settings icon
share icon
Swali

Biblia inasema nini juu ya tamaa?

Jibu


Tamaa ni hamu ubinafsi ya kuwa na kitu zaidi, mara nyingi fedha au mamlaka. Kuna maonyo mengi katika Biblia juu ya kuwa uchoyo na kutamani utajiri. Yesu alionya, "Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo."(Luka 12:15). "Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba… Hamwezi kumtumikia Mungu na mali." (Mathayo 6:19, 24b). Je! Yesu alijishughulisha na upatikanaji wa pesa? Hapana. Badala yake, Alikuwa maskini kwa ajili yetu (2 Wakorintho 8: 9) na "hakuwa na mahali ya kuweka kichwa chake" (Mathayo 8:20). Yesu hakujishughulisha na mamlaka. Badala yake, aliwaagiza, "Yeyote anayetaka kuwa mkuu kati yenu atakuwa mtumishi wenu, na yeyote anayetaka kuwa wa kwanza lazima awe mtumwa wa wote, maana hata Mwana wa Mtu hakuja kutumikiwa, bali kutumikia, na kutoa maisha yake kama fidia kwa wengi "(Marko 10: 43-45).

Tamaa na hamu ya utajiri ni mitego ambayo huleta uharibifu. "Upendo wa fedha ni mzizi wa aina zote za uovu," na Wakristo wanaonywa, "Msiwe na imani yako katika mali" (tazama 1 Timotheo 6: 9-10, 17-18). Tamaa, au kuwa na hamu nyingi zaidi, ni ibada ya sanamu. Waefeso 5: 5 inasema, "Maana neno hili mnalijua hakika, ya kwamba hakuna mwasherati wala mchafu wala mwenye tamaa, ndiye mwabudu sanamu, aliye na urithi katika ufalme wa Kristo na Mungu." Kanuni ya kukumbuka imeandikwa katika Waebrania 13: 5: "Msiwe na tabia ya kupenda fedha; mwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa."

Ni upendo wa fedha, na si pesa yenyewe, hiyo ndiyo tatizo. Upendo wa pesa ni dhambi kwa sababu inatuzuia tusimwabudu Mungu. Yesu alisema ilikuwa vigumu sana kwa matajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu. Wakati mtawala huyo mdogo na tajiri alipomwuliza Yesu atakayotakiwa kufanya ili kurithi uzima wa milele, Yesu alimwambia auze mali yake yote na kuwapa maskini fedha. "Yule kijana alipoposikia hayo, akaenda zake kwa huzuni, kwa kuwa alikuwa na utajiri mkubwa" (ona Mathayo 19: 16-22). Kwa kumwambia apeane pesa zake, Yesu alionyesha tatizo kuu la kijana huyo: uchoyo au upendo wa pesa. Mtu huyo hakuweza kumfuata Kristo kwa sababu alikuwa akifuata fedha. Upendo wake wa ulimwengu huu uliingilia upendo wake kwa Mungu.

Tamaa hukataa kutosheka. Mara nyingi, zaidi tunayopata, tunazidi kuyataka. Mali haitatulinda katika maisha haya au ya milele. Mfano wa Yesu wa tajiri mpumbavu katika Luka 12: 13-21 unaonyesha jambo hili vizuri. Tena, fedha au utajiri sio tatizo. Tatizo ni mtazamo wetu juu yake. Tunapoweka imani yetu katika utajiri au tunajitosa katika hamu ya kutaka zaidi, tunashindwa kumpa Mungu utukufu na ibada Yeye anayostahili. Tunapaswa kumtumikia Mungu, si kupoteza muda wetu kujaribu kuwa tajiri (Mithali 23: 4). Tamaa yetu ya moyo inapaswa kuwa kuhifadhi mali mbinguni na si wasiwasi juu ya nini tutachokula au kunywa au kuvaa. "Lakini tafuta kwanza ufalme [wa Mungu] na uadilifu wake, na haya yote utapewa pia" (tazama Mathayo 6: 25-34).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Biblia inasema nini juu ya tamaa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries