settings icon
share icon
Swali

Je! Ni kiwango gani cha Biblia zilizopitishwa kwa tamaduni simulizi?

Jibu


Kwanza, tunapaswa kutofautisha kati ya "mila" simulizi na "usambazaji" simulizi. Neno mila linamaanisha tamaduni zilizoshikiliwa kwa muda mrefu au utendaji ambao hasa haujaunganishwa na ukweli wowote au Ushahidi. Uhamisho ni njia ya kufikisha ujumbe. Yalimo katika Biblia, kwa kiwango fulani, yelinenwa kwa njia ya moja kwa moja na sio kwa mjibu wa "tamaduni." Badala yake, chenye kilipitishwa ilikuwa elezo la moja kwa moja la ukweli maalum kuhusu watu Fulani, mahali, na nyakati. Mara nyingi, andiko la biblia liliwekwa katika maandishi pindi matukio hayo yaliyoelezewa yalitokea.

Mfano mzuri wa hay ani kitabu cha Luka, ambacho kwa kina kinaelezea mwanzo wake katika mlanong wa 1. Luka anayaweka matokeo ya udadisi wake katika lugha andishi, huku akitumia mazoea ya kushuhudia kwake kwa macho. Wanahistoria wamekipata kitabu cha Luka kuwa habari kamili ya kwanza. Sehemu ya Injili hii inaweza chukuliwa kuwa "tamaduni sungumzi" kabla ya uandishi wake, ingawa wingi wa mambo yalimo yanapatikana katika Injili ya mapema ya Marko.

Marko inaaminika kuandikwa karibu mwaka wa AD 55 mbali sana na matukio yaliyoelezewa kuwa kitengo cha "tamaduni sungumzi." Watu wengi husaau kuwa vitabu vya Injili sivyo uandishi wa mapema wa Kikristo au chanzo cha kwanza cha yaliyomo. Nyaraka za Paulo, kwa mfano, takribani zote ziliandikwa kabla ya vitabu vya Injili kuandikwa. Katika 1 Wakorintho 15 Paulo anaelezea muhtasari wa kimsingi wa imani ya Kikristo. Anasema kuwa maneno hayo ni yale aliyoyafunzwa wakati wa kuokolewa kwake, ambako kulitokea miaka michache baaday ya kufufuka kwa Yesu.

Hiyo pia inaweza kuwa vile vile na Agano la Kale. Mambo yalikuwa yanaandikwa kimakusudi ili kunakili ujumbe au matukio yaliyotokea. Vitabu vya Agano la Kale sio mkusanyiko wa hekaya za kale, zilizosoma katika lugha ya, "hapo zamani za kale" na hazikutolewa katika ukweli wa historia.

Uandishi huu wa moja kwa moja wa ujumbe na matukio unakinzana na uandishi wa imani zingine, kama vile Uislamu. Kurani ilibebwa kwa njia yam domo katika kipindi cha miaka arobaini ya huduma ya Muhammad. Sehemu chache za Kurani ziliandikwa katika vipande na vigae na bali sio kwa mtindo wa mswada. Ni baada ya Muhammad kufa ndipo maneno yake yalipowekwa katika mkusanyiko, ambao wenyewe ulihaririwa na kurekebishwa hadi nakala zenye kushindana zilipoharibiwa na khalifa Uthman. Zaidi ya hayo chanzo kikuu cha maarifa ya Kiislamu ni hadithi, ambayo kwa kweli ni "mila ya mdomo," kwamba uungwaji wake uu katika uaminifu katika uadilifu wa kiroho vyanzo vyake. Mchakato wa Uislamu wa kuamua uaminifu huu unajulikana kama isnad.

Mfano mwingine wa tafauti ya mila ya mdono ya Kikristo ilitoka kwa Yesu Mwenyewe. Mafarisayo walikuwa wametumia mila ya mdomo kwa njia ya kuitafsiri Sheria ya Musa. Ingawa Yesu aliisungumzia juu ya Maandiko na taadhima, alikemea utegemeo wa mila za mdomo kwa kuwa hali yake ilikuwa inaonesha nia za wanamila, badala ya mapenzi ya Mungu (ona Marko 7:6-9).

Maambukizi yam domo kwa yenyewe, sio njia isiyoaminika kabisa, haswa kwa ujumbe rahisi. Katika wakati ambapo watu wengi hawakusoma au kuandika, usambazaji wa mdomo ulikuwa wa kawaida na kudumisha maneno halisi ya asili ilizingatiwa kuwa muhimu. Manufaa halisi ya maandishi kwa ujumbe wa mdomo ni kwamba uandishi hihifadhi picha za ujumbe kutoka kwa wakati yalitokea. Mtu anaweza kulinganisha tafauti kati ya madai tofauti bila malengo, na ujumbe mmoja unaweza kusomwa ten ana tena kwa usahihi sawia mara kwa mara. Kulingana na Ushahidi wa ndani na nje, maneno ya biblia yalihifadhiwa kwa njia ya maandishi kama kumbukumbu za ukweli, na sio mila za mdomo.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Ni kiwango gani cha Biblia zilizopitishwa kwa tamaduni simulizi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries