settings icon
share icon
Swali

Je! Ni muhimu kuchukua aya moja ya Maandiko na kuielezea nje ya muktadha?

Jibu


Kutumia kifungu cha Maandiko nje ya muktadha kunaweza kuelekeza makosani n kutoielewa, ingiwa sio kila wakati. Kunukuu aya moja pekee bila shaka ni kuinukuu nje ya muktadha, lakini hiyo haimaanishi kuwa aya hiyo imetumiwa vibaya. Baadhi "hunukuu nje ya muktadha" na huku aya hudhihirisha ukweli unaojisimamia: wengine huitaji kuzingatia muktadha wa aya hiyo ili kuifasiri vizuri na kuiweka katika matumizi.

Wingi wa usahihi au ubaya wa kunukuu aya moja tu hutegemea dhamira ya mnenaji au mwandhishi. Ikiwa aya moja, imenukuliwa nje ya muktadha imetumika kumaanisha kitu kingine mbali na kile mwandishi alinuia au kupuuza maana nzima ya kufungu, basi ni kutokuwa mwaminifu katika kutumia kifungu hicho. Lakini ikiwa kunukuu aya moja na kunaacha maana kudhihirika na kuheshimu nia ya kifungu, basi ni vyema na sahihi kunukuu aya hiyo. Ingawa aya zinaweza tumika vibaya bila nia mbaya, kwa hivyo ni lazima tuwe waangalifu.

Mfano wa kutumia vibaya kifungu nje ya muktadha ni kunukuu maneno ya Yesu kwenye Luka 12:19, "Pumzika; kula, unywe, ufurahi," na kujaribu kuithibitisha kuwa falsafa ya Yesu kuhusu maisha. Muktadha ambao Yesu anasimulia mfano huu, unafundisha kinyume kabisa na kile maneno hayo yanaonyesha. Kama msimulizi wa hadithi, Yesu anaweka maneno kinywani mwa tajiri mpumbavu, mhusika ambaye atapokea hukumu kutoka kwa Mungu kwa kuishi kwa falsafa kuwa maisha ya anasa ni mema kuishi.

Mfano mwingine wa kutumia vibaya aya nje ya muktadha ni kunukuu sehemu ya kwanza ya Habakuki 2:15 ili kulaani kitendo cha kumpa mtu pombe: "Ole wake yeye awapaye jirani zake kileo." Kutumia aya hii kusema kuwa ni makosa kumpa jirani kileo, mtu huyo anayenukuu aya hiyo anayapadilisha Maandiko. Sehemu aya hiyo iliyosalia ina kihitimisho: "Ole wake yeye awapaye jirani zake kileo, akiimimina kutoka kwenye kiriba cha mvinyo mpaka wamelewa, ili apate kutazama miili yao iliyo uchi!". Dhambi hapa ni ulevi, kujiburudisha kwa kutizama watu wakifanya ngono, tamaa, na unyonyaji wa kijinsia. Fauka ya hayo, uchunguzi wa muktadha wa Habakuki 2:15 unaonyesha kuwa upeanaji wa kileo wafaa kuwa mfano wa dhambi za kitaifa za Babeli.

Katika mifano miwili iliyotangulia, ni dhahiri kwamba aya fulani (au sehemu za aya) haziwezi kufanywa kusimama peke yake na kufundisha somo. Mwanafunzi wa Biblia "ukilitumia kwa usahihi neno la kweli" atakuwa mwangalifu kuepuka mitego kama hiyo ya ufasiri (2 Timotheo 2:15).

Lakini sio vifungu vyote vinavyo tandawa katika utumiaji nje ya muktadha. Kuna matukio ambayo tunaweza kutumia aya moja au hata sehemu ya aya yenyewe na bado tuitendee haki kwa kusudi la kimungu ililo nalo. Kwa mfano, ikiwa tunajaribu kumwambia mtu kwamba wokovu ni zawadi kutoka kwa MUNGU, tunaweza kutumia Yohana 3:16: "Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele." Kwa kweli hii ni aya ambayo inajisimamia pekee yake. Inasema wazi inachosema, na hata uielewa kijuu juu aya hiyo yenyewe humfanya mtu kuamini kwa mjibu wa muktadha wa Yohana 3.

Kwa muhtasari, kunukuu Andiko moja "nje ya muktadha" inaweza kuwa vyema wakati mwingine; na wakati mwingine ni shida. Ikiwa matumizi yetu ya aya, bila muktadha wake kunapendekeza maana tofauti na kile kifungu pana kinaidhinisha, basi ni makosa. Wakati wowote tunaposoma au kumsikia mtu akitumia aya moja tu bila zingine, ni vyema kuipajika aya hiyo kwenye kifungu chake cha asili ili kuona ikiwa bado inaingilia na tafsiri ilikusudiwa.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Ni muhimu kuchukua aya moja ya Maandiko na kuielezea nje ya muktadha?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries