settings icon
share icon
Swali

Biblia inafafanua vipi ufanisi?

Jibu


Wakati Mfalme Daudi alipokuwa karibu kufa, alimpa mwanawe, Sulemani shauri lifuatalo: "Uyashike mausia ya Bwana Mungu wako uende katika njia zake uzishike sharia zake na amri zake n hukumu zake na shuhuda zake sawasawa na ilivyoandikwa katika torati ya Musa upate kufanikiwa katika kila ufanyalo na kila utazamako."(1 Wafalme 2: 3). Daudi hakumwambia mwanawe kujenga ufalme wake na majeshi makubwa, au kukusanya mali kutoka nchi nyingine, wala kuwashinda adui zake katika vita. Badala yake, kufanikiwa ililenga kumtii na kufuata Mungu.Sulemani alipokuwa mfalme, hakuonelea kwa utajiri na nguvu kutoka kwa Bwana, badala yake hekima na ufahamu ili kuwaongoza taifa la Mungu. Mungu alipendezwa na azima hili na alimjalia, akampa Sulemani moyo wa hekima na ufahamu, zaidi kuliko mtu yeyote kabla. Pia alimpa Sulemani mambo ambayo hakuomba-utajiri na heshima kati ya wanadamu (1 Wafalme 3: 1-14). Sulemani alitii shauri la baba yake,na kwa utawala wake wote, na kunakili katika Mithali: "Mwanangu, usisahau sheria yangu, bali moyo wako uzishike amri zangu,maana zitakuongezea wingi wa siku na miaka ya uzima na amani.Rehema na kweli zisifarakane nawe zifunge shingoni mwako,ziandike juu ya kibao cha moyo wako.Ndivyo utakavyopata kibali na akili nzuri mbele za Mungu na mbele ya mwanadamu."(Mithali 3: 1-4).

Yesu alifundisha haya katika Agano Jipya wakati alisema amri kuu zaidi: "nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote na kwa akili zako zote na kwa nguvu zako zote. Ya pili ndiyo hii: 'Mpende jirani yako kama nafsi yako.' Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi. "(Marko 12: 30-31) Kumpenda Mungu ina maana kumtii na kufuata amri zake (Yohana 14:15, 23-24). Mwanzo katika mchakato huu ni kukubali zawadi ya bure ya uzima wa milele uliotolewa na Yesu Kristo (Yohana 3:16) Huu ndio mwanzo wa mafanikio ya kweli ya kibiblia. Mabadiliko huanza zawadi inapopokezwa .Hatua hii hukamilika, si kwa mapenzi ya kibinadamu, bali kwa Roho Mtakatifu wa Mungu (Yohana 1:12). -13) Je, haya hufanyika vipi na hatima yake ni ipi? Mwanzo ni kupitia kumtii na kumtegemea Bwana.Tunapomtii Yeye, hutubadilisha, hutupa asili mpya kabisa (1 Wakorintho 5:17). Tunapokuwa ktika shida na wakati mgumu, kiBiblia"majaribu," tunaweza kuvumilia kwa amani na mwelekeo mkubwa, na tunaanza kufahamu kuwa Mungu hutumia majaribu hayo ili kukamilisha utu wetu wa ndani (Yohana 16:33; Yakobo 1) : 2) Hakika, taabu katika maisha haitufanyi sisi kushindwa, bali kuimarika katika taabu na neema ya Mungu na hekima. Kwa kumtii Mungu, tunapata uhuru zinazotokana na laana za chuki, udanganyifu, uovu, kuchanganyikiwa, matatizo duni, hasira, uchungu, kukosa kusamehe, ubinafsi na kadhalika.

Zaidi ya hayo, wafuasi wa Kristo (Wakristo) humiliki na kudhihirisha mazao ya Roho wa Mungu anayeishi mioyoni mwao-upendo, furaha, amani, uvumilivu, wema, fadhili, upole, uaminifu, na udhibiti binafsi (Wagalatia 5:22) -23). Kwa ujuzi wetu tunajua nini cha kufanya na wapi pa kubadilisha (Mithali 3: 5-6), kiwango kikubwa cha hekima (Yakobo 1: 5), na amani inayozidi ufahamu (Wafilipi 4: 7). Tunapozidi kukua na kukomaa katika Kristo, tunaanza kufikiria wengine sio tu sisi wenyewe. Furaha yetu kubwa inakuwa yale ambayo tunaweza kuwafanyia na kuwapa wengine, na vile tunavyoweza kuwasaidia kukua na kufanikiwa kiroho. Hii ni mafanikio ya kweli, kwa sababu mtu anaweza kuwa na nguvu zote, pesa, umaarufu na sifa ambazo dunia inampa, ilhali kama nafsi yake ni pungufu na yenye machungu, mafanikio ya kidunia hakika bure. "Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwwengu wote na kupata hasara ya nafsi yake?Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake? "(Mathayo 16:26).

Mwishowe katika mafanikio ya kibiblia. Kutoa zawadi nadhifu za kimwili kwa wanawe ikiwemo (chakula, nguo, nyumba, nk), wakati wa kubadilisha maisha yetu ya ndani ni lengo la Mungu kwetu, na hupenda kufanya hivyo (Mathayo 6: 25-33). Ingawa, wengi wetu, mara nyingi huangazia zawadi Zaidi kuliko Anayetoa. Hapo ndipo tunaposhughulika na kuridhika na raha zetuna kukatiza azimio ya kubadilisha Roho ndani yetu, kwa kuangazia mabaya zaidi. Hiyo inaweza kuwa lengo la Bwana kukatiza kipawa chake cha kutupa manufaa-maanake hatuzami kwa zawadi na kutupa mbali naye.

Tazama pande ya pili. Kwa upande wa kulia kuna uridhisho wa kweli, uwezo wa kuangazia shida za maisha pasipo kushindwa nayo, amani inayotuwezesha kushinda hali zote, hekima ili kufahamu ya kufanya, ufahamu na mwelekeo wa maisha, mapenzi kwa wengine , kujikubali, raha bila kizuizi, na mwisho maisha, daima na Mungu atoaye zawadi hizi zote bila malipo. Upande mwingine kuna utajiri na nguvu na "kufanikiwa"inayotolewa na dunia, bila kujumuisha yaliyo upande mwingine. Ungependa kuchakua gani? Biblia inanakiri, "Kwa kuwa hazina yako ilipo,ndipo utakapokuwapo na moyo wako" (Mathayo 6:21). Yaliyo upande wa kulia ndiyo maelezo ya kibiblia ya ufanisi.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Biblia inafafanua vipi ufanisi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries