Biblia inasema nini juu ya kushukuru / shukrani?


Swali: "Biblia inasema nini juu ya kushukuru / shukrani?"

Jibu:
Shukrani ni mandhari maarufu ya Biblia. Wathesalonike wa kwanza 5: 16-18 inasema, "Furahini siku zote; ombeni bila kukoma;shukuruni kwa kila jambo;maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.'' Toa shukrani katika hali zote. Shukrani inapaswa kuwa njia ya uzima kwa ajili yetu, kwa kawaida inatiririka kutoka mioyo yetu na vinywa

Kuangalia Maandiko kwa undani zaidi, tunaelewa kwa nini tunapaswa kushukuru na jinsi ya kuwa na shukrani katika hali tofauti.

Zaburi 136: 1 inasema, "Mshukuruni Bwana, kwa maana fadhili zake ni za milele.'' Hapa tuna sababu mbili za kuwa na shukurani: wema wa Mungu daima na upendo wake wa kudumu. Tunapotambua hali ya uchafu wetu na kuelewa kuwa, mbali na Mungu, kuna kifo tu (Yohana 10:10, Warumi 7: 5), jibu la asili ni kushukuru kwa maisha anayopeana.

Zaburi 30 inamtukuza Mungu kwa ajili ya ukombozi Wake. Daudi anaandika, "Ee Bwana, nitakutukusa,kwa maana umeniinua,Wala hukuwafurahisha adui zangu juu yangu. Ee Bwana Mungu wangu, nalikulilia ukaniponya. Umeniinua nafsi yangu, Ee Bwana, kutoka kuzimu umenihuisha na kunitoa miongoni mwao washukao shimoni . . . .uligeuza matanga yangu kuwa machezo;ulinivua gunia ukanivika furaha.Ili utukufu wangu ukusifu,wala usinyamaze.Ee Bwana,Mungu wangu,Nitakushukuru milele.''(Zaburi 30: 1-12). Hapa Daudi anamshukuru Mungu kufuata hali ya dhahiri ngumu. Zaburi hii ya shukrani haimsifu Mungu wakati huu bali anakumbuka uaminifu wa Mungu uliopita. Ni taarifa ya tabia ya Mungu, ambayo ni ya kushangaza sana kwamba sifa ni jibu pekee inayofaa.

Pia tuna mifano ya kuwa na shukurani katikati ya hali ngumu. Zaburi 28, kwa mfano, inaonyesha dhiki ya Daudi. Ni kilio kwa Mungu kwa rehema, ulinzi, na haki. Baada ya Daudi kumlilia Mungu, anaandika hivi, "Na ahimidiwe Bwana.Maana amesikia sauti ya dua yangu; Bwana ni nguvu zangu na ngao yangu.moyo wangu umemtumainia,name nimesaidiwa; Basi,moyo wangu unashangilia,na kwa wimbo wangu nitamshukuru."(Zaburi 28: 6-7). Katikati ya shida, Daudi anakumbuka ambaye Mungu ni nani, na kwa sababu ya kumjua na kumwamini Mungu, anamshukuru. Ayubu alikuwa na mtazamo sawa wa sifa, hata katika uso wa kifo: "Bwana alitoa na Bwana ametwaa; Jina la Bwana na libarikiwe "(Ayubu 1:21).

Kuna mifano ya kushukuru kwa waumini katika Agano Jipya pia. Paulo aliteswa sana, lakini aliandika, "Ila Mungu ashukuriwe,anayetushangiliza daima katika Kriston kuidhihirisha harufu ya kumjua yeye , " (2 Wakorintho 2:14). Mwandishi wa Waebrania anasema, "Basi , kwa kuwa tunapokea ufalme usioweza kutetemeshwa,na mwe na neema,ambayo kwa hiyo tumtolee Mungu ibada ya kumpendeza pamoja na unyenyekevu na kicho;" (Waebrania 12:28). Petro anatoa sababu ya kushukuru kwa "huzuni na kila aina ya majaribu," akisema kwamba, kwa njia ya shida, imani yetu "inaweza kuthibitishwa kuwa ya kweli na inaweza kusababisha sifa, utukufu na heshima wakati Yesu Kristo akifunuliwa" (1 Petro 1): 6-7).

Watu wa Mungu ni watu wenye kushukuru, kwa sababu wanajua kiasi gani wamepewa. Moja ya sifa za siku za mwisho ni ukosefu wa shukrani, kulingana na 2 Timotheo 3: 2. Watu waovu "hawatashukuru."

Tunapaswa kushukuru kwa sababu Mungu anastahili shukrani zetu. Ni haki tu kumtukuza "kila zawadi nzuri na kamilifu" Yeye anatoa (Yakobo 1:17). Tunaposhukuru, lengo letu linaondoa tamaa za ubinafsi na mbali na maumivu ya hali ya sasa. Kueleza shukrani hutusaidia kukumbuka kwamba Mungu ana udhibiti. Shukrani, basi, sio sahihi tu; kwa kweli ni afya na manufaa kwetu. Inatukumbusha picha kubwa, kwamba sisi ni wa Mungu, na kwamba tumebarikiwa kwa kila baraka za kiroho (Waefeso 1: 3). Kweli, tuna maisha mengi (Yohana 10:10), na kushukuru ni sawa.

English


Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Biblia inasema nini juu ya kushukuru / shukrani?