settings icon
share icon
Swali

Je! Kuna uwezekano mtu kupata alama ya mnyama hii leo?

Jibu


Alama ya mnyama ni aina ya muhuri ambayo wafuasi wa Mpinga Kristo watachukua ili kuonyesha kiapo kwake. Unabii wa ufunuo 13: 16-17 unasema kwamba alama ya mnyama “Pia alimlazimisha kila mmoja, mdogo na mkubwa, tajiri na maskini, mtu huru na mtumwa, atiwe chapa kwenye mkono wake wa kuume au kwenye kipaji chake cha uso, 17 ili kwamba mtu yeyote asiweze kununua wala kuuza isipokuwa amekuwa na hiyo chapa, ambayo ni jina la huyo mnyama au tarakimu za jina lake..”

Hatujui hii alama itaonekana namna gani. Kitambo kidogo, watu wengine walidhani ni muhuri au mchoro wa nambari 666. Ivi karibuni, watu walidhani inaweza kuwa ni nambari katalakilishi. Sasa uvumi unao enea ni kwamba alama ya mnyama itakua microchipu (kijipande cha silikoni chenye sakiti changamano ya elektroniki) ambacho kitapandikizwa kwa binadamu ili waweze kufikia sarafu au mali yao ya kidijitali. Lakini kwa kweli hatuna njia yoyote ya kujua alama ya mnyama itachukua umbo gani.

Watu wengine wanaogopa kwamba tayari washapokea alama ya mnyama. Huenda walimfukuru mungu wakati fulani au walitoa kauli fulani ya msukumo ya utii kwa Mpinga Kristo. Wanaweza kuwa na wasiwasi kuhusu kifaa ambacho kiko katika kadi zao za mikopo. Wengine wameambiwa kwamba kitendo chao cha kumwabudu Bwana siku ya jumapili badala ya sabato kinahusisha kukubali alama ya mnyama. Kuna sababu moja muhimu inayofanya ikue vigumu kupata alama ya mnyama sasa.

Alama ya mnyama bado haijakuwapo.

Usomaji halisi/kawaida wa Ufunuo na nabii zingine za nyakati za mwisho katika Biblia unaonyesha kuwa kuna mpangilio wa matukio ya siku za mwisho. Danieli alitabiri wiki sabini (seti sabini za miaka saba) ambazo zinaonyesha nyakati ambazo mungu aliingiliana na wanaisraeli. Wiki sitini na tisa kati ya hizo zimepita tangu kuandikwa kwa Danieli. Wiki ya mwisho itakua ya dhiki, yaani, wakati Mpinga Kristo, au mnyama, atatua mamlakani. Mtawala huyu ataunganisha mataifa kumi (Danieli 7:24-25; Ufunuo 17:7) na kufanya mapatano ya udanganyifu na Israeli (Danieli 9) .Alama ya mnyama haiwezi kuwepo mpaka mnyama mwenyewe awe na mamlaka wakati wa dhiki.

Sababu nyingine ya kuwafanya waumini wa Yesu Kristo wasiogope kupata alama ya mnyama sasa ni unyakuzi wa kanisa. Katika unyakuo, Yesu atawachukua waumini wote, walio hai na wafu, kutoka duniani (1 Wathesalonike 4:13-18; 1 Wakorintho 15:50-54). Ingawa watu bado watamjua Kristo baada ya unyakuo, wale wote wanaomwamini yesu kabla ya unyakuo watachukuliwa na kuwa pamoja na Bwana. Kulingana na imani kuwa kutakuwa na dhiki kabla, waumini ambao wanaishi katika enzi ya kanisa hawatapata fursa ya kupokea alama ya mnyama.

Kwa ivyo, hakuna kitu ambacho mtu anaeza fanya ivi leo ili kupata, kuchukua, au kupokea alama ya mnyama. Vifaa za kuwekwa (microchips), nambari za mashine, michoro, kukufuru, akiongea kwa sauti kubwa, “ninamfuata mpinga kristo na kukubali alama ya mnyama”- hakuna kati ya izi zinaweza kukupea alama ya mnyama. Alama ya mnyama haiwezi kuwepo bila “mnyama” au mpinga kristo kuitaka.

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Kuna uwezekano mtu kupata alama ya mnyama hii leo?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries