settings icon
share icon
Swali

Agano la Daudi ni nini?

Jibu


Agano la Daudi linamaanisha ahadi za Mungu kwa Daudi kupitia Nathani nabii na hupatikana katika 2 Samweli 7 na baadaye ikafupishwa katika 1 Mambo ya Nyakati 17: 11-14 na 2 Mambo ya Nyakati 6:16. Hili ni agano lisilo na masharti lililofanyika kati ya Mungu na Daudi kwa njia ambayo Mungu ameahidi Daudi na Israeli kwamba Masihi (Yesu Kristo) atakuja kutoka kwa uzao wa Daudi na kabila la Yuda na ataanzisha ufalme ambao utaendelea milele. Agano la Daudi ni lisilo na masharti kwa sababu Mungu haweki hali yoyote ya utii juu ya kutimiza kwake. Uhakikisho wa ahadi zilizowekwa hutegemea uaminifu wa Mungu na haukutegemea kabisa katika utii wa Daudi au Israeli.

Agano la Daudi linazingatia juu ya ahadi kadhaa muhimu ambazo Daudi anapewa. Kwanza, Mungu anathibitisha ahadi ya nchi aliyoifanya katika maagano mawili ya kwanza na Israeli (maagano ya Ibrahimu na Palestina). Ahadi hii inavyoonekana katika 2 Samweli 7:10, "Tena nitawaagizia mahali watu wangu Israeli, nami nitawapanda wapate kuaka mahali pao wenyewe, wasiondolewe tena wala wana wa uovu hawatawatesa tena kama hapo kwanza . "Mungu kisha ameahidi kwamba mwana wa Daudi atamridhi Daudi kuwa mfalme wa Israeli na kwamba mwana huyu (Sulemani) atajenga hekalu. Ahadi hii inaonekana katika 2 Samweli 7: 12-13, "Nitainua mzao wako nyuma yako,atakayetoka viunoni mwako, nami nitaimarisha ufalme wake, naye ndiye atakayejenga nyumba kwa Jina langu. "

Lakini basi ahadi inaendelea na kueneza: "Nacho kiti cha enzi cha ufalme wake nitakifanya imara milele" (2 Samweli 7:13), na "Nyumba yako na ufalme wako vitathibitishwa milele mbele yako; nacho kiti chako cha enzi kitafanywa imara milele "(mstari wa 16). Kenye kilianza kama ahadi ya kwamba mwana wa Daudi, Sulemani atabarikiwa na kujenga hekalu linageuka kuwa kitu tofauti-ahadi ya ufalme wa milele. Mwana mwingine wa Daudi angeweza kutawala milele na kujenga Nyumba ya kudumu. Hii ni kumbukumbu ya Masihi, Yesu Kristo, aliyeitwa Mwana wa Daudi katika Mathayo 21: 9.

Ahadi ya kwamba "nyumba" ya Daudi, "ufalme" na "kiti cha enzi" vitafanywa kuwa milele ni muhimu kwa sababu inaonyesha kwamba Masihi atakuja kutoka kwa uzao wa Daudi na kwamba ataanzisha ufalme ambao atatawala. Agano hili limefupishwa kwa maneno "nyumba," kuahidi nasaba katika kizazi cha Daudi; "Ufalme," kurejelea watu wanaoongozwa na mfalme; "Kiti cha enzi," kusisitiza mamlaka ya utawala wa mfalme; na "milele," kusisitiza asili ya milele na isiyo na masharti ya ahadi hii kwa Daudi na Israeli.

Marejeo mengine ya agano la Daudi yanapatikana katika Yeremia 23: 5; 30: 9; Isaya 9: 7; 11: 1; Luka 1:32, 69; Matendo 13:34; na Ufunuo 3: 7.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Agano la Daudi ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries