settings icon
share icon
Swali

Je! Biblia ii kweli?

Jibu


Mantiki huitaji kuwa kuna lengo moja tu "ukweli" kwa madai yoyote maalum. Madai yanayokinzana hayawezi kuwa kweli. Kwa mfano, kauli "buku yumo pangoni" na "na pango la buku liko tupu" haziwezi kuwa kweli wakati mmoja. Tathmini hii ya ukweli inatumika kwa mambo ya kiroho na vile vile mambo ya kimantiki au ya mwili. Ni busara tosha kudai kuwa Biblia ni ya kweli kwa njia yoyote ile inayoweka kando kauli zingine. Ichunguze Bibli njia yoyote ile ile tunaweza kuchunguza andiko linguine, tunaweza kusema kwa ujasiri kuwa kwa kweli ni ya kweli.

Biblia haiwahimizi wasomi kuichunguza imani yao tu pekee (1 Yohana 4:1), lakini pia inawaamuru wale wanaochunguza madai ya kiroho kwa ukweli (Matendo 17:11). Biblia inafanya madai kwa msingi wa historian a mashahidi wa macho (Luka 1:1-4; 2 Petro 1:16), uhunganisha imani na ushahidi unaoonekana (Yohana 20:30-31), na kuunganisha maoni ya kibiblia na ulimwengu unaoonekana (Zaburi 19:1; Warumi 1). Yesu alisema waziwazi kuwa Anawakilisha ukweli wa kipekee (Yohana 18:37; 14:6). Kwa hivyo Biblia imekusudiew kutafsiriwa kuwa kweli, na ukweli wa kipekee (Yohana 17:17).

Ambapo tunaweza kuangalia madai ya kibiblia dhidi ya ukweli unaoweza kuthibitishwa, Biblia inajithibitisha yenyewe kuwa sahihi. Historia, utafiti we vivuzi (akiolojia), sayansi na falsafa zimeonyesha Maandiko kuwa ya kweli na thabiti. Mawasiliano haya kati ya anuwai tofauti ya ushahidi ni manufaa makubwa Biblia inayo dhidi ya maandiko ya madhehebu mengine. Mara nyingi, imekuwa ndio ya kuamua katika kuwakomboa wakosoaji na wasioamini na kuwaleta katika imani katika Kristo.

Iwe au isiwe kuwa Biblia ii kweli ni swali lililo kando na ikiwa kifungu fulani ni "halisi" au la. Ni busara kusema kuwa kifungu au kauli ii kweli, hata kama kweli hiyo haijawasilishwa kwa maneno halisi. Kwa mfano, ikiwa mtu anaweza kusema wakati wa mvua ya masika kuwa "inanyesha mchezo wa paka na panya," kauli hiyo ni ya kweli- lakini sii halisi. Vifungu vya kitendawili imekusudiwa kutafsiriwa. Kanuni yiyo hiyo inatumika kwa maneno ya Yohana kuhusu Yesu: "Tazama, Mwana-Kondoo wa Mungu!" (Yohana 1:36). Mtu anaweza kuuliza ufafanuzi zaidi, na aambiwe, kwa mjibu wa ujumbe wa Agano la Kale, Yesu si mnyama halisi wa shambani aliye na manyoya mengi, lakini Yeye ni utimilifu wa Sheria na dhabihu iliyochaguliwa na Mungu kuukomboa ulimwengu. Hali hii ya mfano ya kauli ya Yohana haifanyi kauli yake kukosa kuwa ya kweli, bali ni mfano tu. Ni vyema kukumbuka kuwa Biblia inajumuisha vitabu sitini na sita vilivyo tofauti, na kila moja yapo kina aina tofauti ya fasihi na mchanganyiko wa fasihi na lugha ya kimajazi.

Hasa kuliko maandishi yoyote ya kidini, tunao uhakikisho kwamba Biblia ii kweli. Mkusanyiko dhabiti wa dani, unaunganisha Ushahidi, na umuhimu wa uzoefu wetu na kuifanya Biblia kuwa ya kipekee kati ya vitabu. Kama kazi zingine nyingi za dini, Biblia inajitangaza kuwa ya kweli (2 Timotheo 3:16). Mbali na kazi zingine za dini, Biblia kwa msisistizo inaunga tangazo hilo.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Biblia ii kweli?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries