settings icon
share icon
Swali

Ni wapi usemi 'Amefufuka; hakika Amefufuka' unatoka?

Jibu


Salamu ya jadi ya Pasaka katika kanisa la Magharibi ni msemo wa ghafula "Amefufuka!" na mwitikio wa jadi ni "hakika Amefufuka!" meneno hayo wakati mwingine hufuatanishwa na mbadilishano wa busu tatu kwa mashavu, huku ikitegemea kanisa mtu anaishiriki. Katika makanisa ya Dini sahihi na Katholiki salamu hiyo inaitwa "salamu ya Pasaka" na tamaduni ya tangu jadi.

Salamu hiyo mwishoye msingi wake ni Luka 24:34. Tafsiri zote katika historia yote ya kanisa, kutoka Biblia ya Kilatini (takribani AD 400) hadi ESV (Tafsiri ya Kiwango ya Kingeresa) ya mwaka wa (2001) imetafsiri ayah ii vivyo hivyo: "Bwana amefufuka kweli kweli, naye amemtokea Simoni!" namna msemo ulikuwa salamu ya kiwango katika kanisa haijulikani, ingawa kunazo dhana mbali mbali kuhusu jinsi ilivyoanza kutumika na watu wote.

Tunajua kwamba, mwanzo, salamu ilikuwa jambo la kawaida katika ibada ya Mashariki ya utawala wa Kirumi kuliko ilivyokuwa katika kanisa la Magharibi. Kunayo tamaduni katika kanisa la Mashariki kwamba msemo huo ulifanyia maarufu na Mariamu Magdalena wakati anakisiwa kumhutubia Mfalme Teberius huko Rumi kwa maneno "Kristo amefufuka."

Kutumia aina hii ya kuhutubia inapaswa kuwa zaidi ya utamaduni tupu. Maneno "Amefufuka!" yanatukumbusha Habari njema ya furaha tunayoadhimisha wakati wa Pasaka, kwamba kifo cha Yesu hakikuwa cha bure, na kwamba anazoa nguvu za kuyashinda mauti. Kusema "Amaefufuka!" inaturuhusu kushiriki ukweli huu wa ajabu na kila mmoja wetu. Ufufuo wa Kristo unatupa tumaini la wokovu na tumaini la ufufuo wetu na uzima wa milele.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni wapi usemi 'Amefufuka; hakika Amefufuka' unatoka?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries