settings icon
share icon
Swali

Ni kwa nini kuikariri Biblia ni muhimu?

Jibu


Ukariri wa Biblia ni muhimu sana katika maisha ya Kikristo. Kwa kweli, kukariri Maandiko ni mojawapo ya jambo muhimu zaidi kwa ukuaji wa kiroho na ushindi juu ya dhambi. Neno la Mungu ni nguvu kwa sababu ni "Mungu aliyepumua" kutoka kwa akili ya Roho Mtakatifu (2 Timotheo 3: 16-17), na tunapojaza mawazo yetu kwa maneno lake kwa kuriri Maandiko, sisi tunajitengenezea silaha ya nguvu zaidi ya kiroho.

Tunapolikariri Neno la Mungu, vitu kadhaa hutokea. Zaburi 119: 11 inatuambia mtunga-zaburi aliliweka Neno la Mungu ndani ya moyo wake ili asije akamtende dhambi. Sio tu alilisikia na kulisoma Neno, lakini aliliweka ndani na kuliweka katika akili na kumbukumbu kwa matumizi ya baadaye. Neno la Mungu ndio silaha tu ya kweli ya muumini dhidi ya dhambi, na wakati linapowekwa katika akili kupitia kumbukumbu ya Biblia, ni ushawishi mkubwa kwa uungu na uhai wa haki. Waebrania 4:12 inatuambia Neno la Mungu ni "hai na lina nguvu," maana yake lina uwezo usio wa kawaida wa kututengeneza kadri na mfano wa Kristo wakati tunapolitafakari, na hakuna njia bora ya kutafakari juu ya Neno mbali na kuliweka katika mawazo yetu na kumbukumbu zetu.

Waefeso 6: 13-17 inaelezea silaha za muumini katika vita kwa nafsi zetu na maisha ya kiroho. Mambo yote ya silaha yanalinda isipokuwa moja. Silaha tu ya kukera ni "upanga wa Roho, ambayo ni neno la Mungu" (mstari wa 17). Kama vile Yesu alivyotumia Neno la Mungu ili kuzuia mashambulizi ya Shetani (Mathayo 4: 1-11), basi ni lazima tupate kutumia silaha sawia. Lakini mara chache Shetani anatupa wakati wa kuchukua Biblia na kupata vifungu sahihi wakati tunakabiliwa na uongo wake na udanganyifu. Ukariri wa Biblia unahakikisha kuwa tutaweza kuwa na ukweli na kanuni zinazofaa katika akili na kuwaweza kuzikumbuka mara moja ili kujibu kwa uangalifu anayetaka kutuangamiza (1 Petro 5: 8). Warumi 12: 1-2 inatuhimiza "kugeuzwa" mawazo yetu ili tuweei tena kuathiriwa na mawazo ambayo yanatufananisha na ulimwengu huu. Njia pekee ya kugeuza mawazo yetu ni kujijaza na Maandiko.

Kukariri Maandiko ni pendeleo na wajibu wa kila Mkristo. Kuna mifumo mizuri ya kukariri ya Maandiko inapatikana. Hata bila njia maalum iliyochapishwa, mtu yeyote anaweza kuanza na mistari muhimu ya imani ya Kikristo-kama Yohana 3:16 na Waefeso 2: 8-9-na kuendelea kujenga mstari juu ya mstari. La muhimu ni kuendelea kuchunguza ile ambayo tayari wameikariri kabla ya kuongezea ingine mpya. Njia yoyote iliyochaguliwa, faida za kukariri Biblia ni ushindi juu ya dhambi, imani imara, na furaha katika maisha ya Kikristo.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni kwa nini kuikariri Biblia ni muhimu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries