settings icon
share icon
Swali

Je! tunawezaje kujua ni lini vitabu vya Biblia viliandikwa?

Jibu


Tunazo njia chache sana za msingi za kujua ni lini vitabu binafsi vya Biblia viliandikwa: mchanganyiko wa ushahidi wa ndani na nje na, haswa katika Agano la Kale, simulizi za jadi.

Ushahidi wa ndani unaweza kuwa na mtindo wa uandishi na kutaja watu au mahali ambao wanaweza kukadiriwa tarehe zao za kuwepo halisi. Kwa mfano, kitabu cha Ruthu kiliandikwa wakati wa waamuzi, wasomi huweka mtindo wa fasihi kama ule wa wakati wa ufalme wa Israeli — Wafalme — kulingana na maandishi mengine yaliyopewa tarehe ya wakati huo. Kutajwa kwa Daudi (Ruthu 4:17, 22) pia kunamaanisha tarehe fulani baada ya wakati wa utawala wa Daudi.

Mfano mwingine: kitabu cha Danieli kinatumia mtindo wa fasihi na maneno maalum ya Kiajemi na Kiyunani ambayo hukiweka karibu na wakati wa Koreshi Mkuu (karibu 530 B.K.). Ushahidi wa kiisimu kutoka kwa hati za kukunjwa za Bahari ya Chumvi hutupa mifano halisi wa maandishi ya Kiebrania na Kiaramu kutoka karne ya pili na ya tatu KK, wakati ambao wengine wanadai Danieli kuandikwa, ambayo hailingani na kile kinachoopatikana katika Danieli, ambayo iliandikwa karne ya sita KK .

Ushahidi mwingine wa kindani unaweza kuwa hoja ambayo mwandishi anashughulikia. Kwa mfano, vitabu viwili vya Mambo ya Nyakati vinasimulia historia ya watu wa Kiyahudi na jinsi walivyokuja chini ya hukumu ya Mungu kwa njia ya uhamisho kwenda Babeli. Kijadi, wasomi wameamini kuwa Ezra ndiye mwandishi wa vitabu hivi, kwa sababu vitabu viwili vinavyofuata, Ezra na Nehemia (pia viliandikwa na Ezra), vinashughulikia kurudi kutoka uhamishoni na hitaji la kutii sheria ya Mungu, na vimeandikwa kwa mtindo ule ule wa fasihi.

Tarehe ya kurudi kwao, ambayo ilianza chini ya Koreshi Mkuu, inaweza kuhusishwa na rekodi za kihistoria nje ya Biblia ambazo zinaweka utawala wake kutoka takriban KK559 hadi 530 KK. Kuwekwa wakfu kwa hekalu jipya huko Yerusalemu, mnamo 516 KK, kunathibitishwa na rekodi za Dario I, na kurudi kwa pili kwa wahamishwa kuliruhusiwa chini ya Artashasta I, ambaye tunajua alitawala Babeli kutoka 465 hadi 424 KK. Vitu hivi vyote hutusaidia kuweka karibu uandishi wa vitabu hivi vya Agano la Kale. Wasomi wa Kibiblia hutumia marejeleo sawia ili kutoa tarehe za uandishi wa vitabu vingine vya Agano la Kale.

Katika Agano Jipya, vitabu kwa jumla vimepangwa tarehe kwa mjibu wa hoja vinaoshughulikia, kwa mfano, uzushi ulijibuka wa Kinostiki, na ni kiasi ambacho wananukuu kutoka kwa vitabu vingine vya Agano Jipya na marejeleo ya matukio kama vile ukusanyaji wa msaada kwa niapa ya waliokuwa na hitaji huko Yerusalemu vile imejadiliwa katika Warumi na Wakorintho wa 1 na 2. Tunayo pia hadithi za kihistoria, simulizi za ziada za kibiblia kama ile ya mwanahistoria Myahudi Flavius Josephus ili kudhibitisha matukio yaliyoelezewa katika Biblia.

Injili mara nyingi zimepewa tarehe kwa kitu ambacho hakikutajwa: Yesu alitabiri kuanguka kwa Yerusalemu katika Mathayo 24: 1-2, na tunajua kutoka kwa wanahistoria kama vile Josephus kwamba mji huo ulianguka mnamo BK 70. Inaonekana kuwa mantiki kwamba ikiwa unabii mashuhuri kama huo ulikuwa umetimizwa kabla ya kuandikwa kwa Injili kwamba ungekuwa umetajwa, kama vile unabii uliotimizwa wa ufufuo wa Kristo kama unavyopatikana katika Yohana 2:19, 22.

Ni muhimu kutambua kwamba hata miongoni mwa wasomi ambao wanaamini Biblia kuwa imevuviwa na Mungu, Neno lisilo na makosa kunao tofauti kuhusu tarehe halisi ya vitabu vya Biblia viliandikwa. Biblia nzuri ya kusoma au ufafanuzi utaweka mistari anuwai ya ushahidi wa tarehe za vitabu viliandikwa.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! tunawezaje kujua ni lini vitabu vya Biblia viliandikwa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries