settings icon
share icon
Swali

Je, dini ni afyuni kwa umma?

Jibu


Kutaja Ukristo (na/au dini nyingine) "afyuni kwa watu" au "dawa ya umma" ni mbinu ya kawaida kwa kiasi inayotumiwa na wale wanaopuuza dini. Kutumia maneno kama hii ni njia ya kupiga dini bila kujaribu kukanusha au kuizungumza. Karl Marx siye wa kwanza kutumia maneno haya, lakini yeye ndiye watu wengi wanamfikiria wakati wanatumia shambulio hili. Ugomvi wa Marx ulikuwa kwamba dini huwapa watu furaha ya bandia, ya uongo-kama vile afyuni hufanya kwa mlevi wa madawa-na kuwakomboa watu kutokana na uongo huo usiofaa ilikuwa sehemu ya kujenga jamii bora.

Kuanzia hasa na Marx, mashtaka ya "afyuni kwa umma" mara nyingi hutumiwa na wakanamungu. Kwa sababu wanakataa kuwepo kwa Mungu, kwa namna fulani wanaelezea kuendelea kuwepo kwa dini. Hawaoni haja ya dini, kwa hivyo hawaelewi haja ya wengine kwa dini. Marx hakuwa akielezea bayana Ukristo katika kukataa kwake dini. Badala yake, alikuwa akikataa dini kwa ujumla kwa kutumia "watu" kwa namna ya kudharau kumaanisha maskini, wasiojua, na kudanganywa kwa urahisi. Hoja muhimu ya "afyuni kwa umma" kusema ni kwamba dini ni kwa watu wenye akili chache na kihisia wanaochanganyikiwa ambao wanahitaji tegemeo kufaulu maisha. Wakanamungu leo wanafanya madai kama hayo, kama vile wazo kwamba "Mungu ni rafiki wa kufikirika kwa watu wazima."

Hivyo, dini si chochote bali "afyuni kwa umma"? Je! Dini haitimizi chochote bali kutoa tegemeo la kihisia kwa watu wenye akili dhaifu? Ukweli chache rahisi utajibu swali kwa mvuvumo "hapana." (1) Kuna hoja mantiki yenye nguvu, kisayansi, na falsafa za kuwepo kwa Mungu. (2) Ukweli kwamba ubinadamu umeharibiwa na unahitaji ukombozi/wokovu (ujumbe wa msingi wa dini) unaonekana wazi duniani kote. (3) Katika historia ya ubinadamu, wengi wa waandishi wenye akili zaidi na wenye fikira nyingi wamekuwa waumini wa Imani kuwa Mungu yupo na ni muumba na mtawala wa dunia. Je! Wengine wanatumia dini kama tegemeo? Ndiyo. Je! Hiyo inamaanisha madai ya dini ni batili? Hapana. Dini ni jibu la asili kwa ushahidi wa kuwepo kwa Mungu na kutambua kwamba tumeharibiwa na tunahitaji ukarabati.

Wakati huo huo, ni lazima tufautishe kati ya dini ya uongo ambayo inatoa usalama wa uongo-kama vile afyuni inatoa hisia ya uwongo ya ustawi-na Ukristo, ambayo ni dini pekee ya kweli na tumaini la pekee la kweli kwa wanadamu. Dini ya uwongo inategemea wazo kwamba mtu, kupitia kwa aina fulani ya jitihada kwa upande wake (kazi) anaweza kujifanya mwenyewe kukubalika kwa Mungu. Ukristo tu hutambua kwamba mtu "amekufa katika makosa na dhambi" na hawezi kufanya chochote kinachostahili milele mbinguni. Ukristo tu hutoa suluhisho la kutoweza kabisa kwa mwanadamu-badala ya kifo cha Yesu Kristo msalabani.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, dini ni afyuni kwa umma?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries