settings icon
share icon
Swali

Je! Biblia inaunga mkono sayansi ya kustawisha wanadamu?

Jibu


Yujeniki ni vuguvugu la kijamii linalounga mkono uboreshaji wa idadi ya watu kupitia ufugaji wa kuchagua na njia zingine. Mbeleni lilianzishwa na Francis Galton, binamuye Charles Darwin, na kwa msingi wa nadharia ya Darwin ya mageuizi. Neno sayansi dhibiti (yujeniki) kiahalisi humaanisha “kuzaliwa vizuri” na linatokana na neno la Kigiriki linalomaanisha “kuzaliwa vizuri, mwenye hisa nzuri, wa jamii ya kifahari.” Lengo la Yujeniki ni kufanya ulimwengu (au angalau nchi) kuwa mahali pazuri kwa kuongoza njia ya uzazi na “kusafisha” chembe kundi.

Yujeniki hutetea uchunguzi wa maumbile, udhibiti wa kuzaliwa, ubaguzi, na sayansi ya kuboresha maisha ya mwanadamu, kifo cha huruma (eutanasia), kufunga kizazi kwa kulazimishwa, mimba ya lazima, na uavyaji mimba. Yujeniki ilifanywa kwa wazi katika karne za mapema ya 20 katika nchi nyingi, ikiwa ni pamoja na Marekani. Sheria kadhaa za serikali zilipatishwa kuruhusu kulazimishwa kufunga kizazi kwa watu waliowekwa kitaasisi. Sheria kama hiyo katika mji wa Virginia iliponea pingamizi mahakamani, huku Hakimu wa Mahakama Kuu Oliver Wendell Holmes, Jr., akiandika katika uamuzi huo, “Ni bora kwa ulimwengu wote, ikiwa badala ya kungoja kuwaua watoto waliopotoka kwa uhalifu, au kuwaacha njaa kwa ajili ya upumbavu wao, jamii inaweza kuwazuia wale ambao kwa uwazi kabisa hawafai kuendelea na aina yao” (Buck dhidi yake Bell, Mahakama Kuu, 274 U.S. 200, iliamua mnamo Mei 2, 1927). Baada ya Vita vya Pili vya Kidunia, yujeniki kwa jina hilo lilikosa kupendeza watu sana wakati wa ukatili mkubwa wa Nazi ulipojulikana.

Margaret Sanger, mwanzilishi wa Uzazi wa Kupanga, mtekelezaji mkuu wa kuavya mimba wa Marekani, pia alikuwa mtetezi wa yujeniki. Sanger alikosoa vikali “uzalishaji usio na mpango”na “usiofaa.” Katika kitabu chake Mwanamke na kizazi kipya (Woman and the New Race) aliandika, “Jambo la rehema sana ambalo familia kubwa hufanya kwa mmoja wa washirika wake wachanga ni kumuua” (Sura ya V, “Ubaya wa kuanzisha family kubwa/The Wickendess of Creating Large Families,” 1920). Alitamani “kuzalisha jamii ya watu wa asili” na afadhali jamii “izalishe mifugo elfu moja kuliko milioni zilizodumaa” (Redio WFAB Syracuse, Februari 29, 1924, iliyonakiliwa katika “Maana ya Udhibiti wa Uzazi wa Redio (The Meaning of Radio Birth Control),” Aprili 1924, Uk. 111).

Biblia haitaji yujeniki moja kwa moja, lakini dhana iliyo nyuma ya yujeniki- kwamba mwanadamu anaweza kujiboresha kwa kuondoa ulimwengu watu (wasiohitajika”-hakika sio la kibiblia. Na mitindo inayoungwa na yujeniki, ni pamoja na kuavya mimba, kifo cha huruma, na ubaguzi wa kizazi, ni matendo maovu. Mungu alimwambia mwanadamu “azae na kuongezeka” (Mwanzo 1:28; 9:1,7). Hakuna ubaguzi katika amri hiyo ambayo imetolewa katika Maandiko, na hakika hakuna marekebisho ya kizazi/rangi kwa amri hiyo ambayo imependekezwa popote katika Biblia. Kwa waandisi wa masuala ya jamii kutwaa mamlaka ya Mungu juu ya maisha na kifo ili waunde “kizazi bora zaidi” ni dhambi. Kibiblia kunacho kizazi moja-kizazi cha mwanadamu-huku kila mmoja akiwa ametoka kwa Adamu na Hawa. Ubaguzi wa rangi ubora wa kikabila unaenda kinyume na asili ya Mungu: “Mungu hana upendeleo, 35 Lakini katika kila taifa, kila mtu amchaye na kutenda yaliyo haki hukubaliwa naye (Matendo 10:34-35).

Mwanatheolojia Mwingereza G. K. Chesterton aliandika katika kitabu chake cha Yujeni na maovu mengine(Eugenics and Other Evils) mnamo mwaka wa 1922, “Hakuna sababu katika Yujeniki, lakini kunalo wingi wa nia. Wanaounga mkono hawana uwazi sana kuhusu nadharia yake, lakini wataonyesha vitendo vyake kwa uchungu” “A Summary of a False Theory” (kutoka Sura ya 8, “Muhtasari wa Nadharia ya Uongo”). Kwa kuwa mazoezi hayo yanahusisha uavyaji mimba na kifo cha huruma, kwa ufupi yujeniki ni mauaji.

Yujeniki kwa kawaida haitumii jina hilo hii leo, lakini falsafa yake msingi bado ni dhahiri katika matibabu ya maumbile. Uchunguzi wa maumbie hii leo na uharibifu wa jeni ya kujusi ndio aina ya yujeniki iliyosalia. Wakati kasoro imegunduliwa kwa kijusi, baadhi ya wanandoa huamua kuavya mimba. Watoto ambao hawajazaliwa walio na dalili za upungufu ni mojawapo ya mfano: katika nchi ya Marekani, inakadiriwa asilimia 67 ya watato ambao hawajazaliwa wamegunduliwa kuwa na kasoro, wanobeba mimba huavya; katika Ufaransa ni asilimia 77, katika taifa la Udeni (Denmark) ni asilimia 98; Isilandi karibu asilimia 100 (“Ni katika aina gani ya jamii ungependa kuishi? Katika nchi ambayo ugonjwa wa Down syndrome unaisha,” cbsnews.com/news/down-syndrome-iceland, ilianza kusomwa mnamo 6/22/20). Ni yujeniki kwa jina lingine tofauti huku watu wanapoendelea kujaribu kutambua na kuangamiza nyenzo za kijeni wanazoziona kuwa “hazifai” au hazipendezi.

Yujeniki ni jaribio lisilofaa na lisilo la maadili ya uhandisi wa kijamii. Ni njia telezi ambayo wafuasi sugu wa kisayansi Chesterton hutwaa mamlaka ya Mungu na kutafuta kuunda jamii kamili duniani. Karne zilizopita, Ayubu aliomboleza maovu ya siku zake: “Wakati mwanga wa mchana unapotoweka, muuaji huinuka naye huwaua maskini na mhitaji; wakati wa usiku hunyemelea kama mwizi” (Ayubu 24:14). Hili ndilo jukumu la yujeniki: kuua maskini na wenye mahitaji na wale inaowaona kuwa “sio wa maana,” ikizuia “ubora duni wa maisha” (katika makadirio yake) kwa kuchukua maisha, kuwanyima watu uhuru wao na kumfanyia Mungu mzaha.

Siku moja Yesu alipokuwa akipita na wanafunzi wake Yerusalemu, wanafunzi Wake wakamuuliza kuhusu mtu aliyezaliwa kipofu. Walitaka kujua “ni nani aliyetenda dhambi, ni huyu mtu au wazazi wake hata azaliwe kipofu?” (Yohana 9:2). Yesu aliwajibu, “Huyu mtu wala wazazi wake hawakutenda dhambi. Alizaliwa kipofu ili kazi za Mungu zidhihirishwe katika maisha yake” (mstari wa 3). Sisi ndio nani ili tuamue ni nani anaonyesha au haonyeshi kazi ya Mungu?

Kwa kulinganisha yujeniki, Biblia inatuambia tuwatetee wanyonge na wasiojiweza: “Mwokoeni mnyonge na mhitaji, wakomboeni kutoka mkononi mwa mwovu” (Zaburi 82:4); “Heri mtu yule anayemjali mnyonge, Bwana atamwokoa wakati wa shida (Zaburi 41:1; angalia pia Mathayo 25:35-36; Matendo 20:35). Kuwaua wasiojiweza, kuwakusanya wale ambao waliobahatika wanaamua kuwa “hawafai” maishani, au kuwaondoa wanyonge ni kutomcha Mungu kabisa.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Biblia inaunga mkono sayansi ya kustawisha wanadamu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries