settings icon
share icon
Swali

Biblia imenakiri nini juu ya ulazi?

Jibu


Ulazi ni kufanyamaneno Fulani yasiyo ya kweli ili kuharibia mtu sifa. Ulazi iko tofauti na kiburi kiwango kadiri kuwa kiburi ni uharibifu wa tabia ulionakiriwa;ilhali udanganyifu ni wa kusemwa tu.Katika Agano la kale na Jipya,{Methali 10:18,1Petro 2:1} mengi yameandikwa kuhusu ulazi katika Biblia. Udanganyifu ni mojawapo ya makosa ambayo yameingizwa katika nakala ya Amri kumi na Mungu.Amri ya tisa inasema, "Usimshuhudie jirani yako uongo" (Kutoka 20:16). Kwa sababu ya uongo unaoenezwa kutoa ushahidi wa uongo umejumuishwa pamoja na ulazi. Udanganyifu ni kusema uongo kumhusu mwingine kwa lengo la kumfanya aonekane kwa ubaya.

Mungu huchukizwa na uongo (Methali 6: 16-19; 12:22) kwa maana ulazi ni udanganyifu mkubwa. Kwa maaana Mungu ni ukweli (Yohana 14: 6; 1 Yohana 5: 6), chochote kisicho kweli ni kinyume na asili Yake na kwa hiyo ni dharau kwake. Kwa jumla ulazi na uvumi ni mbaya, na Bibilia huhukumu vyote (Mambo ya Walawi 19:16; Mithali 16:27; 2 Wakorintho 12:20). Ulazi hufanya siri zake na kuzitangaza popote wanapofanya madhara Zaidi,hali kadhalika masengenyo hukusanya siri za wengine.

Agano Jipya imefafanua sehemu ya hali yetu ya zamani ya dhambi. Udanganyifu hauna nafasi maishani mwetu tunapokuwa wapya katika Kristo (2 Wakorintho 5:17). Wakolosai 3: 7-8 inasema, "Katika hayo ninyi nanyi mlitembea zamani,mlipoishi katika hayo.Lakini sasa yawekeni mbali nanyi haya haya yote,hasira na ghadhabu,na uovu na matukano,na matusi vinywani mwenu."Maneno yetu yanapaswa kutolewa kwa utukufu wa Mungu, kama vile miili yetu (Warumi 12: 1-2; Waefeso 4:29). Wanaomjua Mungu wanapaswa kuepukana na ulazi: "Kwa huo twamhimidi Mungu Baba yetu,ne kwa huo twawalaani wanadamu waliofanywa kwa mfano wa Mungu.Katika kinywa kile kile hutoka Baraka na laana.Ndugu zangu,haifai mambo hayo kuwa hivyo."(Yakobo 3: 9-10). Ulazi ni mazoea yanayopaswa kutupiliwa mbali kama tunaaa kumfuata Yesu. (tazama Waroma 6: 11-14).

Katika Warumi 1: 28-32, Udanganyifu ni ni moja wapo katika orodha ambayo Paulo anatajaka kuwa zile wsifa za akili zilizozorota. (mstari wa 30). Tunapotukana wengine, tunaonelea kuacha njia ambayo Mungu alituchagulia. Hawezi shiriki nasi katika juhudi zetu za kuharibia wengine kwa vinywa vyetu. Ulazi hutokea katika mioyo, tunapojaribiwa kusema uongo kuhussu wengine, tunafaa mwanzo kujichunguza ili kugundua mizizi mibaya inayootesha tamaa hizo. Yesu akasema, "Bali vitokavyo kinywani vyatoka moyoni;navyo ndivyo vimtiavyo mtu unajisi.Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya,uuaji,uzinzi,uasherati wivi,ushuhuda wa uongo,na matukano. "(Mathayo 15: 18-19). Mungu anataka tujue kuwa kumdanganya mtu ni ishara kuonyesha mioyo yetu haiku sawa Naye. Tamaa ya ulazi inaweza kuota kutoka kwa machungu (Waebrania 12:15), kutoka kwa maumivu yasiyopona (1 Petro 3: 14-16), kutoka kukosa kusamehe (2 Wakorintho 2: 10-11; Waefeso 4:32), kutokana na wivu (Wagalatia 5:20; 2 Wakorintho 12:20), au kutoka kwa dhambi nyingine za moyo.

Suluhu la Mungu kwa ulazi ni kupendana (Yohana 13:34). Hatutawatukana wale tunaowaenzi (1 Wakorintho 13: 4-7). Upendo unataka mazuri kwa wengine, na hiyo inamaanisha kulinda sifa zao kama tufanyavyo zetu (Mathayo 7:12). "Pendo halimfanyii jirani neno baya;basi pendo ndilo utimiliu wa sharia."(Warumi 13:10). Tunapozingatia kumtii Bwana kwa kupenda kama Yeye anatupenda, udanganyifu hautatujaribu.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Biblia imenakiri nini juu ya ulazi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries