzo ya Arminian yaona upatanisho usio na kikomo. Huu ndio utatanisho hasa wa hizi hoja tano. Upatanisho wa kikomo ni imani kwamba Yesu alikufa kwa wateule pekee. Upatanisho usio na kikomo ni imani kwamba Yesu aliwafilia watu wote, lakini kifo chake hakifai hadi pale mtu anapompokea kwa imani.

Mafunzo ya Calvin pia yaongeza imani kuwa neema ya Mungu haizuiliki, bali mafunzo ya Arminian yasema kuwa mtu binafsi anaweza zuia neema ya Mungu. Neema isiyozuilika yapinga kwamba wakati Mungu anamwita mtu kwa wokovu, huyo mtu bila kuepa atakuja kwa wokovu. Neema izuilikayo yasema kwamba Mungu anawaita wote kwa wokovu, lakini watu wangi wanapinga na kukataa huu mwito.

Mafunzo ya Calvin yanaamini kuwa uvumilivu wa watakatifu bali mafunzo ya Arminian yashikilia kuwa wokovu wa masharti. Uvumilivu wa watakatifu wamaanisha dhana kuwa mtu ambaye ametuliwa na Mungu atastahimili kwa imani na kamwe hatamkana Kristo au kugeuka mbali naye. Wokovu wa masharti ni mtazamo kuwa muumini katika Kristo anaweza miliki hiari huru, ageuke mbali na Kristo na hapo apoteze wokovu wake.

Kwa hivyo mjadala kati ya Calvin na Arminian nani ako sawa? Ni jambo la kufahisha kukumbuka kwamba utofautitofauti wa mwili wa Kristo, zote ni mchanganyiko wa mafunzo ya Calvin na Arminian. Kuna alama tano za mafunzo ya Calvin na alama tano za mafunzo ya Arminian, na kwa wakati huo huo alama tatu za Calvin na alama mbili za mafunzo ya Arminian. Waumini wengi huafikia kwa mchanganyiko wa hiyo mizimamo miwili. Mwisho, ni mtazamo wetu sisi wote kuwa mifumo yote miwili imekosea kwa kujaribu kuelezea liziloweza elezeka. Wanadamu hawana uwezo wa kuelewa mambo kama haya. Naam, Mungu ako na mamlaka na anajua mambo yote. Naam, mwanadamu wameitwa kufanya maamuzi ya kweli kuweka imani katika Kristo kwa wokovu. Hizi alama mbili zinahitilafiana kwetu lakini kwa mawazo ya Mungu ziko na maana dhabiti.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Mafundisho ya Calvin na mafunzo ya Arminian- ni mtazamo upi uko sawa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries