settings icon
share icon
Swali

Biblia inasema nini juu ya aibu na majuto?

Jibu


Kila mtu hupata kiwango maalum cha aibu na huzuni kwa sababu ya dhambi zilizotendwa kitambo. Kuna mengi yaliyonakiliwa katika Bibilia juu ya aibu na majuto, na mifano kadhaa ya watu katika Biblia waliopitia hali hizi mbaya.

Unaweza tafakari kiasi cha aibu na majuto Adamu na Hawa waliishi nayo baada ya dhambi yao? Waliharibu uumbaji kamilifu uliotengezwa na Mungu. Adamu na Hawa walikuwa katika dunia kamilifu, wakiwa na akili na miili kamilifu, na walikuwa na ushirika wa karibu kabisa na Mungu. Walipoamua kuasi dhidi ya Mungu, viumbe vyote vilivyoumbwa na Mungu viliathirika kwa mujibu wa dhambi, ikiwemo ugonjwa, uozo, kifo, na kutengwa na Mungu daima. baadaye kila mwanadamu alizaliwa kwa asili na hali ya dhambi-hali ya kiasili ya dhambi. Kwa shukurani, Mungu ni Mtawala mkuu mwenye nguvu, hata hivyo alikuwa na mpangilio wa kuukomboa ulimwengu Wake kupitia kwa njia ya Mwanawe, Yesu Kristo, na kuwapa wanadamu uhuru wa kuamua kati ya wokovu na uzima wa milele pamoja Naye. Ila Adamu na Hawa walilazimika kuishi maisha yao ulimwenguni wakiwa majuto sana kwa kuasi na kupoteza haki na baraka ambazo zingefuata. Tunatambua kuwa walikuwa na aibu kwa kuwa uchi (Mwanzo 3:10). Lazima waliishi maisha yao yote yalio salia kwa majuto-hatimaye, walikumbuka paradiso

Mtume Petro ni mfano mwingine wa kibiblia wa aibu na majuto. Yohana 13: 37-38 inasimulia usiku ule Kristo alisalitiwa. Punde tu baada ya chakula cha Pasaka, Petro anamwambia Yesu kwamba angeweka maisha yake atarini kwa ajili ya Bwana wake. Yesu anamjibu kuwa ifikapo usiku ule Petro hata atamkataa mara tatu kuwa hamjui Bwana. Kisha baadaye usiku huo, Petro kwa sababu ya kuogopa kuuwawa alikataa kuwa anamjua Yesu (Yohana 18: 15-27; Mathayo 26: 31-35, 69-75). Petro Baada ya kumkataa Yesu, "alitoka nje na kuomboleza kwa uchungu" (Luka 22:62). Baadaye, Petro akarejeshwa na akakua katika imani yake, akawa mmoja miongoni mwa wazee waanzilishi wa kanisa la kwanza. Petro hakika alifanya "kuwaimarisha mandugu zake" baada ya kusamehewa, kama vile tu Yesu alivyotabiri (Luka 22:32). Ingawa Petro anaweza kuwa aliishi kuwa na aibu sana na majuto kwa vile alimkataa Yesu adharani, ufahamu wake kuhusu utu na matendo ya Kristo ulizidi hisia zake za kuwa aliasi. Alifahamu kwamba alisamehewa kwa neema ya Mungu, na akazidi majuto yake binafsi na kulisha kondoo za Yesu (Yohana 21:17).

Biblia inatufunza kuwa, tunapokiri dhambi zetu na kuwa na imani katika dhabihu na ufufuo wa Kristo, tunakuwa wana wa Mungu (Yohana 1:12). Tunatakaswa kutoka kwa uovu wetu wote (Wakolosai 1: 15-22), na wokovu wetu umehakikishwa daima (Yohana 10: 27-30; Waebrania 7: 24-25). Tunapozidi kukua kiroho kwa kutumia wakati wetu pamoja na Mungu kila siku katika maombi na kusoma maandiko yake, tunajipata tukimpenda na kumtegemea hata zaidi. Tunaamini kwamba Mungu ametutenga na dhambi zetu kutoka kwetu kama vile upande wa mashariki ulivyo kutoka kwa upande wa magharibi (Zaburi 103: 12). Ndiyo, tunajuta makosa yetu ya zamani, ila sio lengo letu. Tunamtazama Yesu, Mwandishi na Mwenye kuthibiti imani yetu (Waebrania 12: 2). Paulo aliiweka hivi: "Ndugu sijidhanii nasfsi yangu kwamba nimekwisha kushika;ila natenda neno moja tu;nikiyachuchumilia yaliyo mbele;nakaza mwendo,niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu." (Wafilipi 3: 13-14). Aibu na majuto ni sehemu ya yale yaliyo nyuma yetu. Lazima tujifunze kusahau.

Warumi 8: 1 ni faraja kubwa kwa mwamini yeyote anayepambana na hisia za aibu na huzuni zilizobaki: "Sasa hakuna hukumu kwa wale walio katika Kristo Yesu." Sisi ni wenye dhambi, lakini tuna haki. Tuko na zamani yenye aibu, lakini tuko na wakati ujao bora. Tulikuwa tukienda kwa upumbavu na uasi, lakini sasa tunatembea katika maisha mapya (Tito 3: 3-7; Warumi 6: 4). Mungu amekwisha zisaamehe dhambi hizo tunahisi aibu na huzuni kwazo. Tunaweza kuendelea. "Nimesulubiwa pamoja na Kristo;lakini ni hai;wala si mimi tena bali Kristo yu hai ndani yangu;na uhai nilionao sasa katika mwili,ninao katika Imani ya Mwana wa Mungu,ambaye alinipenda,akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu." (Wagalatia 2:20).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Biblia inasema nini juu ya aibu na majuto?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries