settings icon
share icon
Swali

Baal-zebubu alikuwa nani?

Jibu


Beelzebub ni jina la Kigiriki la Baal-Zebubu, mungu wa kipagani wa Kifilista aliyeabudiwa katika mji wa kale wa Wafilisti wa Ekroni wakati wa Agano la Kale. Ni neno linaloashiria "bwana wa nzi" (2 Wafalme 1: 2). Uchunguzi wa akiolojia katika maeneo ya kale ya Wafilisti ulionyesha picha za dhahabu za nzi. Baada ya wakati wa Wafilisti, Wayahudi walibadilisha jina hilo kuwa "Beelzebuli," kama lilivyotumika katika Agano Jipya la Kigiriki, maana yake ni "bwana wa samadi." Jina hili limeelezea mungu wa nzi ambaye aliabudiwa ili kupata ukombozi kutokana na majeruhi ya wadudu hao. Wataalamu wengine wa kibiblia wanaamini Baal-zebubu pia alijulikana kama "mungu wa uchafu," ambayo baadaye ikawa jina la chuki kali katika kinywa cha Mafarisayo. Matokeo yake, Baal-zebubu alikuwa mungu wa pekee, na jina lake lilitumiwa na Wayahudi kama jina badala ya Shetani.

Neno hilo lina sehemu mbili: Baal, ambayo ilikuwa jina la miungu ya uzazi wa Kanaani katika Agano la Kale; na Zebubu, ambayo ina maana "makao makuu." Kuweka vipande viwili pamoja, ilifanya jina ya Shetani mwenyewe, mkuu wa mapepo. Neno hili lilitumiwa kwanza na Mafarisayo katika kuelezea Yesu katika Mathayo 10: 24-25. Kabla ya hapo, walimshtaki Yesu juu ya kutoa "pepo kwa nguzu za mkuu wa pepo" (Mathayo 9:34), akimaanisha Baal-zebubu (Marko 3:22; Mathayo 12:24).

Katika Mathayo 12:22 Yesu alimponya mtu aliyekuwa na pepo ambaye alikuwa kipofu na bubu. Matokeo yake, "watu wote walishangaa na kusema," Je! Huyu ndiye Mwana wa Daudi? "Lakini Mafarisayo waliposikia haya, walikanusha kuwa hii inaweza kuwa kazi ya Mungu, lakini badala yake walitangaza: ' Huyu hatoi pepo, ila kwa Beelzebuli mkuu wa pepo."(Mathayo 12: 23-24).

Ni ajabu kwamba Mafarisayo walijibu kwa muujiza huu wa ajabu wa Yesu kwa njia tofauti sana na ya ile ya umati, ambao walitambua kwamba Yesu alitoka kwa Mungu. Kwa kweli, Mafarisayo walikubali kwamba Yesu alifanya miujiza au kufanya matendo zaidi ya uwezo wowote wa kibinadamu, lakini walidai nguvu hii ilikukuwa kutoka Beelzebuli badala ya Mungu. Kweli, wanapaswa kuwa wanajua vizuri zaidi: shetani hawezi kufanya kazi za wema. Hata hivyo, katika kiburi chao, Mafarisayo hawa walijua kwamba, ikiwa mafundisho ya Yesu yalipokewa sana na watu, ushawishi wao juu yao ulikuwa ungefika kikomo. Kwa hivyo, hawakukataa muujiza, lakini badala yake walisema ilitokana na nguvu ya ibilisi, "Beelzebuli mkuu wa mapepo."

Swali kubwa ni hili: hii ina maana gani kwetu Wakristo leo? Katika Mathayo 10, Yesu anatupa sisi kiini cha maana ya kuwa mwanafunzi wake. Hapa tunajifunza kwamba Yeye ni karibu kutuma mitume Wake ulimwenguni kuhubiri injili (Mathayo 10: 7). Anawapa maagizo maalum juu ya nini cha kufanya na nini cha kisicho cha kufanya. Anawaonya, "Jihadharini na wanadamu; kwa maana watawapeleka mabarazani, na katika masinagogi yao watawapiga; . . . . nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu"(Mathayo 10:17, 22). Kisha anaongezea, "Mwanafunzi hampiti mwalimu wake, wala mtumwa hampiti bwana wake.Yamtosha mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake, na mtumwa kuwa kama bwana wake. Ikiwa wamemwita mwenye nyumba Beelzebuli, je! Si zaidi wale walio wa nyumbani mwake? "(Mathayo 10: 24-25).

Jambo ambalo Yesu anatufanyia leo ni kwamba, ikiwa watu wanamwita Shetani, kama walivyofanya Mafarisayo wa wakati Wake, bila shaka wangewaita wanafunzi Wake sawia. Katika Yohana sura ya 15 Yesu anasema, "Iwapo ulimwengu ukiwachukia, mwajua ya kuwa umenichukia mimi kabla ya kuwachukia ninyi. Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda walio wake; lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi naliwachagua katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia.

Likumbukeni lile neno nililowaambia, Mtumwa si mkubwa kuliko bwana wake. Ikiwa waliniudhi mimi, watawaudhi ninyi; ikiwa walilishika neno langu watalishika na lenu. Lakini haya yote watawatenda kwa ajili ya jina langu, kwa kuwa hawamjui yeye aliyenituma."(Yohana 15: 18-21).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Baal-zebubu alikuwa nani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries