settings icon
share icon
Swali

Je, Biblia inasema nini kuhusu bahati?

Jibu


Neno "bahati" linatumika kuelezea kile kinachoaminika kuwa nafasi inayotokea. Mara nyingi "bahati" hutumiwa hasa kuelezea tukio chanya au la kupendeza, au faida ya aina fulani, inaonekana kupitia nafasi. Swali kuu ni, je vitu hutokea kwa bahati? Ikiwa vinafanyika, basi mtu anaweza kuzungumza juu ya mtu kuwa na bahati au bahati mbaya. Lakini ikiwa havitokei kwa bahati, basi haifai kutumia maneno hayo. Mhubiri 9:11-12 inasema, "Nikarudi, na kuona chini ya jua, ya kwamba sisi wenye mbio washindao katika michezo, wala sio walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; lakini wakati na bahati huwapata wote." Mengi ambayo Mhubiri ushiriki ni kutoka kwa mtazamo wa mtu ambaye anaangalia maisha duniani bila ya Mungu, au maisha "chini ya jua." Kutoka kwa mtazamo kama huo-kumwacha Mungu nje ya picha-kunaonekana kuna bahati nzuri na bahati mbaya.

Mkimbiaji katika mbio anaweza kuwa mwepesi zaidi, lakini kwa sababu mtu aliye mbele yake anajikwaa, kukimbia juu yake na kuanguka na hashindi mbio. Je! Bahati mbaya aje kwake? Au mfalme shujaa anaweza kuwa na jeshi la nguvu zaidi lakini kwa "nafasi" fulani mshale unatapwa juu ya hewa bila mpango maalumu na askari wa adui asiye na jina na kutokea tu kuchoma silaha zake katika mahali penye mazingira magumu zaidi (2 Mambo ya Nyakati 18:33) kusababisha kifo cha mfalme huyo na kupoteza vita. Je, ni bahati mbaya aje kwa Mfalme Ahabu? Ilikuwa suala la bahati? Kusoma 2 Mambo ya Nyakati 18 yote, tunaona kwamba Mungu alikuwa na mkono Wake katika suala hilo tangu mwanzo. Askari aliyerusha mshale hakujua kabisa tao la mtupo wake angani, lakini Mungu katika uhuru wake alijua kila wakati ingekuwa maana ya kifo cha mfalme mwovu Ahabu.

Tukio linalofanana "nafasi" hufanyika katika kitabu cha Ruthu. Ruthu, mjane ambaye alikuwa akituza mama mkwe wake mjane, anatafuta shamba la kubuga nafaka ili awape. "Basi akaenda, akaja akaokota masazo kondeni nyuma ya wavunaji; na bahati yake ikamtukia kwamba akaifika sehumu ya shamba iliyokuwa mali yake huyo Boazi, ambaye alikuwa wa jamaa yake Elimeleki"(Ruthu 2:3). Elimeleki alikuwa mume wa mama mkwe wake, Naomi, hivyo Boazi alikuwa jamaa yake na alikuwa mwenye ukarimu kwa Ruthu. Ruthu akirejea nyumbani akiwa na nafaka kubwa zaidi kuliko Naomi alivyotarajia, "Basi mkwewe akamwuliza, Je! Umeokota wapi leo? Umefanya kazi wapi? Na abarikiwe yeye aliyekufahamu. Naye akamwarifu mkwewe ni nani ambaye alifanya kazi kwake, akasema, Yule mtu alifanya kazi kwake leo jina lake aitwa Boaizi. Naye Naomi akamwambia mkwewe, Na abarikiwe huyo na BWANA, ambaye hakuuwacha wema wake, wala kwa hao walio hai wala kwao waliokufa.Kisha Naomi akamwambia, Mtu huyu ni wa mbari yetu, mmojawapo wa jamaa yetu aliye karibu"(Ruthu 2:19-20). Kwa hivyo Naomi hakuiona kama tukio la" bahati" bali kama majaliwa ya Mungu, kama wengine wanavyofanya baadaye (Ruthu 4:14).

Mithali 16:33 inataja kanuni ya jumla: "Kura hutupwa katika mikunjo ya nguo; Lakini hukumu zake zote ni za Bwana." Hii inahusu matumizi kutupa kura (sawa na kurusha sarafu au kubingirisha dadu) kutatua kesi fulani za mahakama. Kesi inayohusiana na Akani katika Yoshua 7 ni mfano ambao kanuni ya Mithali 16:33 hutumiwa kupata chama chenye hatia. Mithali 18:18 inataja kitu kama hicho: "Kura hukomesha mashindano; hukata maneno ya wakuu." Tena, wazo ni kwamba majaliwa ya Mungu yana jukumu la kuamua katika matokeo ya kupiga kura ili migogoro ya mahakama inaweza kutatuliwa bila kujali jinsi ya ukubwa wa ushindano. Mithali 16:33 ingeonyesha kwamba kitu kama kutokuwa na utaratibu maalumu kama kubingirisha dadu au kurusha sarafu si nje ya udhibiti wa uhuru wa Mungu. Na, kwa hivyo, matokeo yake si tu ya bahati.

Mamlaka ya Mungu yanahusisha mambo mawili. Mapenzi hai ya Mungu au uhuru utahusisha kitu ambacho Anasababisha kutokea kama vile kuongozwa kwa Mfalme mwovu Ahabu katika vita (2 Mambo ya Nyakati 18:18-19). Kifo cha Ahabu sio tu matokeo ya mshale uliotupwa bila mpango maalumu, lakini kama 2 Mambo ya Nyakati 18 inavyoonyesha, Mungu aliongoza kikamilifu matukio yaliyoongoza Ahabu katika vita na kutumia mshale huo uliotupwa bila mpango ili kukamilisha mapenzi Yake yaliyokusudiwa kwa Ahabu siku hiyo.

Mapenzi baridi ya Mungu yanahusisha kuruhusu, badala ya kusababisha, kitu kitatokea. Sura ya 1 ya kitabu cha Ayubu inaonyesha hii katika kile ambacho Mungu aliruhusu Shetani kufanya katika maisha ya Ayubu. Pia inahusika katika uovu kwamba Mungu aliruhusu ndugu za Yusufu kumfanyia Yosufu ili kukamilisha mema zaidi, mema yasiyoonekana kwa Yusufu hadi miaka mingi baadaye (Mwanzo 50:20).

Kwa sababu hatujui ukweli unaoletwa kuona kile kinachoendelea mbinguni, hatuwezi kutambua kila wakati ikiwa mapenzi ya Mungu hai au baridi yanahusika katika matukio ya maisha yetu, lakini tunajua kwamba mambo yote yanayotokea yako chini ya mwavuli wa mapenzi Yake, ikiwa hai au baridi, na, kwa hivyo, hakuna suala ni bahati tu. Wakati mtu anabingirisha dadu ili kucheza mchezo wa ubao, Mungu wakati mwingine anaweza kusababisha dadu kuanguka kwa njia fulani, lakini mara nyingi kuliko yalivyo katika masuala kama hayo yasiofuatana, Yeye anaweza ruhusu dadu kuanguka kama sharia Zake za asili zinaweza kuamua bila kujihusisha wowote hai. Lakini hata wakati hajahusishwa vikamilifu, jinsi dadu inavyoanguka bado iko chini ya mamlaka Yake.

Hivyo ni kwa tukio lolote la maisha; bila kujali jinsi lilivyo ndogo (Mathayo 10:29-31) au jinsi lilivyo kubwa (Danieli 4:35; Mithali 21:1), Mungu ni mkuu juu ya wote (Waefeso 1:11, Zaburi 115:3; Isaya 46:9-10), na hivyo hakuna chochote ni suala la bahati tu.

Kutoka kwa mtazamo wa kidunia, mambo yanaweza kuonekana kufanyika bila mpango maalumu, lakini katika Maandiko yote, ni dhahiri kwamba Mungu ana udhibiti wa viumbe Vyake na kwa namna fulani anaweza kuchukua matendo yasio na mpango ya sheria ya asili, mapenzi ya watu wema na waovu, na madhumuni maovu ya pepo na kuunganisha wote ili kutimiza mapenzi Yake mema na kamilifu (Mwanzo 50:20; sura ya 1 na 42 ya Yohana, Yohana 9:1-7). Na Wakristo, hasa, wanapewa ahadi ya kwamba Mungu hufanya mambo yote, iwe ni mzuri au mbaya, pamoja kwa wema kwa wale wanaompenda Yeye na wanaitwa kulingana na kusudi Lake (Warumi 8:28).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, Biblia inasema nini kuhusu bahati?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries