settings icon
share icon
Swali

Biblia inasemaje kuhusu rushwa / kutoa au kupokea rushwa?

Jibu


Rushwa ni pesa, neema, au mapendeleo mengine iliyotolewa kwa kushawishi dhidi ya kile ni kweli, na halali, au cha haki. Biblia ii wazi kwamba kutoa au kupokea rushwa ni mabaya.

Sheria ya Mungu, iliyotolewa kwa Musa kwa ajili ya watu wa Israeli, iliizuia kuchukua rushwa, "kwani hiyo rushwa huwapofusha macho hao waonao, na kuyapotoa maneno ya wenye haki" (Kutoka 23: 8). Sharia hiyo hiyo inarudiwa katika Kumbukumbu la Torati 16:19: "Usipotoe maamuzi; wala usipendelee uso wa mtu; wala usitwae rushwa; kwa kuwa rushwa hupofusha macho ya wenye akili, na kugeuza daawa ya wenye haki." Madhara mabaya ya kuchukua rushwa ni wazi yaliyotajwa katika vifungu hivi viwili. Hongo hupotoza haki. Ni ushawishi wa kupofusha juu ya hekima na ufahamu. Inaighubika kweli na kuipotosha au kubadilisha maneno ya wale ambao ni wa haki machoni pa Mungu.

Sheria iliendelea zaidi katika kesi ya rushwa inayohusisha mauaji ya mtu asiye na hatia. hakimu ambaye anachukua rushwa ili ahukumu kifo mtu asiye na hatia alikuwa na hatia kama mwuaji aliyelipwa-alipaswa kuawa "alaaniwe" (Kumbukumbu la Torati 27:25). Kulikuwa na matukio ambapo sheria hii dhidi ya rushwa ilikiukwa, kwa athari mbaya. Wanaume wawili walioshuhudia dhidi ya Naboti (1 Wafalme 21: 4-16) na wale walioshuhudia Stefano (Matendo 6: 8-14) walikuwa wamepewa rushwa; katika matukio hayo mawili, mtu asiye na hatia aliuawa. Wakati viongozi wa juu wanatoa na kupokea rushwa, husababisha uovu katika jamii. "Mfalme huithibitisha nchi kwa hukumu; Bali yeye apokeaye rushwa huipindua" (Mithali 29: 4). Rushwa ni mojawapo ya tabia ya jamii amboyo imeoza.

Isaya alitabiri juu ya uovu wa Israeli wakati waligeuka kutoka kwa Mungu mmoja wa kweli na sheria zake. Isaya aliifananisha mji wa Yerusalemu na kahaba asiyeamini; jiji mara moja lilikua limejaa haki, lakini ilikuwa ni mahali pa uasi, mauaji, na wizi. Viongozi wake walikuwa wale waliopenda rushwa na kukimbilia fedha walizowaletewa (Isaya 1: 2-23). Waisraeli hawakufaa kufuata njia za uovu bali walipaswa kumwiga Mungu katika mwenendo wao: "Kwa maana Bwana, Mungu wenu, yeye ndiye Mungu wa miungu, na Bwana wa mabwana, Mungu mkuu, mwenye kuogofya, asiyependelea nyuso za watu, wala hakubali rushwa" (Kumbukumbu la Torati 10:17).

Mfano mbaya zaidi wa rushwa katika Biblia ni vipande thelathini vya fedha ambazo Yuda alipokea kumsaliti Bwana Yesu. Matokeo ya moja kwa moja ya udanganyifu wa Yuda ni kwamba Yesu alikamatwa na kusulubiwa. Hatimaye, hata Yuda alitambua kuwa kukubali rushwa ilikuwa mbaya. Lakini alipojaribu kurejesha fedha kwa makuhani wakuu na wazee, walikataa, wakiita "pesa ya damu" (Mathayo 27: 3-9).

Delila alilipwa ili kumnasa Samsoni (Waamuzi 16: 5). Wana wa Samweli hawakuheshimu ofisi yao kwa kuchukua rushwa (1 Samweli 8: 3). Hamani mwenye uovu alimshtaki Mfalme Ahasuero ili kujaribu kuwaangamiza Wayahudi katika Uajemi (Esta 3: 9). Feliki akamwacha Paulo gerezani, akiwa na matumaini ya kupata rushwa kutoka kwa Paulo (Matendo 24:26). Na askari walidai kwa kulinda kaburi la Yesu walipwa rushwa na makuhani wakuu na wazee kueneza uongo juu ya kutoweka kwa mwili wa Yesu (Mathayo 28: 12-15). Katika kila kesi, wale waliopokea rushwa hawakujali chochote cha ukweli au haki.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Biblia inasemaje kuhusu rushwa / kutoa au kupokea rushwa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries