settings icon
share icon
Swali

Je! Biblia ya Kiyahudi ni gani / Tanakh?

Jibu


Biblia ya Kiyahudi (pia inaitwa Biblia ya Kiebrania au Tanakh) ni neno lingine ambalo Wakristo wanatumia kuita sehemu ya Biblia ya Agano la Kale. Haswa toleo la 1917 la Agano la Kale iliitwa Biblia ya Kiyahudi na ilitayarishwa na chapisho moja la Kiyahudi la Marekani.

Sifa moja mwafaka ya Biblia ya Kiyahudi ni kuwa inagawanya Agano la Kale katika sehemu zake za kitamaduni za Kiebrania. Sehmeu nne ni Pamoja na Kumashi (Chumash) ambavyo ni vitabu vitano vya Musa, Neviim (Manabii), Treisar (Manabii wadogo), na Ketuvim (uandishi). Mpangalio wa vitabu katika Biblia ya Kiyahudi ya mwaka wa 1917 ilijumuisha majina ya Kiebrania vile ifuatavyo:

Chumash / Sheria / Vitabu vitano vya Musa
Bereshit / Mwanzo
Shemot / Kutoka
VaYikra / Walawi
BaMidbar / Hesabu
Devarim / Kumbukumbu

Neviim / Vitabu vya Manabii
Yehoshua / Yoshua
Shoftim / Waamuzi
Shmuel A and B / 1—2 Samweli
Melachim A and B / 1—2 Wafalme
Yishiyah / Isaya
Yermiyah / Yeremia
Yechezchial / Ezekieli
Daniyel / Danieli

Treisar / The Minor Prophets
Hoshea / Hosea
Yoel / Yoeli
Amos / Amosi
Ovadiyah / Obadia
Yonah / Yona
Michah / Mika
Nachum / Nahumu
Habakuk / Habakuki
Tzefaniyah / Sefania
Haggi / Hagai
Zechariyah / Zekaria
Malachi / Malaki

Ketuvim / Mashahiri
Tehilim / Zabiri
Mishlei / Mithali
Eyov / Ayubu

Megilot, hujumuisha:
Shir HaShirim / Wimbo
Ruth / Ruthu
Eichah / Maombolezo
Keholet / Mhubiri
Esther / Esta
Ezra / Ezra
Nechemiyah / Nehemia
Divrei Yamim A and B / 1—2 Mambo ya Nyakati

Kwa muhtasari, Biblia ya Kiyahudi inaweza rejelea Agano la Kale lote au toleo fulani la Agano la Kale mnamo mwaka wa 1917 na Jumuiya ya Uchapishaji ya Kiyahudi. Katika hali nyingi, watu wanatumia neno Biblia ya Kiebrania, Biblia ya Kiyahudi, na Agano la kale kikabala.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Biblia ya Kiyahudi ni gani / Tanakh?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries