settings icon
share icon
Swali

Je! Ni nani aliigawanya Biblia katika milango na aya? Ni kwa nini na ni linii hili lilifanyika?

Jibu


Wakati vitabu vya Biblia vilikuwa vimeandikwa, havikuwa na milango au aya. Biblia iligawanywa katika milango na aya ili itusaidie kufungua Maandiko kwa haraka na kwa urahisi. Ni rahisi mno kupata "Yohana mlango wa 3, aya ya 16" kuliko kupata "jinsi gani Mungu aliupenda ulimwengu…" Katika sehemu chache, mwisho wa sura zimeekwa vipaya na kwa mjibu wa hiyo ujumbe hauambatani vyema kwa Pamoja. Kwa ujumla, mgawanyiko wa sura na aya unasaidia sana.

Mgawanyiko wa sura unaotumiwa sana hii leo ulianzishwa na Stefano Langton, Archbishop wa Canterbury. Langton aliziweka mgawanyiko wa sura unaotumika hii leo ulianzishwa karibu mwaka wa AD 1227. Biblia ya Kingeresa ya Wycliffe ya mwaka wa 1382 ilikuwa Biblia ya kwanza kutumia mtindo huu wa sura. Tangu kuzinduliwa kwa Biblia ya Wycliffe, takribani tafsiri zote za Biblia zimefuata mgawanyiko wa sura wa Longton.

Biblia ya Kiebrania ya Agano la Kale iligawanywa katika sura na waalimu wa Kiyahudi na Nathan katika mwaka wa AD 1448. Robert Estienne, ambeye pia alikuwa anajulikana kama Setphanus, alikuwa wa kwanza kuigawanya Agano Jipya katika kiwango cha aya mwaka wa 1555. Stephanus kimsingi alitumia mtindo wa wa mgawanyiko wa Nathani wa Agano la Kale. Tangu wakati huo, kuanza na Biblia ya Geneva, mgawanyiko wa sura na aya ulionzishwa na Stephanus umekubalika takribani na matoleo yote ya Biblia.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Ni nani aliigawanya Biblia katika milango na aya? Ni kwa nini na ni linii hili lilifanyika?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries