settings icon
share icon
Swali

Kwa nini niamini Biblia? Biblia inaweza kuaminika?

Jibu


Sisi sote tunaamini kitu. Hata watu wenye wasiwasi kati yetu huamini katika mambo mengi. Tunaposimama, tunaamini kwamba miguu yetu itatushikilia. Tunapoketi, tunaamini kiti. Tunaamini kwamba, tunapovuta pumzi, tunapata kiwango kizuri cha oksijeni cha kututegemeza. Tunapolala, tunaamini kwamba dunia itaendelea kuzunguka na kwa hivyo asubuhi itafika. Tumechagua kuweka imani kwa mambo haya kwa sababu ya uaminifu wao wa zamani. Tunachagua kutumaini, na kama sivyo basi tungeishi katika hali ya hofu na kutokuwa na uhakika.

Wakati inapofikia ni suala la Mungu na Biblia, kanuni zizo hizo zinatumika. Tunachagua kile tunachokiamini. Imani katika Mungu inamaanisha kwamba tumechagua kuamini kwamba Yeye yuko, kwamba Yeye ndiye ambaye Biblia inasema kuwa Yeye ndiye, na kwamba imani yetu — au ukosefu wake — utaathiri sana maisha yetu na umilele. Walakini, njia mbadala ielekezay kwa imani sio "ukosefu wa imani." Kuchagua dhidi ya imani katika Mungu pia kunahitaji imani. Lazima tuamini kwamba Mungu hayupo, kwamba hawezi hatuwezi kumjua, na kwamba chaguo hili haliathiri maisha yetu na umilele yetu. Kukataa kuwepo kwa Mungu kunachukua imani kubwa zaidi kwa sababu maswali yaliyoulizwa katika Biblia bado yanahutaji kujibiwa. Wale ambao hupuuza Biblia lazima kutoa majibu yao wenyewe kwa maswali mengi ambayo hanya majibu aliyo tayari, kama vile yale yanayoshughulikia kusudi la uhai na ugumu wa muundo wa ajabu wa ulimwengu. Wengi wanaochagua kuamini kitu kingine isipokuwa Biblia lazima mwishowe wakubaliane na mtu asiyeamini kuwa kuna Mungu Bertrand Russell, ambaye alihitimisha kuwa, ikiwa maisha zaidi ya kaburi ni hadithi, basi maisha kabla ya kaburi hayana maana.

Wakati tunachagua mahali pa kuweka imani yetu, lazima tuzingatie kusadikia kwa kila chaguo. Biblia inafanya madai ya kushangaza juu yake. Watu wengine hufikiri wanaweza kuchagua ni sehemu gani za Bibilia wanazoona ni za kweli, lakini Kitabu chenyewe hakijawahi kutupa chaguo hilo. Inasema kwamba ni Neno la Mungu lililovuviwa (2 Timotheo 3:16), hiyo ni kweli (Zaburi 119: 160; Yohana 17:17), na kwamba ndicho kitabu cha mwongozo wa maisha yetu (Zaburi 119: 105; Luka 4: 4). Kusadiki kuwa hilo sio la kweli inamaanisha kuwa kila kitu kingine ambacho Biblia inasema ni cha kutuhumiwa; kwa hivyo, kudai ahadi huku ukipuuza amri sio jambo la busara.

Kutangaza kwamba Biblia haiaminiki inamaanisha kuwa lazima tupate maelezo mengine yanayofaa kuhusu asili yake ya miujiza. Kwa mfano, takribani unabii 2,500 uliotolewa katika Biblia, mamia au maelfu ya miaka mbeleni, 2,000 ya unabii huo umetimizwa, na 500+ uliobaki unaendelea kadri na wakati unavyosonga. Uwezekano wa unabii huu wote kutimizwa bila makosa ni takriban moja kati ya 1020000. Kwa hivyo, kusadiki kwamba Biblia sio kitabu cha miujiza ni kinyume kihesabu.

Kuna mambo kadhaa ya kuzingatia katika kuamua uaminifu wa Biblia, la kwanza likiwa ni kauli isiyopingika kwamba Biblia ii kweli kwa sababu inasema ni kweli. Kwa kweli itakuwa upumbavu msingi wa Imani ukiwa juu sababu peke yake. Hatuwezi kabidhi kitabu chetu cha hundi kwa mgeni ambaye anasema tunaweza kumwamini kwa sababu anaaminika. Lakini tunaweza kuanza na madai ya Biblia ya kuaminika kwa Biblia na kisha tutafute ushahidi unaounga mkono ili kuyathibitisha.

Kinachoweza kutusaidia kuisadiki Biblia ni madai ya waandishi wenyewe. Waandishi wa Agano la Kale walitangaza kwamba walinena maneno ya Mungu (Kutoka 20: 1–4; Kumbukumbu 8: 3; Isaya 1: 2; Yeremia 1: 1–13). Wanaume fulani waliteuliwa na Mungu kama manabii, wafalme, au viongozi na walitambuliwa hivyo na watu waliowahudumia. Manabii walithibitisha matamko yao mengi kwa maneno, "Ndivyo asema Bwana" (kwa mfano, Yeremia 45: 2; Zekaria 7:13). Tamko hili mara nyingi lilikumbwa na uasi na mateso (Mathayo 23:37; 1 Wafalme 19:10; Matendo 7:52). Hakukuwa na sababu yoyote ya kidunia ya nabii kutangaza habari mbaya kwa watu ambao wangeweza kumpiga mawe. Walakini, manabii waliendelea kuutangaza ujumbe wao kwa sababu walikuwa na uhakika thabiti kwamba Bwana aliwehesabia waibu katika kumwakilisha Yeye kwa uaminifu. Maneno ya manabii kisha yakarekodiwa kwa vizazi vijavyo na kukubaliwa kama maneno ya Mungu, hata na Yesu mwenyewe (Mathayo 4:10; Luka 4: 8).

Waandishi wa Agano Jipya walitambua sababu anuwai za kuandika. Luka, kwa mfano, alikuwa daktari na mwanahistoria aliyeheshimiwa na ambaye alisafiri na Paulo katika safari zake za umishonari. Anaelezea kusudi la kitabu chake katika sura ya kwanza: "kama vile yalivyokabidhiwa kwetu na wale waliokuwa mashahidi walioyaona na watumishi wa Bwana, 3mimi nami baada ya kuchunguza kila kitu kwa uangalifu kuanzia mwanzo, niliamua kukuandikia habari za mambo hayo, ewe mtukufu Theofilo, 4ili upate kujua ukweli kuhusu yale uliyofundishwa" (Luka 1: 2–4). Luka alitafiti kibinafsi madai juu ya Yesu ili kudhibitisha ukweli wa hadithi ya injili na akaandika vitabu vya Luka na Matendo.

Barua za Paulo kwa makanisa zilipokelewa na hadhiria iliyokusudiwa kama ile iliyotoka kwa Bwana (1 Wathesalonike 2:13). Ni muhimu pia kutambua kwamba waandishi wengi wa Agano Jipya waliuawa kwa ajili ya maneno yao. Haiwezekani kwamba watu wengi kama hao, wote wakiutangaza ukweli mmoja, wangepata kuteswa mno na mwishowe kuuawa kwa maneno ambayo walijua kuwa ni uwongo.

Jambo lingine linalotusaidia kuisadiki Biblia ni mbadiliko wa maisha ambayo Biblia imekuwa nayo kwa maelfu ya miaka. Biblia imehimili majaribio ya wafalme, madikteta, na jamii nzima iliyonuia kuiangamiza Biblia na bado Biblia inabaki kuwa kitabu kinachouzwa zaidi kuliko vitabu vyote nyakati zote. Maneno yake yana tumaini ambalo halipatikani katika maandishi mengine yoyote ya kidini na imebadilisha maisha ya mamilioni. Dini zingine za ulimwengu zinadai kufuata kwa uaminifu, lakini gundi inayowaghubika waamini wao ni hofu, vitisho, au juhudi za kibinadamu. Biblia inaahidi kile ambacho hakuna kitabu kingine kinaweza kuahidi: maisha, tumaini, na kusudi kama karama kutoka kwa Mungu Mweza-Yote. Maneno yake yamebadilisha wauaji, madhalimu, na mataifa kwa sababu Biblia inajidhihirisha kuwa ukweli katika sehemu ya ndani kabisa ya roho ya mwanadamu (Mhubiri 3:11). Biblia inaweza kukataliwa, kuchukiwa, au kupuuzwa, lakini ushawishi wake kwa wale wanaoitii hauwezi kupuuzwa.

Mwishowe, Mungu amempa kila mmoja wetu hiari ya kuchagua kile tunachoamini. Lakini pia ameweka alama za vidole vyake katika uumbaji wake wote, na Ameandika mwongozo ili tuweze kujua jinsi ya kuishi (Zaburi 19: 1; 119: 11; 1 Petro 2: 11-12). Neno lake limetupa ushahidi wa kutosha kwamba linaweza kuaminika, na wale wanaoiamini Biblia wana msingi thabiti wa kujenga maisha yao juu yake (ona Mathayo 7: 24–28).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kwa nini niamini Biblia? Biblia inaweza kuaminika?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries